2 Nyakati 2:1-18, 2 Nyakati 3:1-17, 2 Nyakati 4:1-22, 2 Nyakati 5:1 NEN

2 Nyakati 2:1-18

Maandalizi Ya Kujenga Hekalu

(1 Wafalme 5:1-18)

2:1 Kum 12:5; 1Fal 5:5; Mhu 2:14Solomoni akatoa amri kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana na jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe. 2:2 2Nya 10:4; 1Fal 5:15Solomoni akaandika watu 70,000 kuwa wachukuzi wa mizigo, na watu 80,000 kuwa wachonga mawe vilimani, na watu 3,600 kuwa wasimamizi wao.

2:3 2Sam 5:11; 1Nya 14:1Solomoni akapeleka ujumbe huu kwa Mfalme Hiramu wa Tiro:

“Unitumie magogo ya mierezi kama ulivyomfanyia baba yangu Daudi wakati ulipompelekea mierezi ya kujenga jumba lake la kifalme la kuishi. 2:4 Kut 12:5; 25:30; Law 24:8; Kut 29:42; Hes 28:10; Kut 30:7; Mt 12:4Sasa ninakaribia kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana Mungu wangu na kuliweka wakfu kwake kwa ajili ya kufukizia uvumba wenye harufu nzuri mbele zake, mahali pa kuweka mikate ya Wonyesho kwa kufuata utaratibu na kwa ajili ya mahali pa kutolea sadaka za kuteketezwa kila siku asubuhi na jioni, siku za Sabato na Mwezi Mwandamo pia katika sikukuu zilizoamriwa za Bwana Mungu wetu. Hili ni agizo la kudumu kwa ajili ya Waisraeli.

2:5 1Nya 22:5; 16:25; Za 135:5; Kut 15:11; Za 86:8-9; Yer 10:6“Hekalu nitakalolijenga litakuwa kubwa, kwa sababu Mungu wetu ni mkuu kuliko miungu mingine yote. 2:6 1Fal 8:27; Yer 23:24; 2Nya 6:28; Kut 3:11; Isa 66:1Lakini ni nani awezaye kumjengea Hekalu, maadamu mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kumtosha? Mimi ni nani basi hata nimjengee Hekalu, isipokuwa liwe tu mahali pa kutolea dhabihu za kuteketezwa mbele zake?

2:7 Kut 35:31; 1Nya 22:16“Hivyo basi nitumie mtu mwenye ustadi wa kufanya kazi ya kutengeneza dhahabu na fedha, shaba na chuma, nyuzi za rangi ya zambarau, nyekundu na buluu, mwenye uzoefu wa kutia nakshi, ili afanye kazi Yuda na Yerusalemu pamoja na mafundi wangu wenye ustadi, ambao baba yangu Daudi aliwaweka.

2:8 1Fal 5:6; 19:11“Pia nitumie magogo ya mierezi, miberoshi na misandali kutoka Lebanoni kwa maana najua kwamba watu wako wanao ujuzi wa kupasua mbao huko. Watu wangu watafanya kazi pamoja na watu wako ili wanipatie mbao kwa wingi kwa sababu Hekalu nitakalojenga lazima liwe kubwa na zuri kabisa. 2:10 1Fal 5:11; Ezr 3:7Nitawapa watumishi wako, yaani, maseremala wakatao mbao, kori 20,0002:10 Kori 20,000 za ngano ni sawa na lita 4,400. za unga wa ngano, kori 20,000 za shayiri, bathi 20,0002:10 Bathi 20,000 za mvinyo au mafuta ni sawa na lita 440,000. za mvinyo, na bathi 20,000 za mafuta ya zeituni.”

2:11 1Fal 10:9; 2Nya 9:8; Kum 33:3Ndipo Hiramu mfalme wa Tiro akamjibu Solomoni kwa barua:

“Kwa sababu Bwana anawapenda watu wake, amekufanya wewe kuwa mfalme wao.”

2:12 Neh 9:6; Mdo 4:24; Za 146:6; 1Fal 5:7; Za 33:6; 102:25; Ufu 10:6Naye Hiramu akaongeza kusema:

“Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli aliyezifanya mbingu na nchi! Amempa Mfalme Daudi mwana mwenye hekima, aliyejaliwa maarifa na ufahamu, ambaye atajenga Hekalu kwa ajili ya Bwana, na jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe.

2:13 1Fal 7:13“Mimi nitamtuma kwako Huramu-Abi, mtu mwenye ustadi mwingi, 2:14 Kut 31:6; 35:31-35; 1Fal 7:13ambaye mama yake alitoka Dani na baba yake alitoka Tiro. Yeye ni stadi wa kutengeneza vitu, kufanya kazi zote za dhahabu, fedha, shaba, chuma, mawe na mbao pamoja na kufuma. Ni stadi katika kutia rangi ya zambarau, buluu, nyekundu na nguo za kitani safi. Yeye ana ujuzi katika aina zote za kutia nakshi na anaweza kufuatiliza mchoro wowote wa kazi anayopewa. Atafanya kazi na mafundi wako na wale wa bwana wangu, Daudi baba yako.

“Sasa basi bwana wangu na awapelekee watumishi wake ngano, shayiri, mafuta ya zeituni na mvinyo kama alivyoahidi, 2:16 Yos 19:46; Mdo 9:36; Yon 1:3; 1Fal 5:8nasi tutakata magogo yote yale unayohitaji kutoka Lebanoni nasi tutayafunga pamoja na kuyaweka yaelee baharini mpaka Yafa. Kisha utaweza kuyachukua mpaka Yerusalemu.”

2:17 1Nya 22:2; 2Sam 24:2; 2Nya 8:7-8; 1Fal 5:1Ndipo Solomoni akaamuru ifanyike hesabu ya wageni wote waliokuwa katika Israeli, baada ya ile hesabu iliyofanywa na Daudi; wakapatikana watu 153,600. Akawaweka watu 70,000 miongoni mwao kuwa wachukuzi wa mizigo, na 80,000 kuwa wachonga mawe vilimani, na 3,600 wakiwa wasimamizi juu yao ili wawahimize watu kufanya kazi.

Read More of 2 Nyakati 2

2 Nyakati 3:1-17

Solomoni Ajenga Hekalu

(1 Wafalme 6:1-38; 7:15-22)

3:1 Mdo 7:47; Mwa 28:17; 2Sam 24:18; Yn 2:19-21; 1Fal 6:1; 1Nya 29:19; 1Kor 6:19; Mwa 22:2Ndipo Solomoni akaanza kujenga Hekalu la Bwana katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, pale ambapo Bwana alikuwa amemtokea Daudi baba yake. Ilikuwa katika kiwanja cha kupuria cha Arauna,3:1 Pia anaitwa Ornani kwa Kiebrania. Myebusi, mahali palipotolewa na Daudi. 3:2 Ezr 5:11Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa utawala wake.

3:3 Eze 41:2; 1Fal 6:2-3Msingi aliouweka Solomoni kwa ajili ya kulijenga Hekalu la Mungu ulikuwa urefu wa dhiraa sitini3:3 Dhiraa 60 ni sawa na mita 27. na upana dhiraa ishirini.3:3 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9. 3:4 1Fal 6:3Ukumbi wa mbele wa Hekalu ulikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, yaani, kuanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa upana wa nyumba hiyo na kimo chake dhiraa thelathini.3:4 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5.

Akaufunika ndani kwa dhahabu safi. 3:5 Eze 40:16; 1Fal 6:17Akaufunika ukumbi mkuu kwa mbao za miberoshi na kufunikwa kwa dhahabu safi na kuupamba kwa miti ya mitende na kuifanyizia kwa minyororo. Alilipamba Hekalu kwa vito vya thamani. Hiyo dhahabu aliyotumia ilikuwa dhahabu ya Parvaimu. 3:7 1Fal 6:29-35; Eze 41:18Akazifunika boriti za dari, miimo na vizingiti vya milango, kuta na milango ya Hekalu kwa dhahabu, naye akatia nakshi ya makerubi kwenye kuta.

3:8 Kut 26:32-33Akajenga Patakatifu pa Patakatifu, urefu na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini, sawasawa na upana wa Hekalu. Alifunika ndani kwa talanta 1203:8 Talanta 120 za dhahabu ni sawa na tani 23. za dhahabu safi. Misumari ya dhahabu ilikuwa na uzito wa shekeli hamsini.3:9 Shekeli 50 za dhahabu ni sawa na gramu 600. Alivifunika pia vyumba vya juu kwa dhahabu.

3:10 Kut 25:18; 1Fal 6:23Katika sehemu ya Patakatifu pa Patakatifu akafanyiza jozi moja ya makerubi ya kuchongwa na kuyafunika kwa dhahabu. Urefu wa mabawa ya hao makerubi ulikuwa jumla ya dhiraa ishirini. Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano,3:11 Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25. nalo liligusa ukuta wa Hekalu, bawa lake lingine, lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano, ambalo liligusa bawa la kerubi lingine. Vivyo hivyo bawa moja la kerubi wa pili lilikuwa na urefu wa dhiraa tano na liligusa ukuta mwingine wa pili wa Hekalu na bawa lake lingine, lilikuwa pia na urefu wa dhiraa tano nalo liligusa bawa la kerubi wa kwanza. Mabawa ya makerubi hawa yalitanda dhiraa ishirini. Walisimama kwa miguu yao, nyuso zao zikielekea ukumbi mkubwa.

3:14 Kut 26:31-33; Ebr 9:3; Mwa 3:24; Mt 27:51Akatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na za kitani safi, na kutarizi makerubi juu yake.

3:15 1Fal 7:15; Ufu 3:12; Yer 52:21Mbele ya Hekalu Solomoni akatengeneza nguzo mbili, ambazo kwa pamoja zilikuwa na dhiraa thelathini na tano kwenda juu kwake, na urefu wa kila moja ilikuwa na taji juu yake yenye dhiraa tano. 3:16 1Fal 7:17-22Akatengeneza minyororo iliyosokotwa, na kuiweka juu ya zile nguzo. Pia akatengeneza makomamanga 100, na kuyashikamanisha kwenye minyororo. Akazisimamisha hizo nguzo mbele ya Hekalu, moja upande wa kusini na nyingine upande wa kaskazini. Ile moja ya upande wa kusini akaiita Yakini,3:17 Yakini maana yake Atathibitisha. na ya upande wa kaskazini akaiita Boazi.3:17 Boazi maana yake Imo nguvu.

Read More of 2 Nyakati 3

2 Nyakati 4:1-22

Vifaa Vya Hekalu

(1 Wafalme 7:23-51)

4:1 Eze 43:13; Kut 27:1-2; 2Fal 16:14; 1Fal 9:25Mfalme Solomoni akatengeneza madhabahu ya shaba yenye urefu wa dhiraa ishirini,4:1 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9. upana wa dhiraa ishirini na kimo chake dhiraa kumi.4:1 Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5. 4:2 Kut 30:18; Ufu 4:6; 15:2; 1Fal 7:23Akatengeneza Bahari ya kusubu, yenye umbo la mviringo, ya dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo na kimo cha dhiraa tano. Kamba ya urefu wa dhiraa thelathini4:2 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5. ingeweza kuizunguka. 4:3 1Fal 7:24Chini ya huo ukingo, kulikuwa na mafahali kuizunguka, yaani mafahali kumi katika kila dhiraa moja.4:3 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45. Hayo mafahali waliyasubu katika safu mbili yakiwa ya kitu kimoja na hiyo Bahari.

4:4 Eze 48:30-34; Ufu 21:13Bahari hiyo ilikaa juu ya mafahali kumi na wawili, mafahali watatu walielekeza nyuso zao kaskazini, watatu magharibi, watatu kusini na watatu mashariki. Bahari hiyo ilikaa juu ya hao mafahali, nazo sehemu zao za nyuma zilielekeana. 4:5 1Fal 7:26Unene wake ulikuwa nyanda nne,4:5 Nyanda nne ni sawa na sentimita 7.5. na ukingo wake ulifanana na ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi iliyochanua. Iliweza kuchukua bathi 3,000.4:5 Bathi 3,000 ni sawa na lita 60,000.

4:6 Kut 30:18; 1Fal 7:26; Ebr 9:9; 4:7Kisha akatengeneza masinia kumi kwa ajili ya kuoshea vifaa, naye akayaweka matano upande wa kusini na matano upande wa kaskazini. Ndani yake ndimo walioshea vifaa vya kutumika katika sadaka za kuteketezwa, lakini ile Bahari ilikuwa ni kwa ajili ya makuhani kunawia.

4:7 Kut 25:31, 40; 1Fal 7:49Akatengeneza vinara vya taa kumi vya dhahabu kama ilivyoainishwa kwao na kuviweka hekaluni, vinara vitano upande wa kusini na vitano upande wa kaskazini.

4:8 Kut 25:23; Hes 4:14; 1Fal 7:48-49Akatengeneza meza kumi na kuziweka hekaluni, tano upande wa kusini na tano upande wa kaskazini. Pia akatengeneza mabakuli 100 ya dhahabu ya kunyunyizia.

4:9 2Fal 21:5; 2Nya 33:5Akatengeneza ukumbi wa makuhani na ukumbi mwingine mkubwa na milango yake, naye akaifunika hiyo milango kwa shaba. Akaweka ile Bahari upande wa kusini, kwenye pembe ya kusini mashariki ya nyumba.

4:11 1Fal 7:14Pia akatengeneza masufuria, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia.

Kwa hiyo Huramu akakamilisha kazi katika Hekalu la Mungu kama vile Mfalme Solomoni alikuwa amemwagiza, yaani:

zile nguzo mbili;

yale mataji mawili yaliyokuwa juu ya hizo nguzo,

zile nyavu mbili za kupamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli yaliyowekwa juu ya zile nguzo;

4:13 Yer 52:23; Wim 4:13; Kut 28:33-34; 1Fal 7:20yale makomamanga 400 kwa ajili ya hizo nyavu mbili (safu mbili za makomamanga kwa kila wavu yakipamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo);

4:14 1Fal 7:27-30vishikio pamoja na masinia yake;

hiyo Bahari na hao mafahali kumi na wawili chini yake;

pia hayo masufuria, masepetu, uma za nyama na vyombo vingine vyote vilivyohusiana.

Vitu vyote ambavyo Huramu-Abi alimtengenezea Mfalme Solomoni kwa ajili ya Hekalu la Bwana vilikuwa vya shaba iliyosuguliwa. 4:17 Mwa 33:17; 1Fal 7:46Mfalme aliagiza wavisubu vitu hivi kwenye kalibu za udongo wa mfinyanzi katika uwanda wa Yordani kati ya Sukothi na Sereda.4:17 Au Sarethani. 4:18 1Fal 7:23, 47Vitu hivi vyote Mfalme Solomoni alivyotengeneza vilikuwa vingi sana hivi kwamba uzito wa shaba haungekadirika.

4:19 Kut 25:23, 30; 2Fal 24:13; Dan 5:2-3; Yer 28:3; 1Nya 28:6Solomoni pia akatengeneza samani zote zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mungu:

madhabahu ya dhahabu;

meza za kuweka mikate ya Wonyesho;

4:20 Kut 27:20-21vinara vya taa vya dhahabu safi pamoja na taa zake ili ziwake mbele ya sehemu takatifu ya ndani kama ilivyoelekezwa;

4:21 Kut 37:20; 1Fal 6:18-35; Kut 25:31maua ya dhahabu yaliyofanyizwa, taa na makoleo (vilikuwa vya dhahabu bora kabisa);

4:22 Hes 7:14; Law 10:1; 1Fal 6:21mikasi ya dhahabu safi, mabakuli ya kunyunyizia, masinia na vyetezo; milango ya dhahabu ya Hekalu: yaani milango ya ndani ya Patakatifu pa Patakatifu, na milango ya ukumbi mkuu.

Read More of 2 Nyakati 4

2 Nyakati 5:1

5:1 1Fal 6:14; 2Sam 8:11; 1Nya 26:26-28; 22:14Hivyo Solomoni alipomaliza kazi ya Hekalu la Bwana, akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu: yaani, fedha, dhahabu na samani; kisha akaviweka katika hazina za Hekalu la Mungu.

Read More of 2 Nyakati 5