1 Nyakati 15:1-29, 1 Nyakati 16:1-36 NEN

1 Nyakati 15:1-29

Sanduku La Agano Laletwa Yerusalemu

(2 Samweli 6:12-22)

15:1 Za 132:1-5; 2Sam 6:17; 1Nya 17:1-5; Mdo 7:46Baada ya Daudi kujijengea nyumba zake katika Mji wa Daudi, akatengeneza sehemu kwa ajili ya Sanduku la Mungu, kisha akasimamisha hema kwa ajili yake. 15:2 Hes 3:6; Kum 31:9, 25; 2Nya 29:11; Hes 4:2, 15; Kum 10:5; Yos 3:3Kisha Daudi akasema, “Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kulibeba Sanduku la Mungu isipokuwa Walawi peke yao, kwa sababu Bwana aliwachagua kulibeba Sanduku la Bwana na kuhudumu mbele zake milele.”

15:3 1Nya 13:5; 1Fal 8:1Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu ili kulipandisha Sanduku la Bwana na kulileta hadi kwenye sehemu aliyokuwa ametengeneza kwa ajili yake. Kisha Daudi akawakusanya pamoja wazao wa Aroni na Walawi:

15:5 Kut 6:16-18Kutoka wazao wa Kohathi,

Urieli kiongozi na ndugu zake 120,

Kutoka wazao wa Merari,

Asaya kiongozi na ndugu zake 220.

Kutoka wazao wa Gershoni,15:7 Namna nyingine ya kutaja Gershomu.

Yoeli kiongozi na ndugu zake 130.

15:8 Kut 6:22Kutoka wazao wa Elisafani,

Shemaya kiongozi na ndugu zake 200.

15:9 Hes 26:58; Kut 6:18Kutoka wazao wa Hebroni,

Elieli kiongozi na ndugu zake 80.

Kutoka wazao wa Uzieli,

Aminadabu kiongozi na ndugu zake 112.

15:11 1Nya 12:28; 1Sam 22:20Kisha Daudi akawaita makuhani Sadoki na Abiathari, pamoja na Walawi Urieli, Asaya, Yoeli, Shemaya, Elieli na Aminadabu. 15:12 Kut 29:10; Law 11:44; Eze 48:11; Yn 17:17; Law 10:3; 2Nya 5:11; 29:5, 15; Rum 12:1-2Akawaambia, “Ninyi ndio viongozi wa jamaa za Walawi. Ninyi pamoja na Walawi wenzenu inawapasa mjitakase na kulipandisha Sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli hadi mahali ambapo nimetengeneza kwa ajili yake. 15:13 1Fal 8:4; 2Sam 6:3; 1Nya 13:11Ilikuwa ni kwa sababu hii, ninyi Walawi, hamkulipandisha Sanduku la Bwana mara ya kwanza, hata ikasababisha Bwana Mungu wetu kuwaka hasira dhidi yetu. Hatukumuuliza jinsi ya kufanya ili tupate kulileta jinsi alivyoagiza.” Kwa hiyo makuhani pamoja na Walawi wakajitakasa ili kulipandisha Sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli. 15:15 Kut 25:14; Hes 4:5-15Nao Walawi wakalichukua Sanduku la Mungu mabegani mwao wakitumia mipiko, kama vile Mose alivyoamuru sawasawa na neno la Bwana.

15:16 Ezr 2:41; Neh 11:23; Amo 6:5; Ay 21:12; Za 68:25; 1Nya 6:31; 13:8; Za 33:2Daudi akawaambia viongozi wa Walawi kuwaweka ndugu zao waimbaji ili waimbe nyimbo za shangwe, wakiwa na vyombo vya uimbaji: zeze, vinubi na matoazi.

15:17 1Nya 6:33-44Basi Walawi wakawaweka Hemani mwana wa Yoeli; kutoka miongoni mwa ndugu zake, Asafu mwana wa Berekia; kutoka miongoni mwa ndugu zao Wamerari, Ethani mwana wa Kushaiya; 15:18 2Sam 6:10; 1Nya 26:4-5hawa ndio waliochaguliwa kuwa wasaidizi wao: Zekaria, Yaazieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Benaya, Maaseya, Matithia, Elifelehu, Mikneya, pamoja na mabawabu Obed-Edomu na Yehieli.

15:19 1Nya 16:12-13; 29:26Waimbaji Hemani, Asafu na Ethani walichaguliwa kupiga matoazi ya shaba; Zekaria, Azieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Maaseya na Benaya walikuwa wapiga zeze kufuatana na sauti ya alamothi,15:20 Huenda ni aina ya uimbaji. na Matithia, Elifelehu, Mikneya, Obed-Edomu, Yehieli na Azazia walikuwa wapiga vinubi, wakiongozwa kwa kufuata sauti ya sheminithi.15:21 Huenda ni aina ya uimbaji. Kenania kiongozi wa Walawi alikuwa msimamizi wa uimbaji; huu ndio uliokuwa wajibu wake kwa sababu alikuwa stadi katika hilo.

Berekia na Elikana walikuwa mabawabu kwa ajili ya Sanduku. 15:24 2Nya 5:12; Hes 10:8; 2Nya 29:26; Za 81:3Shebania, Yoshafati, Nethaneli, Amasai, Zekaria, Benaya na Eliezeri, makuhani, walikuwa wapiga tarumbeta mbele ya Sanduku la Mungu. Obed-Edomu na Yehiya waliwekwa pia kuwa mabawabu wa Sanduku.

15:25 2Sam 16:12-13; 2Nya 5:2; Yer 3:16; Kum 12:7, 18; Ezr 6:16Basi Daudi pamoja na wazee wa Israeli na majemadari wa vikosi vya elfu wakaenda ili kulipandisha Sanduku la Agano la Bwana kutoka nyumba ya Obed-Edomu kwa shangwe. 15:26 Ay 42:8; Hes 23:1-4, 29Kwa sababu Mungu alikuwa amewasaidia Walawi waliokuwa wanalichukua Sanduku la Agano la Bwana, mafahali saba na kondoo dume saba walitolewa dhabihu. Basi Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, kama walivyokuwa wamevaa Walawi wote waliokuwa wanalichukua lile Sanduku, waimbaji nao walivaa vivyo hivyo, pamoja na Kenania aliyekuwa anaongoza nyimbo za waimbaji. Daudi alivaa pia kisibau cha kitani safi. 15:28 Kut 19:13; 1Nya 13:8Hivyo Israeli wote wakalipandisha Sanduku la Agano la Bwana kwa shangwe, wakipiga pembe za kondoo dume, tarumbeta, matoazi, wakipiga zeze na vinubi.

15:29 2Sam 6:16; Mdo 2:13Sanduku la Agano la Bwana lilipokuwa linaingia katika Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani. Naye alipomwona Mfalme Daudi akicheza na kusherehekea, akamdharau moyoni mwake.

Read More of 1 Nyakati 15

1 Nyakati 16:1-36

Sanduku Lawekwa Ndani Ya Hema

16:1 2Sam 6:17-19Wakaleta Sanduku la Mungu na kuliweka ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, na wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu. 16:2 Kut 39:43; Hes 6:23-27Baada ya Daudi kumaliza kutoa hizo sadaka za kuteketezwa na hizo sadaka za amani, akawabariki watu katika jina la Bwana. Kisha akamgawia kila Mwisraeli mwanaume na mwanamke mkate, andazi la tende na andazi la zabibu kavu.

16:4 1Nya 15:1-2Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku la Bwana kufanya maombi, kumshukuru na kumsifu Bwana, Mungu wa Israeli: Asafu ndiye alikuwa mkuu wao, akisaidiwa na Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaya, Obed-Edomu na Yeieli. Hawa ndio wangepiga zeze na vinubi, Asafu angepiga matoazi, nao Benaya na Yahazieli makuhani, ndio wangepiga tarumbeta mara kwa mara mbele ya Sanduku la Agano la Mungu.

Zaburi Ya Daudi Ya Shukrani

(Zaburi 105:1-15; 96:1-13; 106:1, 47-48)

16:7 2Sam 23:1; Za 47:7Siku ile, kitu cha kwanza Daudi alichofanya ni kumkabidhi Asafu na wenzake zaburi hii ya shukrani kwa Bwana:

16:8 Za 107:1; 118:1; 2Fal 19:19Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake;

wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.

16:9 Za 100:1; Kut 15:1; Za 7:17; 95:1-2Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa;

waambieni matendo yake yote ya ajabu.

16:10 Za 34:3; Isa 45:25Lishangilieni jina lake takatifu;

mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.

16:11 Za 27:8; Mit 8:17; Amo 5:6-14Mtafuteni Bwana na nguvu zake;

utafuteni uso wake siku zote.

16:12 Za 78:43; 103:2Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya,

miujiza yake na hukumu alizozitamka,

enyi wazao wa Israeli mtumishi wake,

enyi wana wa Yakobo, wateule wake.

16:14 Isa 29:9; 4:4Yeye ndiye Bwana Mungu wetu;

hukumu zake zimo duniani pote.

Hulikumbuka agano lake milele,

neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,

16:16 Mwa 17:2; Neh 9:8; Ebr 6:13-18; Za 105:8-10; Mwa 15:18; 26:3agano alilolifanya na Abrahamu,

kiapo alichomwapia Isaki.

16:17 Mwa 35:9-12Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri,

kwa Israeli liwe agano la milele:

16:18 Mwa 13:14-17“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani

kuwa sehemu utakayoirithi.”

16:19 Mwa 34:30; Ebr 11:13; Kum 7:7Walipokuwa wachache kwa idadi,

wachache sana na wageni ndani yake,

walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine,

kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.

16:21 Mwa 20:3; Kut 7:15-18; Za 9:5; Mwa 12:17Hakuruhusu mtu yeyote awaonee;

kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:

16:22 Mwa 20:7; Za 105; 15; 1Yn 2:27“Msiwaguse niliowatia mafuta;

msiwadhuru manabii wangu.”

16:23 Za 47:1; 96:1Mwimbieni Bwana dunia yote;

tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.

16:24 Isa 12:4Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa,

matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.

16:25 Za 18:3; 76:7; 89:7; Kut 18:11; Isa 40:25-26; Za 24:8Kwa kuwa Bwana ni mkuu,

mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote;

yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.

16:26 Law 19:4; Isa 45:20; 1Kor 8:4; Za 115:4-8; Yer 10:3Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu,

lakini Bwana aliziumba mbingu.

Fahari na enzi viko mbele yake;

nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.

16:28 Za 29:1-2; 8:1Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa,

mpeni Bwana utukufu na nguvu,

mpeni Bwana utukufu

unaostahili jina lake.

Leteni sadaka na mje katika nyua zake;

mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake.

16:30 Za 2:11; 33:8Dunia yote na itetemeke mbele zake!

Ulimwengu ameuweka imara; hauwezi kusogezwa.

16:31 Isa 44:23; 35:10; 49:13; Mao 5:19; Isa 52:7; Lk 2:13; Ufu 14:2Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi;

semeni katikati ya mataifa, “Bwana anatawala!”

16:32 Kut 20:11; Za 98:7; 96:10Bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;

mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo ndani yake.

16:33 Isa 14:8; 55:12; Za 110:6Kisha miti ya msituni itaimba,

itaimba kwa furaha mbele za Bwana,

kwa maana anakuja kuihukumu dunia.

16:34 Isa 12:4; Za 25:7; Ezr 3:11; Yer 33:1Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema;

upendo wake wadumu milele.

16:35 Kum 32:15; Mik 7:7; Ezr 3:11; Yer 33:11; Za 106:47Mlilieni, “Ee Mungu Mwokozi wetu, tuokoe.

Tukusanye tena na utukomboe kutoka kwa mataifa,

ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu,

na kushangilia katika sifa zako.”

16:36 Kum 27:15; 1Fal 8:15; Neh 8:6; 10:27; 2Nya 8:14; Za 72:18-19Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli,

tangu milele na hata milele.

Nao watu wote wakasema, “Amen,” na “Msifuni Bwana.”

Read More of 1 Nyakati 16