Zekaria 5:1-11, Zekaria 6:1-15, Zekaria 7:1-14, Zekaria 8:1-23 NEN

Zekaria 5:1-11

Maono Ya Sita: Kitabu Kinachoruka

5:1 Za 10:7; Yer 36:4Nikatazama tena: na hapo mbele yangu kulikuwa na kitabu kilichoruka!

5:2 Yer 1:13Akaniuliza, “Unaona nini?”

Nikamjibu, “Naona kitabu kinachoruka chenye, urefu wa dhiraa ishirini5:2 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9. na upana wa dhiraa kumi.”5:2 Dhiraa 10 ni sawa mita 4.5.

5:3 Mal 3:9; Kut 20:15; 20:7; Isa 48:1Akaniambia, “Hii ni laana inayotoka kwenda juu ya nchi yote, kwa kuwa kufuatana na yale yaliyoandikwa katika upande mmoja, kila mwizi atafukuziwa mbali, pia kufuatana na yaliyo upande wa pili, kila aapaye kwa uongo atafukuziwa mbali. 5:4 Zek 8:17; Law 14:34-35; Mit 3:33; Hab 2:9-11; Mal 3:5Bwana Mwenye Nguvu Zote asema, ‘Nitaituma hiyo laana, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi na nyumba ya huyo aapaye kwa uongo kwa Jina langu. Itabaki katika nyumba yake na kuiharibu, pamoja na mbao zake na mawe yake.’ ”

Maono Ya Saba: Mwanamke Ndani Ya Kikapu

5:5 Mik 6:10Kisha yule malaika aliyekuwa akizungumza nami akanijia na kuniambia, “Tazama juu uone ni nini kile kinachojitokeza.”

Nikamuuliza, “Ni kitu gani?”

Akanijibu, “Ni kikapu cha kupimia.” Kisha akaongeza kusema, “Huu ni uovu wa watu katika nchi nzima.”

Kisha kifuniko kilichotengenezwa kwa madini ya risasi kilichokuwa kimefunika kile kikapu, kiliinuliwa na ndani ya kile kikapu alikuwako mwanamke ameketi! 5:8 Mit 6:11Akasema, “Huu ni uovu,” tena akamsukumia ndani ya kikapu na kushindilia kifuniko juu ya mdomo wa kikapu.

5:9 Law 11:19Kisha nikatazama juu: na pale mbele yangu, walikuwepo wanawake wawili, wakiwa na upepo katika mabawa yao! Walikuwa na mabawa kama ya korongo, nao wakainua kile kikapu na kuruka nacho kati ya mbingu na nchi.

Nikamuuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Wanakipeleka wapi hicho kikapu?”

5:11 Mwa 10:10; Yer 29:5, 28; Dan 1:2Akanijibu, “Wanakipeleka katika nchi ya Babeli na kujenga nyumba kwa ajili yake. Itakapokuwa tayari, kikapu kitawekwa pale mahali pake.”

Read More of Zekaria 5

Zekaria 6:1-15

Maono Ya Nane: Magari Manne Ya Vita

6:1 2Fal 2:12Nikatazama juu tena: nikaona mbele yangu magari manne ya vita yakija kutoka kati ya milima miwili, milima ya shaba! 6:2 Ufu 6:5; Zek 1:8Gari la kwanza lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na farasi weusi, 6:3 Ufu 6:2la tatu lilivutwa na farasi weupe na gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu. 6:4 Zek 5:10Nikamuuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Hawa ni nani bwana wangu?”

6:5 Eze 37:9; Mt 24:31; Yos 3:11; Za 68:17; Ebr 1:7; 1:7, 14; Dan 7:10; Lk 1:19Malaika akanijibu, “Hizi ni roho nne za mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya kazi yake. 6:6 Yer 1:14Gari linalovutwa na farasi weusi linaelekea katika nchi ya kaskazini, la farasi weupe linaelekea magharibi na la farasi wa madoadoa ya kijivu linaelekea kusini.”

6:7 Isa 43:6; Mwa 13:17Wakati hao farasi wenye nguvu walipokuwa wakitoka, walikuwa wakijitahidi kwenda duniani kote. Akasema, “Nenda duniani kote!” Kwa hiyo wakaenda duniani kote.

6:8 Mhu 10:4; Eze 5:13; 24:13; Zek 1:10Kisha akaniita, “Tazama, wale wanaokwenda kuelekea nchi ya kaskazini wamepumzisha Roho yangu katika nchi ya kaskazini.”

Taji Kwa Ajili Ya Yoshua

Neno la Bwana likanijia kusema: 6:10 Ezr 2:1; 7:14-16; Yer 28:6“Chukua fedha na dhahabu kutoka kwa watu waliohamishwa, yaani Heldai, Tobia na Yedaya ambao wamefika kutoka Babeli. Siku iyo hiyo nenda nyumbani kwa Yosia mwana wa Sefania. 6:11 Kut 28:36; Za 21:3; 1Nya 6:15; Ezr 2:2; 3:2; Zek 3:1Chukua fedha na dhahabu utengeneze taji, nawe uiweke kichwani mwa kuhani mkuu Yoshua, mwana wa Yehosadaki. 6:12 Isa 4:2; Eze 17:22; Ezr 3:8-10; Zek 4:6-9; Isa 9:6; Mik 5:5; Yer 23:5; 33:15; Zek 13:7; Mk 15:39; Lk 1:78; Yn 1:45; Za 80:15-17; Efe 2:20; Ebr 2:9Umwambie, hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Huyu ndiye mtu ambaye jina lake ni Tawi, naye atachipua kutoka mahali pake na kujenga Hekalu la Bwana. 6:13 Za 110:4; 21:5Ni yeye atakayejenga Hekalu la Bwana, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki katika kiti cha enzi naye atakuwa kuhani katika kiti chake cha enzi. Hapo patakuwa amani kati ya hao wawili.’ 6:14 Kut 28:12; Mk 14:9Taji itatolewa kwa Heldai, Tobia, Yedaya na Heni mwana wa Sefania kama kumbukumbu ndani ya Hekalu la Bwana. 6:15 Efe 2:13; Isa 60:10; Zek 2:9-11; Isa 58:12; Yer 7:23Wale walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga Hekalu la Bwana, nanyi mtajua ya kwamba Bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtii Bwana Mungu wenu kwa bidii.”

Read More of Zekaria 6

Zekaria 7:1-14

Haki Na Rehema, Sio Kufunga

7:1 Ezr 5:1; Neh 1:1Katika mwaka wa nne wa utawala wa Mfalme Dario, neno la Bwana lilimjia Zekaria siku ya nne ya mwezi wa tisa, mwezi wa Kisleu. 7:2 Yer 26:19; Zek 8:21; Hag 2:10-14Watu wa Betheli walikuwa wamemtuma Shareza na Regem-Meleki pamoja na watu wao, kumsihi Bwana 7:3 Zek 12:12-14; 2Fal 25:9; Yer 52:12-14; Kum 17:9; Mal 2:7kwa kuwauliza makuhani wa nyumba ya Bwana Mwenye Nguvu Zote na manabii, “Je, imempasa kuomboleza na kufunga katika mwezi wa tano, kama ambavyo nimekuwa nikifanya kwa miaka mingi?”

Kisha neno la Bwana Mwenye Nguvu Zote likanijia kusema: 7:5 Isa 58:5; 2Fal 25:25; Dan 9:2; Zek 1:12; Mt 6:16; Rum 14:6“Waulize watu wote wa nchi na makuhani, ‘Je, mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na wa saba kwa miaka sabini iliyopita, mlifunga kweli kwa ajili yangu? 7:6 Isa 43:23Na mlipokuwa mkila na kunywa, je, hamkuwa mnasherehekea kwa ajili ya nafsi zenu? 7:7 Isa 1:11-20; Yer 22:21; 17:26; 44:4-5Je, haya sio maneno ya Bwana aliyosema kupitia manabii waliotangulia, wakati Yerusalemu pamoja na miji inayoizunguka ilipokuwa katika hali ya utulivu na ya mafanikio, wakati Negebu na Shefala zikiwa zimekaliwa na watu?’ ”

Neno la Bwana likamjia tena Zekaria: 7:9 Yer 22:3; 42:5; Zek 8:16; Kum 22:1“Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Fanyeni hukumu za haki, onyesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi. 7:10 Yer 49:11; Kut 22:21-22; Law 25:17; Isa 1:23; Ay 35:8; Eze 45:9; Mik 6:8Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’

7:11 Isa 9:9; Yer 32:33; 11:10; 17:23; 8:5; Eze 5:6“Lakini wakakataa kusikiliza, wakanipa kisogo kwa ukaidi na kuziba masikio yao. 7:12 Yer 5:3; 17:1; 42:21; Eze 11:19; Neh 9:29; Dan 9:12Wakaifanya mioyo yao migumu kama jiwe gumu na hawakuisikiliza sheria au maneno ambayo Bwana Mwenye Nguvu Zote aliyatuma kwa njia ya Roho wake kupitia manabii waliotangulia. Kwa hiyo Bwana Mwenye Nguvu Zote alikasirika sana.

7:13 Yer 7:27; 11:11; 14:12; Mit 1:28; Isa 1:15; Mao 3:44; Eze 20:31“ ‘Wakati nilipoita, hawakusikiliza, kwa hiyo walipoita, sikusikiliza,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 7:14 Kum 4:27; 28:64-67; Law 26:33; Yer 7:34; 23:19; 44:6; Za 44:11; Isa 33:8; Eze 12:19‘Niliwatawanya kwa upepo wa kisulisuli miongoni mwa mataifa yote, mahali ambapo walikuwa wageni. Nchi ikaachwa ukiwa nyuma yao kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuingia au kutoka. Hivi ndivyo walivyoifanya ile nchi iliyokuwa imependeza kuwa ukiwa.’ ”

Read More of Zekaria 7

Zekaria 8:1-23

Bwana Anaahidi Kuibariki Yerusalemu

Neno la Bwana Mwenye Nguvu Zote likanijia tena. 8:2 Yoe 2:18; Nah 1:2Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Nina wivu sana kwa ajili ya Sayuni, ninawaka wivu kwa ajili yake.”

8:3 Zek 1:16; Isa 1:26; 48:1; 52:8; Yoe 3:21; Zek 2:10; Za 15:2; Yer 33:16; Mik 4:1; Za 48:1-2; Yer 31:23Hili ndilo asemalo Bwana: “Nitarudi Sayuni na kufanya makao Yerusalemu. Kisha Yerusalemu utaitwa mji wa kweli, mlima wa Bwana Mwenye Nguvu Zote utaitwa Mlima Mtakatifu.”

8:4 Isa 65:20; 1Sam 2:31Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Kwa mara nyingine tena wazee wanaume kwa wanawake walioshiba umri wataketi katika barabara za Yerusalemu, kila mmoja akiwa na mkongojo wake mkononi kwa sababu ya umri wake. 8:5 Yer 30:20; 31:13Barabara za mji zitajaa wavulana na wasichana wanaocheza humo.”

8:6 Za 118:23; 126:1-3; Yer 32:17, 27; Hes 11:23; Ay 42:2; Lk 1:37; Rum 4:21Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Mambo haya yanaweza kuonekana ya ajabu kwa mabaki ya watu wakati huo, lakini yaweza kuwa ya ajabu kwangu?” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

8:7 Za 107:3; Isa 11:11; 43:5Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi za mashariki na magharibi. 8:8 Eze 11:19-20; 36:28; 37:12; Zek 2:11; 10:10; Yer 11:4; 31:24; Isa 51:16; Ebr 8:10; Law 25:17; Yer 4:2; Zek 4:2; 13:9; Ufu 21:3Nitawarudisha waje kuishi Yerusalemu, watakuwa watu wangu nami nitakuwa mwaminifu na wa haki kwao kama Mungu wao.”

8:9 Ezr 5:1; 3:11; Hag 2:4Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Ninyi ambao sasa mnasikia maneno haya yanayozungumzwa na manabii ambao walikuwepo wakati wa kuwekwa kwa msingi wa nyumba ya Bwana Mwenye Nguvu Zote, mikono yenu na iwe na nguvu ili Hekalu liweze kujengwa. 8:10 Isa 5:10; Hag 1:6; 2Nya 15:5Kabla ya wakati huo, hapakuwepo na ujira kwa mtu wala mnyama. Hakuna mtu aliyeweza kufanya shughuli yake kwa usalama kwa sababu ya adui yake, kwa kuwa nilikuwa nimemfanya kila mtu adui wa jirani yake. 8:11 Isa 12:1Lakini sasa sitawatendea mabaki ya watu hawa kama nilivyowatenda zamani,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

8:12 Za 65:13; 85:12; Yoe 2:22; Za 67:6; Mwa 27:28; Isa 60:21; Hos 2:21; Oba 1:17; Isa 61:7; Mt 6:33; 1Tim 4:8“Mbegu itakua vizuri, mzabibu utazaa matunda yake, ardhi itatoa mazao yake, na mbingu zitadondosha umande wake. Vitu hivi vyote nitawapa mabaki ya watu kama urithi wao. 8:13 Hes 5:27; Kum 13:15; Yer 42:18; Za 102:8; 48:8; Mwa 12:2; Yoe 2:14; Hag 2:5; Efe 6:10Jinsi mlivyokuwa kitu cha laana katikati ya mataifa, ee Yuda na Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka. Msiogope, bali iacheni mikono yenu iwe na nguvu.”

8:14 Eze 24:14; Yer 31:28; 2Nya 36:16Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Kama nilivyokuwa nimekusudia kuleta maangamizi juu yenu, wakati baba zenu waliponikasirisha na sikuonyesha huruma,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, 8:15 Yer 29:11; 31:28; 32:42; Mik 7:18-20“hivyo sasa nimeazimia kufanya mema tena kwa Yerusalemu na Yuda. Msiogope. 8:16 Za 15:2; Yer 33:16; Eze 18:8; 45:9; Amo 5:15; Zek 7:9; Efe 4:25; Mit 12:19Haya ndiyo mtakayoyafanya: Semeni kweli kila mtu kwa mwenzake, na mtoe hukumu ya kweli na haki kwenye mahakama zenu, 8:17 Mit 3:29; 6:16-19; Yer 7:9; Zek 5:4usipange mabaya dhidi ya jirani yako, wala msipende kuapa kwa uongo. Nayachukia yote haya,” asema Bwana.

Neno la Bwana Mwenye Nguvu Zote likanijia tena. 8:19 2Fal 25:7, 25; Yer 39:2; 52:4, 12; Za 30:11; Yer 41:1; Isa 35:10Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Saumu za miezi ya nne, tano, saba na kumi itakuwa sikukuu za furaha na za shangwe kwa Yuda. Kwa hiyo uipende kweli na amani.”

Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Mataifa mengi na wakazi wa miji mingi watakuja, 8:21 Zek 7:2; Yer 26:19na wenyeji wa mji mmoja watakwenda kwenye mji mwingine na kusema, ‘Twende mara moja na tukamsihi Bwana, na kumtafuta Bwana Mwenye Nguvu Zote. Mimi mwenyewe ninakwenda.’ 8:22 Za 86:9; 117:1; Isa 2:2-3; 44:5; 45:14; 49:6; Zek 2:11Pia watu wa kabila nyingi na mataifa yenye nguvu yatakuja Yerusalemu kumtafuta Bwana Mwenye Nguvu Zote na kumsihi.”

8:23 Za 102:22; Isa 13:1; 14:1; 45:14; 56:3; 1Kor 14:25; Yer 23:33Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Katika siku hizo watu kumi kutoka lugha zote na mataifa, watangʼangʼania upindo wa joho la Myahudi mmoja na kusema, ‘Twende pamoja nawe kwa sababu tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nawe.’ ”

Read More of Zekaria 8