Wimbo 5:1-16, Wimbo 6:1-13, Wimbo 7:1-13, Wimbo 8:1-14 NEN

Wimbo 5:1-16

Mpenzi

5:1 Yoe 3:18; Wim 4:12; 4:16; Isa 55:1Nimekuja kwenye bustani yangu, dada yangu,

bibi arusi wangu;

nimekusanya manemane yangu pamoja

na kikolezo changu.

Nimekula sega langu la asali na asali yangu;

nimekunywa divai yangu na maziwa yangu.

Marafiki

Kuleni, enyi marafiki, mnywe;

kunyweni ya kutosha, ee wapenzi.

Shairi La Nne

Mpendwa

5:2 Efe 5:275:2 Mit 8:4; Wim 6:9; 4:7; 1:15Nililala lakini moyo wangu ulikuwa macho.

Sikiliza! Mpenzi wangu anabisha:

“Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu,

hua wangu, asiye na hitilafu.

Kichwa changu kimeloa umande,

na nywele zangu manyunyu ya usiku.”

Nimevua joho langu:

je, ni lazima nivae tena?

Nimenawa miguu yangu:

je, ni lazima niichafue tena?

Mpenzi wangu aliweka mkono wake kwenye tundu la komeo;

moyo wangu ulianza kugonga kwa ajili yake.

Niliinuka kumfungulia mpenzi wangu,

mikono yangu ikidondosha manemane,

vidole vyangu vikitiririka manemane,

penye vipini vya komeo.

5:6 Wim 6:1-2; 3:15:6 Hos 5:15; Mao 3:8Nilimfungulia mpenzi wangu,

lakini mpenzi wangu alishaondoka;

alikuwa amekwenda zake.

Moyo wangu ulishuka kwa kuondoka kwake.

Nilimtafuta lakini sikumpata.

Nilimwita lakini hakunijibu.

5:7 Wim 3:3Walinzi walinikuta

walipokuwa wakifanya zamu za ulinzi mjini.

Walinipiga, wakanijeruhi,

wakaninyangʼanya joho langu,

hao walinzi wa kuta!

5:8 Wim 2:7; 1:14; 2:5Enyi binti za Yerusalemu, ninawaagiza:

kama mkimpata mpenzi wangu,

mtamwambia nini?

Mwambieni ninazimia kwa mapenzi.

Marafiki

Je, mpendwa wako ni bora kuliko wengine namna gani,

wewe uliye mzuri kupita wanawake wote?

Je, mpendwa wako ni mzuri kuliko wengine, namna gani,

hata unatuagiza hivyo?

Mpendwa

5:10 Za 45:2Mpenzi wangu anangʼaa, tena ni mwekundu,

wa kuvutia miongoni mwa wanaume kumi elfu.

Kichwa chake ni dhahabu safi kuliko zote,

nywele zake ni za mawimbi

na ni nyeusi kama kunguru.

5:12 Mwa 49:12; Wim 1:15Macho yake ni kama ya hua

kandokando ya vijito vya maji,

aliyeogeshwa kwenye maziwa,

yaliyopangwa kama vito vya thamani.

Mashavu yake ni kama matuta ya vikolezo

yakitoa manukato.

Midomo yake ni kama yungiyungi

inayodondosha manemane.

5:14 Ay 28:6Mikono yake ni fimbo za dhahabu

iliyopambwa kwa krisolitho.

Mwili wake ni kama pembe ya ndovu iliyongʼarishwa

iliyopambwa na yakuti samawi.

5:15 1Fal 4:33; Wim 7:4Miguu yake ni nguzo za marmar

zilizosimikwa katika vitako vya dhahabu safi.

Sura yake ni kama Lebanoni,

bora kama miti yake ya mierezi.

5:16 Wim 4:3; 7:9; Yer 31:3; Rum 8:35Kinywa chake chenyewe ni utamu,

kwa ujumla yeye ni wa kupendeza.

Huyu ndiye mpenzi wangu, huyu ndiye rafiki yangu,

ee binti za Yerusalemu.

Read More of Wimbo 5

Wimbo 6:1-13

Marafiki

6:1 Wim 1:8; 5:6Mpenzi wako amekwenda wapi,

ewe mzuri kupita wanawake wote?

Mpenzi wako amegeukia njia ipi,

tupate kumtafuta pamoja nawe?

Mpendwa

6:2 Sef 3:17; Isa 40:11; Wim 4:12; 5:13; 5:6Mpenzi wangu amekwenda bustanini mwake,

kwenye vitalu vya vikolezo,

kujilisha bustanini

na kukusanya yungiyungi.

6:3 Wim 7:10; 2:16Mimi ni wake mpenzi wangu,

na mpenzi wangu ni wangu;

yeye hujilisha katikati ya yungiyungi.

Shairi La Tano

Mpenzi

6:4 2Kor 10:4; 1Fal 15:33; Yos 12; 24; Za 48:2; Hes 1:52; Za 50:2Wewe ni mzuri, mpenzi wangu, kama Tirsa,

upendezaye kama Yerusalemu,

umetukuka kama jeshi lenye bendera.

Uyageuze macho yako mbali nami,

yananigharikisha.

Nywele zako ni kama kundi la mbuzi

wanaoteremka kutoka Gileadi.

Meno yako ni kama kundi la kondoo

watokao kuogeshwa.

Kila mmoja ana pacha lake,

hakuna hata mmoja aliye peke yake.

6:7 Mwa 24:65; Wim 4:3Mashavu yako nyuma ya shela yako

ni kama vipande viwili vya komamanga.

6:8 Za 45:9; Mwa 22:24; Es 2:14Panaweza kuwepo malkia sitini,

masuria themanini

na mabikira wasiohesabika;

6:9 Wim 1:15; 5:2; 3:4lakini hua wangu, mkamilifu wangu,

ni wa namna ya pekee,

binti pekee kwa mama yake,

kipenzi cha yeye aliyemzaa.

Wanawali walimwona na kumwita aliyebarikiwa;

malkia na masuria walimsifu.

Marafiki

Ni nani huyu atokeaye kama mapambazuko,

mzuri kama mwezi, mwangavu kama jua,

ametukuka kama nyota zifuatanazo?

Mpenzi

6:11 Wim 7:12Niliteremka kwenye bustani ya miti ya milozi

ili kutazama machipuko ya bondeni,

kuona kama mizabibu imechipua

au kama mikomamanga imechanua maua.

Kabla sijangʼamua,

shauku yangu iliniweka

katikati ya magari ya kifalme ya kukokotwa na farasi ya watu wangu.

Marafiki

6:13 Kut 15:20Rudi, rudi, ee Mshulami;

rudi, rudi ili tupate kukutazama!

Mpenzi

Kwa nini kumtazama Mshulami,

kama kutazama ngoma ya Mahanaimu?6:13 Mahanaimu hapa ina maana ya majeshi mawili.

Read More of Wimbo 6

Wimbo 7:1-13

7:1 Za 45:13Ee binti wa mwana wa mfalme,

tazama jinsi inavyopendeza miguu yako katika viatu!

Miguu yako yenye madaha ni kama vito vya thamani,

kazi ya mikono ya fundi stadi.

Kitovu chako ni kama bilauri ya mviringo

ambayo kamwe haikosi divai iliyochanganywa.

Kiuno chako ni kichuguu cha ngano

kilichozungukwa kwa yungiyungi.

7:3 Wim 4:5Matiti yako ni kama wana-paa wawili,

mapacha wa paa.

7:4 Hes 21:26; Wim 4:4; 5:15; Za 144:12Shingo yako ni kama mnara wa pembe ya ndovu.

Macho yako ni vidimbwi vya Heshboni

karibu na lango la Beth-Rabi.

Pua lako ni kama mnara wa Lebanoni

ukitazama kuelekea Dameski.

7:5 Isa 35:2Kichwa chako kinakuvika taji kama mlima Karmeli.

Nywele zako ni kama zulia la urujuani;

mfalme ametekwa na mashungi yake.

7:6 Wim 1:15; 4:10Tazama jinsi ulivyo mzuri na unavyopendeza,

ee pendo, kwa uzuri wako!

7:7 Wim 4:5Umbo lako ni kama la mtende,

nayo matiti yako kama vishada vya matunda.

7:8 Wim 2:5Nilisema, “Nitakwea mtende,

nami nitayashika matunda yake.”

Matiti yako na yawe kama vishada vya mzabibu,

harufu nzuri ya pumzi yako kama matofaa,

7:9 Wim 5:16na kinywa chako kama divai

bora kuliko zote.

Mpendwa

Divai na iende moja kwa moja hadi kwa mpenzi wangu,

ikitiririka polepole juu ya midomo na meno.

7:10 Wim 2:16; 6:3; Za 45:11; Gal 2:20Mimi ni mali ya mpenzi wangu,

nayo shauku yake ni juu yangu.

Njoo, mpenzi wangu, twende mashambani,

twende tukalale huko vijijini.

7:12 Za 63:3-8; Wim 6:11; 4:13; 2:13-15Hebu na twende mapema

katika mashamba ya mizabibu

tuone kama mizabibu imechipua,

kama maua yake yamefunguka,

na kama mikomamanga imetoa maua:

huko nitakupa penzi langu.

7:13 Gal 5:227:13 Mwa 30:14; Wim 4:16Mitunguja hutoa harufu zake nzuri,

kwenye milango yetu kuna matunda mazuri,

mapya na ya zamani,

ambayo nimekuhifadhia wewe,

mpenzi wangu.

Read More of Wimbo 7

Wimbo 8:1-14

8:1 Mit 9:2; Wim 3:4Laiti ungelikuwa kwangu kama ndugu wa kiume,

ambaye aliyanyonya matiti ya mama yangu!

Kisha, kama ningekukuta huko nje,

ningelikubusu,

wala hakuna mtu yeyote angelinidharau.

Ningelikuongoza na kukuleta

katika nyumba ya mama yangu,

yeye ambaye amenifundisha.

Ningelikupa divai iliyokolezwa unywe,

asali ya maua ya mikomamanga yangu.

8:3 Wim 2:6Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu,

na mkono wake wa kuume unanikumbatia.

8:4 Wim 2:7; 3:5Binti za Yerusalemu, ninawaagiza:

msichochee wala kuamsha mapenzi

hata yatakapotaka yenyewe.

Shairi La Sita

Marafiki

8:5 Wim 3:4-6; Yn 17:14Ni nani huyu anayekuja kutoka nyikani

akimwegemea mpenzi wake?

Mpendwa

Nilikuamsha chini ya mtofaa,

huko mama yako alipotunga mimba yako,

huko yeye alipata utungu akakuzaa.

8:6 Wim 1:2; Hes 5:14; Hag 2:23; Isa 49:16Nitie kama muhuri moyoni mwako,

kama muhuri kwenye mkono wako;

kwa maana upendo una nguvu kama mauti,

wivu wake ni mkatili kama kuzimu.

Unachoma kama mwali wa moto,

kama mwali mkubwa wa moto wa Bwana hasa.

8:7 Mit 6:35Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,

mito haiwezi kuugharikisha.

Kama mtu angelitoa mali yote ya nyumbani mwake

kwa ajili ya upendo,

angelidharauliwa kabisa.

Marafiki

Tunaye dada mdogo,

matiti yake hayajakua bado.

Tutafanya nini kwa ajili ya dada yetu

wakati atakapokuja kuposwa?

Kama yeye ni ukuta,

tutajenga minara ya fedha juu yake.

Na kama yeye ni mlango,

tutamzungushia mbao za mierezi.

Mpendwa

8:10 Kol 2:7; Eze 16:7Mimi ni ukuta,

nayo matiti yangu ni kama minara.

Ndivyo ambavyo nimekuwa machoni pake

kama yule anayeleta utoshelevu.

8:11 Mhu 2:4; Mt 21:33; Isa 7:23Solomoni alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-Hamoni;

alikodisha shamba lake la mizabibu kwa wapangaji.

Kila mmoja angeleta kwa ajili ya matunda yake

shekeli 1,0008:11 Shekeli 1,000 ni kama kilo 11.5. za fedha.

Lakini shamba langu la mizabibu

ambalo ni langu mwenyewe

ni langu kutoa;

hizo shekeli 1,000 ni kwa ajili yako, ee Solomoni,

na shekeli mia mbili8:12 Shekeli 200 ni kama kilo 2.3. ni kwa ajili

ya wale wanaotunza matunda yake.

Mpenzi

8:13 Wim 2:14Wewe ukaaye bustanini

pamoja na marafiki mliohudhuria,

hebu nisikie sauti yako!

Mpendwa

8:14 Mit 5:19; Wim 2:8-17Njoo, mpenzi wangu,

uwe kama swala

au kama ayala kijana

juu ya milima iliyojaa vikolezo.

Read More of Wimbo 8