Kumbukumbu 30:11-20, Kumbukumbu 31:1-29 NEN

Kumbukumbu 30:11-20

Uzima Na Mauti

30:11 Za 19:8; Isa 45:19-23; 63:1Ninachokuagiza leo sio kigumu sana kwako au usichokiweza. 30:12 Mit 30:4; Rum 10:6; Yn 3:13Hakiko juu mbinguni, ili uulize, “Ni nani atakayepanda mbinguni kukileta na kututangazia ili tuweze kutii?” 30:13 Ay 28:14; Rum 10:7Wala hakiko ngʼambo ya bahari, ili uulize, “Ni nani atakayevuka bahari kwenda kukichukua na kututangazia ili tupate kutii?” 30:14 Kum 6:6; Rum 10:8La hasha! Lile neno liko karibu sana nawe; liko kinywani mwako na ndani ya moyo wako ili uweze kulitii.

30:15 Mit 10:16; 11:9; 12:28; 3:1-2; Kum 28:11; Za 25:13; 106:5; Mwa 2:17; Kum 11:26Tazama, naweka mbele yako leo uzima na mafanikio, mauti na maangamizo. 30:16 Kum 6:5; 4:1; 32:17; Neh 9:29Ninakuamuru leo kwamba umpende Bwana Mungu wako, utembee katika njia zake, na kutunza maagizo yake, amri na sheria zake; ndipo utakapoishi na kuongezeka, naye Bwana Mungu wako atakubariki katika nchi unayoingia kuimiliki.

Lakini kama moyo wako ukigeukia mbali ukawa huna utii, kama umevutwa kuisujudia miungu mingine na kuiabudu, 30:18 Kum 8:19nakutangazia leo hii kwamba hakika utaangamizwa. Hutaishi maisha marefu katika nchi unayovuka Yordani kuiingia na kuimiliki.

30:19 Kum 4:26; 11:26Leo ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yako kwamba nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana. Basi sasa chagueni uzima, ili wewe na watoto wako mpate kuishi, 30:20 Kum 6:5; 4:1; 8:3; 32:47; 10:20; Za 27:1; Yn 5:26; Mdo 17:28; Mit 3:22; Mwa 12:7; Za 37:3na ili upate kumpenda Bwana Mungu wako, uisikilize sauti yake na kuambatana naye. Kwa kuwa Bwana ndiye uzima wako, na atakupa wingi wa siku ili upate kuishi katika nchi aliyoapa kuwapa baba zako Abrahamu, Isaki na Yakobo.

Read More of Kumbukumbu 30

Kumbukumbu 31:1-29

Yoshua Kutawala Baada Ya Mose

(Hesabu 27:12-23)

Kisha Mose akaenda akasema maneno haya kwa Waisraeli wote: 31:2 Kut 7:7; Hes 27:17; Kum 34:7; 1Fal 3:7; Kum 3:23-26“Sasa nina miaka mia moja na ishirini nami siwezi tena kuwaongoza. Bwana ameniambia, ‘Hutavuka Yordani.’ 31:3 Hes 27:18; Kum 9:3; 7:1; 3:28Bwana Mungu wenu, yeye mwenyewe atavuka mbele yenu. Ataangamiza mataifa haya mbele yenu, nanyi mtaimiliki nchi yao. Pia Yoshua atavuka mbele yenu, kama Bwana alivyosema. 31:4 Hes 21:33Naye Bwana atawafanyia watu hao kile alichowafanyia Sihoni na Ogu, wafalme wa Waamori, ambao aliwaangamiza pamoja na nchi yao. 31:5 Kum 2:33; 7:2Bwana atawakabidhi kwenu, nanyi lazima mwatendee yale yote niliyowaamuru. 31:6 Yos 1:6-9, 18; 10:23; 1Nya 22:13; 28:20; 2Nya 32:7; Yer 1:8, 17; Eze 2:6; Mwa 28:15; Kum 1:29; 20:4; Mt 28:20; Za 56:9; 118:6; Kum 4:31; 1Sam 12:22; 1Fal 6:13; Za 94:14; Isa 41:17; Ebr 13:5Kuweni imara na moyo wa ushujaa. Msiogope wala msifadhaike kwa sababu yao, kwa kuwa Bwana Mungu wenu anakwenda pamoja nanyi; kamwe hatawaacha wala hatawatupa ninyi.”

31:7 Hes 27:23; Yos 1:6; Kum 1:38; 3:28Kisha Mose akamwita Yoshua na akamwambia mbele ya Israeli wote, “Uwe imara na moyo wa ushujaa, kwa kuwa ni lazima uende na watu hawa katika nchi ile Bwana aliyowaapia baba zao kuwapa, nawe ni lazima uwagawie kama urithi wao. 31:8 Kut 13:21; Mwa 28:15; Kut 33:14; Kum 4:31Bwana mwenyewe atakutangulia naye atakuwa pamoja nawe; kamwe hatakuacha wala hatakutupa. Usiogope, wala usifadhaike.”

Kusoma Sheria

31:9 Kut 17:14; Hes 4:15; 1Nya 15:2Kwa hiyo Mose akaandika sheria hii na kuwapa makuhani, wana wa Lawi, waliochukua Sanduku la Agano la Bwana na wazee wote wa Israeli. 31:10 Kum 15:1; Kut 23:16; Kum 16:13; Law 23:34Kisha Mose akawaamuru, akasema: “Mwishoni mwa kila miaka saba, katika mwaka wa kufuta madeni, wakati wa Sikukuu ya Vibanda, 31:11 Kum 16:16; 12:5; Yos 8:34-35; 2Fal 23:2; Neh 8:2Waisraeli wote wanapokuja mbele za Bwana Mungu wenu mahali atakapopachagua, utasoma sheria hii mbele yao masikioni mwao. 31:12 Kum 4:10; Hag 1:12; Mal 1:6; 3:5, 16Kusanya watu wote, wanaume, wanawake, watoto na wageni wanaoishi katika miji yenu, ili waweze kusikia na kujifunza kumcha Bwana Mungu wenu na kufuata kwa bidii maneno yote ya sheria hii. 31:13 Kum 11:2; Za 78:6-7; Mit 22:6; Efe 6:4Watoto wao, ambao hawaijui sheria hii, lazima waisikie na kujifunza kumcha Bwana Mungu wenu kwa muda mtakaoishi katika nchi mnayovuka Yordani kuimiliki.”

Kuasi Kwa Waisraeli Kunatabiriwa

31:14 Mwa 25:8; Hes 27:13; 23; Kum 34:9; Yos 1:1-9; Hes 27:19; Kut 33:9-11Bwana akamwambia Mose, “Sasa siku ya kifo chako imekaribia. Mwite Yoshua, mkajihudhurishe katika Hema la Kukutania, mahali nitakapompa maagizo ya kazi.” Kwa hiyo Mose na Yoshua wakaja na kujihudhurisha kwenye Hema la Kukutania.

31:15 Kut 33:9; Za 99:7Kisha Bwana akatokea katika Hema katika nguzo ya wingu, nalo wingu likasimama juu ya ingilio la Hema. 31:16 Mwa 15:15; Kut 34:15; Kum 4:25-28; Amu 2:12; 10:6-13; 1Fal 9:9; 18:18; 19:10; Yer 2:13; 5:19; 19:4; 2Sam 7:12; 2Fal 22:16, 17; Isa 1:4Kisha Bwana akamwambia Mose: “Unakwenda kupumzika na baba zako, nao watu hawa hivi karibuni watazini na miungu migeni ya nchi wanayoingia. Wataniacha na kuvunja Agano nililofanya nao. 31:17 Kum 32:16; Amu 2:14; 20; 10:7; 2Fal 13:3; 22:13; Za 106:29, 40; Yer 7:18; 21:5; 36:17; Amu 6:13; 2Nya 15:2; 24:20; Ezr 8:22; Za 44:9; Isa 2:6; Kum 32:20; Isa 1:15; 45:15; 53:3; 54:8; Ay 13:24; Za 13:1; 27:9; 30:7; 104:29; Isa 50:6; Yer 33:5; Eze 39:29; Mik 3:4; Yer 4:20; Eze 7:26; Hes 14:42; Hos 9:12Siku hiyo nitawakasirikia na kuwaacha; nitawaficha uso wangu, nao wataangamizwa. Maafa mengi na shida nyingi zitakuja juu yao, nao siku hiyo watauliza, ‘Je, maafa haya hayakuja juu yetu kwa sababu Mungu wetu hayuko pamoja nasi?’ Nami hakika nitauficha uso wangu siku hiyo kwa sababu ya maovu yao yote kwa kugeukia miungu mingine.

31:19 Mwa 31:50“Sasa ujiandikie wimbo huu,31:19 Wimbo huu hapa ina maana wimbo wa Mose. uwafundishe Waisraeli na uwaamuru wauimbe, ili upate kuwa ushahidi wangu dhidi yao. 31:20 Kum 6:10-12; Za 4:2; 16:4; 40:4; Yer 13:25; Dan 3:28; Amo 2:4; Kum 8:19; 11:16-17Nitakapokwisha kuwaingiza katika nchi itiririkayo maziwa na asali, nchi niliyowaahidi baba zao kwa kiapo, nao watakapokula wakashiba na kufanikiwa, watageukia miungu mingine na kuiabudu, wakinikataa mimi na kuvunja Agano langu. 31:21 Kum 4:30; 1Nya 28:9; Hos 5:3; Yn 2:24-25Maafa na shida zitakapokuja juu yao, wimbo huu utashuhudia dhidi yao, kwa sababu hautasahauliwa na wazao wao. Ninajua lile wanaloandaa kufanya, hata kabla sijawaingiza katika nchi niliyowaahidi kwa kiapo.” Hivyo Mose akaandika wimbo huu siku ile na akawafundisha Waisraeli.

31:23 Yos 1:6Bwana akampa Yoshua mwana wa Nuni agizo hili: “Uwe hodari na shujaa, kwa kuwa utawaleta Waisraeli katika nchi niliyowaahidi kwa kiapo, nami mwenyewe nitakuwa pamoja nawe.”

31:24 Kum 17:18; 2Fal 22:8; Kum 28:58Baada ya Mose kumaliza kuandika kwenye kitabu maneno ya sheria hii kutoka mwanzo hadi mwisho, akawapa Walawi wale waliolibeba Sanduku la Agano la Bwana agizo hili, akawaambia: “Chukueni Kitabu hiki cha Sheria mkakiweke kando ya Sanduku la Agano la Bwana Mungu wenu. Hapo ndipo kitakapokaa kama shahidi dhidi yenu. 31:27 Kut 23:21; 32:9; Kum 9:27; 2Nya 30:8; Za 78:8; Isa 48:4; Za 32Kwa kuwa ninajua jinsi mlivyo waasi na mlivyo na shingo ngumu. Kama mmekuwa mkiasi dhidi ya Bwana nikiwa bado niko hai na nikiwa pamoja nanyi, mtaasi mara ngapi baada ya kufa kwangu! 31:28 Kum 4:26; 30:19; 32:1; Ay 20:27; Isa 26:21Kusanyeni mbele yangu wazee wote wa makabila yenu na maafisa wenu wote, ili nipate kusema maneno haya masikioni mwao na kuziita mbingu na nchi ili kushuhudia dhidi yao. 31:29 Kum 4:16; Ufu 9:20; 1Fal 9:9; 22:23; 2Fal 22:16Kwa kuwa ninajua baada ya kifo changu hakika mtakuwa waovu kabisa na kugeuka kutoka njia niliyowaamuru ninyi. Katika siku zijazo, maafa yatawapata kwa sababu mtafanya maovu mbele ya macho ya Bwana, na kuchochea hasira yake kwa yale mikono yenu itakayokuwa imefanya.”

Read More of Kumbukumbu 31