Wimbo 1:1-17, Wimbo 2:1-17, Wimbo 3:1-11, Wimbo 4:1-16 NEN

Wimbo 1:1-17

1:1 1Fal 4:32; Za 45Wimbo ulio bora wa Solomoni.

Shairi La Kwanza

Mpendwa

1:2 Wim 8:6; Mwa 14:18; Amu 9:13; Wim 4:10Unibusu kwa busu la kinywa chako,

kwa maana upendo wako unafurahisha kuliko divai.

1:3 Es 2:12; Za 45:8-14; Mhu 7:1Manukato yako yananukia vizuri,

jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa.

Ndiyo sababu wanawali wanakupenda!

1:4 Yer 31:3; Flp 3:12; Wim 2:3Nichukue twende nawe, na tufanye haraka!

Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake.

Marafiki

Tunakushangilia na kukufurahia,

tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai.

Mpendwa

Tazama jinsi ilivyo bora wakupende!

1:5 Wim 2:14; 2:7; 5:16; 4:3; Mwa 25:13Mimi ni mweusi, lakini napendeza,

enyi binti za Yerusalemu,

mweusi kama mahema ya Kedari,

kama mapazia ya hema la Solomoni.

1:6 Za 69:8; Wim 7:12; 8:12; 2:15Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi,

kwa sababu nimefanywa mweusi na jua.

Wana wa mama yangu walinikasirikia

na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu.

Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha.

1:7 Wim 3:1-4; Isa 13:20; Mwa 24:65Niambie, wewe ambaye ninakupenda,

unalisha wapi kundi lako la kondoo

na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri.

Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shela

karibu na makundi ya rafiki zako?

Marafiki

1:8 Wim 5:9; 6:1Kama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko wote,

fuata nyayo za kondoo,

na kulisha wana-mbuzi wako

karibu na hema za wachungaji.

Mpenzi

1:9 Wim 2:2; 2Nya 1:16-17Mpenzi wangu, ninakufananisha na farasi jike

aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao.

1:10 Eze 16:11; Isa 61:10; Wim 5:13Mashavu yako yanapendeza yakiwa na vipuli,

shingo yako ikiwa na mikufu ya vito.

Tutakufanyia vipuli vya dhahabu,

vyenye kupambwa kwa fedha.

Mpendwa

1:12 Wim 4:11-14Wakati mfalme alipokuwa mezani pake,

manukato yangu yalisambaza harufu yake nzuri.

1:13 Mwa 37:25Mpenzi wangu kwangu mimi ni kifuko cha manemane

kati ya matiti yangu.

1:14 Wim 4:13; 1Sam 23:291:14 2Nya 20:2; Wim 2:3; 5:8Mpenzi wangu kwangu mimi ni kama kishada cha maua ya mhina

kutoka mashamba ya mizabibu ya En-Gedi.

Mpenzi

1:15 Wim 4:7; 7:6; Za 74:19; Yer 48:28Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!

Tazama jinsi ulivyo mzuri!

Macho yako ni kama ya hua.

Mpendwa

Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!

Ee, tazama jinsi unavyopendeza!

Na kitanda chetu ni cha majani mazuri.

Mpenzi

1:17 1Fal 6:9Nguzo za nyumba yetu ni mierezi,

na mapao yetu ni miberoshi.

Read More of Wimbo 1

Wimbo 2:1-17

Mpendwa

2:1 1Nya 27:29; Hos 14:5; Wim 5:13; Isa 55:1Mimi ni ua la Sharoni,

yungiyungi ya bondeni.

Mpenzi

Kama yungiyungi katikati ya miiba

ndivyo alivyo mpenzi wangu katikati ya wanawali.

Mpendwa

2:3 Mwa 3:6; Wim 1:4, 14; 4:16Kama mti wa mtofaa miongoni mwa miti ya msituni

ndivyo alivyo mpenzi wangu

miongoni mwa wanaume vijana.

Ninafurahia kuketi kivulini mwa mwanaume huyu,

na tunda lake ni tamu kwangu.

2:4 Es 1:11; Hes 1:52Amenichukua mpaka kwenye ukumbi wa karamu,

na bendera ya huyu mwanaume

juu yangu ni upendo.

2:5 Wim 7:8; 5:8Nitie nguvu kwa zabibu kavu,

niburudishe kwa matofaa,

kwa maana ninazimia kwa mapenzi.

2:6 Wim 8:3Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu,

na mkono wake wa kuume unanikumbatia.

2:7 Wim 5:8; 3:5; 8:4Binti za Yerusalemu, ninawaagiza

kwa paa na kwa ayala wa shambani:

Msichochee wala kuamsha mapenzi

hata yatakapotaka yenyewe.

Shairi La Pili

Mpendwa

2:8 Wim 8:14Sikiliza! Mpenzi wangu!

Tazama! Huyu hapa anakuja,

akirukaruka juu milimani

akizunguka juu ya vilima.

2:9 2Sam 2:18; Wim 8:14Mpenzi wangu ni kama paa au ayala kijana.

Tazama! Anasimama nyuma ya ukuta wetu,

akitazama kupitia madirishani,

akichungulia kimiani.

Mpenzi wangu alizungumza na kuniambia,

“Inuka, mpenzi wangu,

mrembo wangu, tufuatane.

Tazama! Wakati wa masika umepita,

mvua imekwisha na ikapita.

Maua yanatokea juu ya nchi;

majira ya kuimba yamewadia,

sauti za njiwa zinasikika

katika nchi yetu.

2:13 Nah 3:12; Wim 7:122:13 Mik 7:1; Isa 28:4; Yer 24:2; Hos 9:10Mtini unatunga matunda yake ya mwanzoni,

zabibu zinazochanua zaeneza harufu nzuri.

Inuka, njoo mpenzi wangu.

Mrembo wangu, tufuatane.”

Mpenzi

2:14 Wim 8:13; Mwa 8:8; Wim 1:15Hua wangu penye nyufa za majabali,

mafichoni pembezoni mwa mlima,

nionyeshe uso wako,

na niisikie sauti yako,

kwa maana sauti yako ni tamu,

na uso wako unapendeza.

2:15 Amu 15:4; Wim 7:12; Eze 13:4; Za 80:13Tukamatie mbweha,

mbweha wale wadogo

wanaoharibu mashamba ya mizabibu,

mashamba yetu ya mizabibu yaliyochanua.

Mpendwa

2:16 Wim 7:10; 4:5; 6:3Mpenzi wangu ni wangu, nami ni wake,

yeye hujilisha katikati ya yungiyungi.

2:17 Wim 4:6; 1:14; Rum 13:12Mpaka jua linapochomoza,

na vivuli vikimbie,

rudi, mpenzi wangu,

na uwe kama paa,

au kama ayala kijana

juu ya vilima vya Betheri.

Read More of Wimbo 2

Wimbo 3:1-11

3:1 Isa 26:9; Wim 5:6Usiku kucha kwenye kitanda changu

nilimtafuta yule moyo wangu umpendaye;

nilimtafuta, lakini sikumpata.

Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini,

katika barabara zake na viwanja;

nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye.

Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata.

3:3 Wim 5:7; Isa 21:6-11Walinzi walinikuta

walipokuwa wakizunguka mji.

Nikawauliza, “Je, mmemwona

yule moyo wangu umpendaye?”

3:4 Wim 8:2; 6:9; 8:5; Rum 8:35-39; Mit 8:17; 4:13Kitambo kidogo tu baada ya kuwapita

nilimpata yule moyo wangu umpendaye.

Nilimshika na sikumwachia aende

mpaka nilipomleta katika nyumba ya mama yangu,

katika chumba cha yule aliyenichukua mimba.

3:5 Wim 2:7; 8:4Binti za Yerusalemu, ninawaagiza

kwa paa na kwa ayala wa shambani:

Msichochee wala kuamsha mapenzi

hata yatakapotaka yenyewe.

Shairi La Tatu

Mpenzi

3:6 Wim 8:6; 4:6, 14; Kut 30:34; Yer 2:2Ni nani huyu anayekuja kutoka jangwani

kama nguzo ya moshi,

anayenukia manemane na uvumba

iliyotengenezwa kwa vikolezo vyote

vya mfanyabiashara?

3:7 1Sam 8:11Tazama! Ni gari la Solomoni

lisindikizwalo na mashujaa sitini,

walio wakuu sana wa Israeli,

3:8 Ay 15:22; Za 91:5wote wamevaa panga,

wote wazoefu katika vita,

kila mmoja na upanga wake pajani,

wamejiandaa kwa ajili ya hofu za usiku.

Mfalme Solomoni alijitengenezea gari;

alilitengeneza kwa mbao kutoka Lebanoni.

3:10 Mt 22:37; Efe 3:19; Rum 5:8Nguzo zake alizitengeneza kwa fedha,

kitako chake kwa dhahabu.

Kiti chake kilipambwa kwa zambarau,

gari lake likanakshiwa njumu kwa upendo

na binti za Yerusalemu.

3:11 Isa 3:16; 54:5; 32:9-13; 62:5; Yer 3:14Tokeni nje, ninyi binti za Sayuni,

mkamtazame Mfalme Solomoni akiwa amevaa taji,

taji ambalo mama yake alimvika

siku ya arusi yake,

siku ambayo moyo wake ulishangilia.

Read More of Wimbo 3

Wimbo 4:1-16

Mpenzi

4:1 Wim 1:15; 5:12; Mwa 37:25; Hes 32:1; Mwa 24:65; Yer 22:6; Mik 7:14Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu!

Ee, jinsi ulivyo mzuri!

Macho yako nyuma ya shela yako

ni kama ya hua.

Nywele zako ni kama kundi la mbuzi

zikishuka kutoka Mlima Gileadi.

4:2 Wim 6:6Meno yako ni kama kundi la kondoo waliokatwa manyoya sasa hivi,

watokao kuogeshwa.

Kila mmoja ana pacha lake,

hakuna hata mmoja aliye peke yake.

4:3 Wim 5:16; 6:7Midomo yako ni kama uzi mwekundu,

kinywa chako kinapendeza.

Mashavu yako nyuma ya shela yako

ni kama vipande viwili vya komamanga.

4:4 Eze 27:10; Neh 3:19; 2Sam 22:51; Za 144:12Shingo yako ni kama mnara wa Daudi,

uliojengwa kwa madaha,

juu yake zimetundikwa ngao elfu,

zote ni ngao za mashujaa.

4:5 Wim 7:3; 6:2-3; Mit 5:19; Isa 66:10-12Matiti yako mawili ni kama wana-paa wawili,

kama wana-paa mapacha

wajilishao katikati ya yungiyungi.

4:6 Wim 2:6-7; 3:6; 2:17Hata kupambazuke na vivuli vikimbie,

nitakwenda kwenye mlima wa manemane

na kwenye kilima cha uvumba.

4:7 Wim 1:15Wewe ni mzuri kote, mpenzi wangu,

hakuna hitilafu ndani yako.

4:8 Kum 3:9; 1Nya 5:23; Wim 5:1Enda nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu,

enda nami kutoka Lebanoni.

Shuka kutoka ncha ya Amana,

kutoka juu ya Seniri, kilele cha Hermoni,

kutoka mapango ya simba

na kutoka mlima wapendapo kukaa chui.

4:9 Isa 54:5; Za 73:6; Yn 3:29; Mwa 41:43Umeiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu;

umeiba moyo wangu

kwa mtazamo mmoja wa macho yako,

kwa kito kimoja cha mkufu wako.

4:10 Wim 7:6; 1:2; Amu 9:13; Za 45:8; Isa 57:9Tazama jinsi pendo lako linavyofurahisha,

dada yangu, bibi arusi wangu!

Pendo lako linafurahisha aje zaidi ya divai,

na harufu ya manukato yako zaidi ya kikolezo chochote!

4:11 Hos 14:6; Za 19:10; Mit 24:13-14; Mwa 27:27Midomo yako inadondosha utamu kama sega la asali,

bibi arusi wangu;

maziwa na asali viko chini ya ulimi wako.

Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya Lebanoni.

4:12 Mit 5:15-18; Isa 58:11; Wim 6:2; 5:1Wewe ni bustani iliyofungwa, dada yangu,

bibi arusi wangu;

wewe ni chanzo cha maji kilichozungushiwa kabisa,

chemchemi yangu peke yangu.

4:13 Wim 6:11; 7:12; 1:14Mimea yako ni bustani ya mikomamanga

yenye matunda mazuri sana,

yenye hina na nardo,

4:14 Kut 30:23; Wim 3:6; 1:12; Hes 24:6nardo na zafarani,

mchai na mdalasini,

pamoja na kila aina ya mti wa uvumba,

manemane na udi,

na aina zote za vikolezo bora kuliko vyote.

4:15 Isa 27:2; 58:11; Yer 31:12; Mit 5:18Wewe ni chemchemi ya bustani,

kisima cha maji yatiririkayo,

yakitiririka kutoka Lebanoni.

Mpendwa

4:16 Wim 2:3Amka, upepo wa kaskazini,

na uje, upepo wa kusini!

Vuma juu ya bustani yangu,

ili harufu yake nzuri iweze kuenea mpaka ngʼambo.

Mpendwa wangu na aje bustanini mwake

na kuonja matunda mazuri sana.

Read More of Wimbo 4