1 Samweli 1:1-28, 1 Samweli 2:1-26 NEN

1 Samweli 1:1-28

Kuzaliwa Kwa Samweli

1:1 Mwa 18:25; 1Sam 9:5; Yos 17:17-18; 21:20-22; 1Nya 6:27-34; Rut 1:2Kulikuwepo na mtu mmoja kutoka Rama, Msufi kutoka nchi ya vilima vya Efraimu, ambaye jina lake aliitwa Elikana mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu. 1:2 Mwa 4:19; Kum 21:15-17Alikuwa na wake wawili, mmoja aliitwa Hana na mwingine Penina. Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na mtoto.

1:3 Kut 23:14; 1Sam 2:19; 20:6; Lk 2:41; Kum 12:5-7; 1Sam 2:31; 14:3; Yos 18:1; Amu 18:31; Za 78:60; Yer 7:12-14Kila mwaka mtu huyu alikwea kutoka mji wake ili kuabudu na kutoa dhabihu kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote huko Shilo, ambapo Hofni na Finehasi, wana wawili wa Eli, walikuwa makuhani wa Bwana. 1:4 Law 7:15-18; Kum 12:17-18; Mwa 29:34Kila mara ilipofika siku ya Elikana kutoa dhabihu, aliwapa mafungu Penina mkewe na wanawe wote pamoja na binti zake. 1:5 Mwa 37:3; 11:30; 29:31Lakini alimpa Hana fungu maradufu kwa sababu alimpenda, ingawa Bwana alikuwa amemfunga tumbo. 1:6 Mwa 16:4-5Kwa sababu Bwana alikuwa amemfunga tumbo, mke mwenzake alikuwa anamchokoza ili kumuudhi. 1:7 2Sam 12:17; Za 102:4; Kut 23:14; Kum 16:16; Kut 23:14Hili liliendelea mwaka baada ya mwaka. Kila mara Hana alipokwenda katika nyumba ya Bwana, mke mwenzake alikuwa akimkasirisha mpaka analia na kushindwa kula. 1:8 Rut 4:15Elikana mumewe akawa anamwambia, “Hana, kwa nini unalia? Kwa nini huli? Kwa nini kuvunjika moyo? Je, mimi si bora zaidi kwako kuliko watoto kumi?”

1:9 1Sam 3:3Siku moja walipokuwa wamemaliza kula na kunywa huko Shilo, Hana alisimama. Wakati huo kuhani Eli alikuwa ameketi kwenye kiti pembeni mwa mwimo wa mlango wa Hekalu la Bwana. 1:10 Ay 3:20; 7:11; 10:1; 21:25; 23:2; 27:2; Isa 38:15; Yer 20:18Kwa uchungu wa rohoni Hana alilia sana na akamwomba Bwana. 1:11 Amu 11:30; 13:7; 13:5; Lk 1:15; Mwa 17:1; 8:1; Za 24:10; 46:7; Isa 1:9; Hes 6:1-21; 21:2; 30:3-8; Mhu 5:4; Mwa 29:32; Kut 4:31Naye akaweka nadhiri, akisema, “Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, laiti ungeangalia huzuni kuu ya mtumishi wako na kunikumbuka mimi, wala usimsahau mtumishi wako nawe ukampa mwana, basi huyo mwana nitamtoa kwa Bwana kwa siku zote za maisha yake, wala wembe hautapita kichwani mwake.”

Alipokuwa anaendelea kumwomba Bwana, Eli alichunguza kinywa chake. Hana alikuwa akiomba moyoni mwake, midomo yake ikiwa inachezacheza lakini sauti haikusikika. Eli akafikiri alikuwa amelewa naye akamwambia, “Utaendelea kulewa mpaka lini? Achilia mbali mvinyo wako.”

1:15 2Fal 4:27; Za 42:4; 62:8; Mao 2:19Hana akajibu, “Si hivyo bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye huzuni kubwa. Mimi sijanywa mvinyo wala kileo, nilikuwa ninaumimina moyo wangu kwa Bwana. 1:16 Za 55:2; 2Kor 6:15Usimdhanie mtumishi wako kuwa mwanamke mwovu; nimekuwa nikiomba hapa katika wingi wa uchungu mkuu na huzuni.”

1:17 Hes 6:26; 1Sam 20:42; 2Fal 5:19; Mdo 15:33; Mwa 25:21; Za 20:3-5; Mwa 33:15; Yn 16:24Eli akamjibu, “Nenda kwa amani, naye Mungu wa Israeli na akujalie kile ulichomwomba.”

1:18 Mwa 18:3; Rut 2:13; Rum 15:13; Ufu 2:13; Mhu 9:7Hana akasema, “Mtumishi wako na apate kibali machoni pako.” Kisha akaondoka zake na kula chakula, wala uso wake haukuwa na huzuni tena.

1:19 Yos 18:25; Mwa 8; 1; 29:31Kesho yake asubuhi na mapema waliamka wakaabudu mbele za Bwana na kisha wakarudi nyumbani kwao huko Rama. Elikana akakutana kimwili na mkewe Hana, naye Bwana akamkumbuka. 1:20 Mwa 17:19; 29:32; 30:6; Kut 2:10; Mt 1:21; 1Sam 7:5; 12:23; 1Nya 6:27; Yer 15:1; Ebr 11:32Hivyo wakati ulipotimia, Hana akapata mimba na akamzaa mwana. Hana akamwita jina lake Samweli, akasema, “Kwa kuwa nilimwomba kwa Bwana.”

Hana Anamweka Samweli Wakfu

1:21 Mwa 28:20; Hes 30:2; Kum 12:11Wakati huyo mtu Elikana alipanda pamoja na jamaa yake yote kutoa dhabihu ya mwaka kwa Bwana na kutimiza nadhiri yake, 1:22 Lk 2:22; Kut 13:2; 1Sam 2:11; 3:1Hana hakwenda. Alimwambia mume wake, “Baada ya mtoto kuachishwa kunyonya, nitamchukua na kumpeleka mbele za Bwana, naye ataishi huko wakati wote.”

1:23 Mwa 25:21; 21:8; Hes 30:7; 2Sam 7:25Elikana mumewe akamwambia, “Fanya lile unaloona ni bora zaidi kwako. Ukae hapa mpaka utakapomwachisha kunyonya, Bwana na akujalie kutimiza nadhiri yako.” Hivyo huyo mwanamke akakaa nyumbani na kumnyonyesha mwanawe mpaka alipomwachisha kunyonya.

1:24 Hes 15:8-10Baada ya mtoto kuachishwa kunyonya, Hana akamchukua huyo mtoto, akiwa mdogo hivyo hivyo, pamoja na fahali wa miaka mitatu, efa ya unga1:24 Efa moja ya unga ni sawa na kilo 22. na kiriba cha divai, naye akamleta mtoto kwenye nyumba ya Bwana huko Shilo. Walipokwisha kumchinja yule fahali, wakamleta mtoto kwa Eli, naye Hana akamwambia Eli, “Hakika kama uishivyo, bwana wangu, mimi ndiye yule mama ambaye alisimama hapa karibu nawe akiomba kwa Bwana. 1:27 1Sam 2:20; Za 66:19-20; Mit 7:7Niliomba mtoto huyu, naye Bwana amenijalia kile nilichomwomba. 1:28 Amu 13:7; Mwa 24:26, 52Hivyo sasa ninamtoa kwa Bwana. Kwa maana maisha yake yote atakuwa ametolewa kwa Bwana.” Naye akamwabudu Bwana huko.

Read More of 1 Samweli 1

1 Samweli 2:1-26

Maombi Ya Hana

2:1 Lk 1:46-55; Za 13:5; 33:21; 18:2; 89:17; 148:4; 6:8; Hes 10:35; Zek 10:7; Flp 4:6Kisha Hana akaomba na kusema:

“Moyo wangu wamshangilia Bwana,

katika Bwana pembe yangu imeinuliwa juu.

Kinywa changu chajisifu juu ya adui zangu,

kwa kuwa naufurahia wokovu wako.

2:2 Kut 15:11; 8:10; 33:22; Law 11:44; Isa 40:25; 46:5; Mwa 49:25; Kum 32:37; 2Sam 22:2-32; 23:2-3; Za 31:3; 71:3“Hakuna yeyote aliye mtakatifu kama Bwana,

hakuna mwingine zaidi yako;

hakuna Mwamba kama Mungu wetu.

2:3 Za 17:10; 31:18; 73:8; 75:4; 94:4; Yos 22:22; 1Sam 16:7; 1Fal 8:39; 1Nya 28:9; 2Nya 6:30; Mit 15:11; 24:11-12; Yer 11:20; 17:16“Msiendelee kusema kwa kiburi hivyo

wala msiache vinywa vyenu kunena kwa kiburi,

kwa kuwa Bwana ndiye Mungu ajuaye,

na kwa yeye matendo hupimwa.

2:4 2Sam 1:27; Za 37:15; 46:9; 76:3; Ay 17:9; Isa 40:31; 41:1; 52:1; 57:10“Pinde za mashujaa zimevunjika,

lakini wale wanaojikwaa wamevikwa nguvu.

2:5 Lk 1:53; Za 113:9; Isa 54:1; Yer 15:9; Gal 4:27Wale waliokuwa na chakula tele wamejikodisha wenyewe

ili kupata chakula,

lakini wale waliokuwa na njaa

hawana njaa tena.

Mwanamke yule aliyekuwa tasa

amezaa watoto saba,

lakini yule ambaye alikuwa na wana wengi

amedhoofika.

2:6 Kum 32:39; Ay 5:18; Hos 6:1; Yn 5:25-29; 11:25, 26; Ufu 1:18Bwana huua na huleta uhai,

hushusha chini mpaka kaburini2:6 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. na hufufua.

2:7 Kum 8:18; Ay 5:11; 40:12; Za 75:7; Isa 2:12; 13:11; 22:19; Dan 4:37; Za 75:8Bwana humfanya mtu maskini naye hutajirisha,

hushusha na hukweza.

2:8 Za 113:7-8; 72:12; 107:41; 145:14; 146:8; 104:5; Mit 8:29; Mt 23:12; 2Sam 7:8; Ay 36:7; 15:7; 38:4; Isa 22:23; 40:12; Yer 10:12; Eze 21:26; Yak 2:5; 1Fal 16:2Humwinua maskini kutoka mavumbini

na humwinua mhitaji kutoka lundo la majivu;

huwaketisha pamoja na wakuu

na kuwafanya warithi kiti cha enzi cha heshima.

“Kwa kuwa misingi ya dunia ni ya Bwana;

juu yake ameuweka ulimwengu.

2:9 Za 91:12; 121:3; Mit 3:26; 2:8; Ay 10:22; 37:4-5; 38:1; Za 18:13; 29:3; 96:13; 98:9; 18:1; 21:1; 59:16; 89:24; Kum 33:17; Lk 1:69; Isa 66:6; 5:30; 8:22; 59:9; 60:2; Yer 13:16; Amo 5:18-20; Sef 1:14-15; Mt 8:12; 25:31-32; 1Sam 17:47; 2Sam 22:14Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake,

lakini waovu watanyamazishwa kwenye giza.

“Si kwa nguvu mtu hushinda;

2:10 Za 96:13wale wampingao Bwana

wataharibiwa kabisa.

Atapiga radi dhidi yao kutoka mbinguni;

Bwana ataihukumu miisho ya dunia.

“Atampa nguvu mfalme wake,

na kuitukuza pembe

ya mpakwa mafuta wake.”

2:11 Yos 18:25; Hes 16:9; 1Sam 3:1; 2:18Kisha Elikana akaenda nyumbani Rama, lakini mtoto akahudumu mbele za Bwana chini ya kuhani Eli.

Wana Waovu Wa Eli

2:12 Yer 2:8; 9:6; Kum 13:13; Rum 1:28Wana wa Eli walikuwa watu wabaya kabisa, hawakumheshimu Bwana. 2:13 Kum 18:3; Law 7:29-36; 1Sam 2:12Basi ilikuwa desturi ya makuhani pamoja na watu kwamba kila mara yeyote anapotoa dhabihu na huku nyama ikiwa inachemshwa, mtumishi wa kuhani angalikuja na uma wenye meno matatu mkononi mwake. 2:14 Hes 15:30; Isa 22:14; Yer 7:16; Ebr 10:26-31Angeutumbukiza huo uma kwenye sufuria au birika au sufuria kubwa au chungu, naye kuhani angalijichukulia mwenyewe chochote ambacho uma ungekileta. Hivi ndivyo walivyowatendea Waisraeli wote waliokuja Shilo. Lakini hata kabla mafuta ya mnyama hayajachomwa, mtumishi wa kuhani angalikuja na kusema kwa mtu ambaye alikuwa akitoa dhabihu, “Mpe kuhani nyama akaoke, kwani hatapokea nyama iliyochemshwa kutoka kwako, ila iliyo mbichi tu.”

2:16 Law 3:3, 14-16; 7:29-34Kama mtu akimwambia, “Mafuta ya mnyama na yachomwe kwanza, ndipo uchukue chochote unachotaka,” mtumishi angalijibu, “Hapana, nipe sasa, kama huwezi nitaichukua kwa nguvu.”

2:17 Hes 14:11; Yer 7:21; Eze 22:26; Mal 2:7-9; 1Sam 2:22; Rut 1:17; Mt 26:63Hii Dhambi ya hawa vijana ilikuwa kubwa sana machoni pa Bwana, kwa kuwa waliitendea dhabihu ya Bwana kwa dharau.

2:18 1Sam 22:18; 23:9; 2Sam 6:14; 1Nya 15:27; Mwa 18:25; 1Sam 16:10-12; Ay 1:21; 2:10; Za 39:9Lakini Samweli alikuwa akihudumu mbele za Bwana, kijana akivaa kisibau cha kitani. 2:19 1Sam 1:3; Mwa 18:25; 1Sam 18:14; 2Tim 4:22; 1Sam 9:6Kila mwaka mama yake alimshonea joho dogo na kumchukulia wakati alipokwea pamoja na mumewe kutoa dhabihu ya mwaka. 2:20 1Sam 1:27; Lk 2:34; Amu 20:1Eli alikuwa akiwabariki Elikana na mkewe, akisema, “Bwana na akupe watoto kwa mwanamke huyu ili kuchukua nafasi ya yule aliyekuwa amemwomba na akamtoa kwa Bwana.” Kisha wakawa wanakwenda nyumbani. 2:21 Mwa 21:1; Amu 13:24; Lk 1:80; 2:40Bwana akawa mwenye neema kwa Hana, naye akapata mimba akazaa wana watatu na binti wawili. Wakati huo, kijana Samweli akaendelea kukua mbele za Bwana.

2:22 Kut 38:8Basi Eli, ambaye alikuwa mzee sana, alisikia kuhusu kila kitu ambacho wanawe walikuwa wakiwafanyia Israeli wote na jinsi walivyokutana kimwili na wanawake waliohudumu kwenye ingilio la Hema la Kukutania. Hivyo akawaambia, “Kwa nini mmefanya mambo kama haya? Nimesikia kutoka kwa watu wote juu ya haya matendo yenu maovu. Sivyo, wanangu, hii si habari nzuri ambayo ninasikia ikienea miongoni mwa watu wa Bwana. 2:25 Kut 4:21; 32:10; Yos 11:20; Hes 11:2; 1Sam 3:14; 1Fal 13:6; Ay 9:33; Za 106:30; Isa 1:18; 22:14; Yer 15:1; Ebr 10:26Kama mtu akifanya dhambi dhidi ya mtu mwenzake, mtu mwingine aweza kumwombea kwa Mungu, lakini kama mtu akimfanyia Mungu dhambi, ni nani atakayemwombea?” Hata hivyo wanawe hawakusikia maonyo ya baba yao, kwa sababu Bwana alitaka kuwaua.

2:26 Amu 13:24; Lk 2:52; Mit 3:4; Mdo 2:47; Rum 14:18Naye kijana Samweli akaendelea kukua katika kimo, akimpendeza Bwana na wanadamu.

Read More of 1 Samweli 2