Zekaria 9:1-17, Zekaria 10:1-12, Zekaria 11:1-17 NEN

Zekaria 9:1-17

Hukumu Juu Ya Adui Za Israeli

Neno:

9:1 Isa 17:1; Amo 1:5; Za 145:15Neno la Bwana liko kinyume na nchi ya Hadraki

na Dameski itakuwa mahali pa kupumzika,

kwa kuwa macho ya watu na ya kabila zote

za Israeli yako kwa Bwana,

9:2 Yer 49:23; Eze 28:1-19; Mwa 10:15; Amo 1:9; Oba 1:20pia juu ya Hamathi inayopakana nayo,

juu ya Tiro na Sidoni,

ingawa wana ujuzi mwingi sana.

9:3 Ay 27:16; Eze 28:4Tiro amejijengea ngome imara,

amelundika fedha kama mavumbi

na dhahabu kama taka za mitaani.

9:4 Isa 23:1, 11; Yer 25:22; Eze 26:3-5; 27:32-36; 28:18Lakini Bwana atamwondolea mali zake

na kuuangamiza uwezo wake wa baharini,

naye atateketezwa kwa moto.

9:5 Yer 47:5; Sef 2:5; Mdo 8:26Ashkeloni ataona hili na kuogopa;

Gaza atagaagaa kwa maumivu makali,

pia Ekroni, kwa sababu

matumaini yake yatanyauka.

Gaza atampoteza mfalme wake

na Ashkeloni ataachwa pweke.

9:6 Isa 14:30Wageni watakalia mji wa Ashdodi,

nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti.

9:7 Ay 25:2; Yoe 3:4; Sef 2:4; Yer 47:1Nitaondoa damu vinywani mwao,

chakula kile walichokatazwa kati ya meno yao.

Mabaki yao yatakuwa mali ya Mungu wetu,

nao watakuwa viongozi katika Yuda,

naye Ekroni atakuwa kama Wayebusi.

9:8 Isa 26:1; 52:1; 54:14; Zek 14:21; Yoe 3:17; Kum 33:27; Za 34:7; Kut 3:7Lakini nitailinda nyumba yangu

dhidi ya majeshi ya wanyangʼanyi.

Kamwe mdhalimu hatashambulia watu wangu tena,

kwa maana sasa ninawachunga.

Kuja Kwa Mfalme Wa Sayuni

9:9 Isa 62:11; 9:6-7; 43:3-11; 1Fal 1:39; Za 24:7; 149:2; Mik 4:8; Yer 23:5-6; Sef 3:14-15; Zek 2:10; Mwa 49:11; Mt 21:5; 1Fal 1:33; Yn 12:15; 1:49; Lk 19:38; Mdo 22:14; 1Pet 3:18Shangilia sana, ee Binti Sayuni!

Piga kelele, Binti Yerusalemu!

Tazama, Mfalme wako anakuja kwako,

ni mwenye haki, naye ana wokovu,

ni mpole, naye amepanda punda,

mwana-punda, mtoto wa punda.

9:10 Mik 4:3; 5:10; Hos 1:7; 2:18; Zek 10:4; Isa 2:4; Za 72:8; Isa 11:10; Efe 2:14; Kol 1:20-21; Za 2:8; Isa 9:6-7; Mik 5:4; Ufu 11:15Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu

na farasi wa vita kutoka Yerusalemu,

nao upinde wa vita utavunjwa.

Atatangaza amani kwa mataifa.

Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari,

na kutoka Mto Frati hadi mwisho wa dunia.

9:11 Kut 24:8; Mt 26:28; Lk 22:20; Isa 10:4; 42:7; Yer 38:6; Isa 61:1Kwako wewe, kwa sababu ya damu ya Agano langu nawe,

nitawaacha huru wafungwa wako

watoke kwenye shimo lisilo na maji.

9:12 Yoe 3:16; Isa 40:2; Kum 21:17Rudieni ngome yenu, enyi wafungwa wa tumaini;

hata sasa ninatangaza kwamba

nitawarejesheeni maradufu.

9:13 2Sam 22:25; Isa 49:2; Yoe 3:6; Yer 51:20Nitampinda Yuda kama nipindavyo upinde wangu,

nitamfanya Efraimu mshale wangu.

Nitawainua wana wako, ee Sayuni,

dhidi ya wana wako, ee Uyunani,

na kukufanya kama upanga wa shujaa wa vita.

Bwana Atatokea

Kisha Bwana atawatokea;

mshale wake utamulika

kama umeme wa radi.

Bwana Mwenyezi atapiga tarumbeta,

naye atatembea katika tufani za kusini,

9:15 Isa 31:5; 37:35; Zek 12:8; 10:7; 14:3, 20; Kut 27:2; Law 4:25na Bwana Mwenye Nguvu Zote atawalinda.

Wataangamiza na kushinda

kwa mawe ya kutupa kwa kombeo.

Watakunywa na kunguruma kama waliolewa mvinyo;

watajaa kama bakuli linalotumika kunyunyizia

kwenye pembe za madhabahu.

9:16 Isa 10:20; Yer 31:11; Eze 37:23; Mal 3:17; Isa 11:12Bwana Mungu wao atawaokoa siku hiyo

kama kundi la watu wake.

Watangʼara katika nchi yake

kama vito vya thamani kwenye taji.

Jinsi gani watavutia na kuwa wazuri!

Nafaka itawastawisha vijana wanaume,

nayo divai mpya vijana wanawake.

Read More of Zekaria 9

Zekaria 10:1-12

Bwana Ataitunza Yuda

10:1 Law 26:4; 1Fal 8:36; Za 104:13; 135:7; Ay 14:9; Yer 14:22; Yoe 2:32Mwombeni Bwana mvua wakati wa vuli;

ndiye Bwana atengenezaye mawingu ya tufani.

Huwapa watu manyunyu ya mvua,

pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu.

10:2 Eze 21:21; Isa 44:25; 40:19; Yer 23:16; Hes 27:17; Hos 3:4; Mt 9:36Sanamu huzungumza udanganyifu,

waaguzi huona maono ya uongo;

husimulia ndoto ambazo si za kweli,

wanatoa faraja batili.

Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo

walioonewa kwa kukosa mchungaji.

10:3 Isa 14:9; Yer 25:34; Eze 34:8-10; Kut 4:31; Rut 1:6; Sef 2:7; Lk 1:68; 1Pet 2:12“Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji,

nami nitawaadhibu viongozi;

kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote

atalichunga kundi lake,

nyumba ya Yuda,

naye atawafanya kuwa kama farasi

mwenye kiburi akiwa vitani.

10:4 Za 118:22; Mdo 4:11; Isa 22:23; Zek 9:10Kutoka Yuda litatokea Jiwe la pembeni,

kutoka kwake vitatoka vigingi vya hema,

kutoka kwake utatoka upinde wa vita,

kutoka kwake atatoka kila mtawala.

10:5 2Sam 22:43; Mik 7:10; 5:8; Amo 2:15; Hag 2:22; Zek 12:4Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa

wanaokanyaga barabara za matope

wakati wa vita.

Kwa sababu Bwana yu pamoja nao,

watapigana na kuwashinda wapanda farasi.

10:6 Eze 30:24; 36:37; Za 102:13; 34:17; Isa 37:19; 14:1; 58:9; 65:24; Zek 8:7-8; 13:9“Nitaiimarisha nyumba ya Yuda

na kuiokoa nyumba ya Yosefu.

Nitawarejesha kwa sababu

nina huruma juu yao.

Watakuwa kama watu ambao

sijawahi kuwakataa

kwa sababu mimi ndimi Bwana Mungu wao,

nami nitawajibu.

10:7 Zek 9:15; 1Sam 2:1; Isa 60:5; Yoe 2:23Waefraimu watakuwa kama mashujaa,

mioyo yao itafurahi kana kwamba ni kwa divai.

Watoto wao wataona na kufurahi,

mioyo yao itashangilia katika Bwana.

10:8 Isa 5:26; Yer 33:22; Eze 36:11Nitawaashiria na kuwakusanya ndani.

Hakika nitawakomboa,

nao watakuwa wengi

kama walivyokuwa mwanzoni.

10:9 Isa 44:21; Eze 6:9Ijapokuwa niliwatawanya miongoni mwa mataifa,

hata hivyo wakiwa katika nchi za mbali

watanikumbuka mimi.

Wao na watoto wao watanusurika katika hatari

nao watarudi.

10:10 Isa 11:11; 49:19; Zek 8:8; Yer 50:19; Rum 11:25; Kut 14:26-27Nitawarudisha kutoka Misri

na kuwakusanya toka Ashuru.

Nitawaleta katika nchi ya Gileadi na Lebanoni,

na hapo hapatakuwa na nafasi ya kuwatosha.

10:11 Isa 19:5-7; 51:10; Sef 2:13; Eze 29:15; 30:13Watapita katika bahari ya mateso;

bahari iliyochafuka itatulizwa

na vilindi vyote vya Mto Naili vitakauka.

Kiburi cha Ashuru kitashushwa,

nayo fimbo ya utawala ya Misri itatoweka.

10:12 Eze 30:24; Mik 4:5Nitawaimarisha katika Bwana,

na katika jina lake watatembea,”

asema Bwana.

Read More of Zekaria 10

Zekaria 11:1-17

11:1 Eze 31:3; 2Nya 36:19; Zek 12:6Fungua milango yako, ee Lebanoni,

ili moto uteketeze mierezi yako!

11:2 Isa 2:13; 32:19; 10:34Piga yowe, ee mti wa msunobari,

kwa kuwa mwerezi umeanguka;

miti ya fahari imeharibiwa!

Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani,

msitu mnene umefyekwa!

11:3 Isa 5:29; Yer 2:15; 50:44; Eze 19:9Sikiliza yowe la wachungaji;

malisho yao manono yameangamizwa!

Sikia ngurumo za simba;

kichaka kilichostawi sana

cha Yordani kimeharibiwa!

Wachungaji Wawili Wa Kondoo

11:4 Yer 25:34Hili ndilo asemalo Bwana Mungu wangu: “Lilishe kundi lililokusudiwa kuchinjwa. 11:5 Yer 50:7; Eze 34:2-3; Kum 29:19; Yer 2:3; Hos 12:8; Yn 16:2; 1Tim 6:9; 2Pet 2:3Wanunuzi wake huwachinja na kuondoka pasipo kuadhibiwa. Wale wanaowauza husema, ‘Bwana asifiwe, mimi ni tajiri!’ Wachungaji wao wenyewe hawawahurumii. 11:6 Zek 14:13; Isa 9:19-21; Yer 13:14; Mao 2:21; 5:8; Mik 5:8; 7:2-6Kwa kuwa sitawahurumia tena watu wa nchi,” asema Bwana. “Nitawakabidhi kila mtu mkononi mwa jirani yake na mfalme wake. Wataitenda jeuri nchi, nami sitawaokoa kutoka mikononi mwao.”

11:7 Yer 25:34; Sef 3:12; Mt 11:5Kwa hiyo nikalilisha kundi lililotiwa alama kwa kuchinjwa, hasa kundi lililoonewa sana. Kisha nikachukua fimbo mbili, moja nikaiita Fadhili na nyingine Umoja, nami nikalilisha kundi. 11:8 Eze 14:5; Hos 5:7Katika mwezi mmoja nikawaondoa wachungaji watatu.

Kundi la kondoo likanichukia, nami nikachoshwa nao, 11:9 Yer 43:11; 15:2; Isa 9:20nikasema, “Sitakuwa mchungaji wenu. Waache wanaokufa wafe na wanaoangamia waangamie. Wale waliobakia kila mmoja na ale nyama ya mwenzake.”

11:10 Za 89:39; Yer 14:21Kisha nikachukua fimbo yangu inayoitwa Fadhili nikaivunja, kutangua Agano nililofanya na mataifa yote. Likatanguka siku hiyo, kwa hiyo wale waliodhurika katika kundi, waliokuwa wakiniangalia wakajua kuwa hilo lilikuwa neno la Bwana.

11:12 Mwa 23:16; Mt 26:15; Kut 21:32Nikawaambia, “Mkiona kuwa ni vyema, nipeni ujira wangu, la sivyo, basi msinipe.” Kwa hiyo wakanilipa vipande thelathini vya fedha.

11:13 Kut 21:32; Mt 27:9-10; Mdo 1:18-19Naye Bwana akaniambia, “Mtupie mfinyanzi,” hiyo bei nzuri waliyonithaminia! Kwa hiyo nikachukua hivyo vipande thelathini vya fedha na kumtupia huyo mfinyanzi katika nyumba ya Bwana.

Kisha nikaivunja fimbo yangu ya pili iitwayo Umoja, kuvunja undugu kati ya Yuda na Israeli!

Kisha Bwana akaniambia, “Vitwae tena vifaa vya mchungaji mpumbavu. Kwa maana ninakwenda kumwinua mchungaji juu ya nchi ambaye hatamjali aliyepotea, wala kuwatafuta wale wachanga au kuwaponya waliojeruhiwa, wala kuwalisha wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo wanono na kuzirarua kwato zao.

11:17 Yer 23:1; Eze 30:21-22; Isa 13:1; Yn 10:12; Mik 3:6“Ole wa mchungaji asiyefaa,

anayeliacha kundi!

Upanga na uupige mkono wake na jicho lake la kuume!

Mkono wake na unyauke kabisa,

jicho lake la kuume lipofuke kabisa!”

Read More of Zekaria 11