Ruthu 3:1-18, Ruthu 4:1-22 NEN

Ruthu 3:1-18

Ruthu Na Boazi Kwenye Sakafu Ya Kupuria

3:1 Rut 1:9, 14, 19; 1Kor 7:36; 1Tim 5:8; Kum 4:40; Za 128:2; Yer 22:15, 16Kisha Naomi akamwambia mkwewe, “Binti yangu, je, nisingelikutafutia pumziko ambako utatunzika vyema? 3:2 Rut 2:1, 8; Law 2:14; Hes 18:27; Amu 6:11Je, Boazi, ambaye umekuwa pamoja na watumishi wake wasichana, si jamaa yetu wa karibu? Usiku wa leo atakuwa anapepeta ngano kwenye sakafu ya kupuria. 3:3 2Sam 12:20; 14:2; 2Fal 5:10; Za 26:6; 51:2; Isa 1:16; 61:3; Yer 4:14; Eze 16:9; Mwa 41:14; Kut 32:6; Mhu 2:3; Yer 15:17Basi oga na ukajipake marashi, ujivalie nguo zako nzuri. Kisha uende kwenye sakafu ya kupuria, lakini angalia asijue kwamba upo pale mpaka atakapomaliza kula na kunywa. Atakapokwenda kulala, angalia mahali atakapolala. Kisha uende ufunue miguu yake, ulale. Naye atakuambia utakalofanya.”

3:5 Efe 6:1; Kol 3:20Ruthu akajibu, “Lolote usemalo nitatenda.” 3:6 Hes 18:27Basi akashuka mpaka kwenye sakafu ya kupuria, akafanya kila kitu mama mkwe wake alichomwambia kufanya.

3:7 Amu 19:6; 1Sam 25:36; 2Sam 13:28; 1Fal 21:7; Es 1:10; Wim 7:2; 2Nya 31:6; Yer 50:26; Hag 2:16Wakati Boazi alipomaliza kula na kunywa, naye akawa amejawa na furaha, alikwenda kulala mwisho wa lundo la nafaka. Ruthu akanyemelea polepole, akafunua miguu yake, na akalala. Usiku wa manane, kitu kilimshtua Boazi, akajigeuza, akagundua yupo mwanamke amelala miguuni pake.

3:9 Eze 16:8; Rut 2:20Akauliza, “Wewe ni nani?”

Akajibu, “Ni mimi Ruthu, mjakazi wako. Uitande nguo yako juu yangu, kwa sababu wewe ndiwe jamaa wa karibu wa kutukomboa.”

3:10 Amu 17:2; Yos 2:12Akamwambia, “Binti yangu, ubarikiwe na Bwana. Wema huu wa sasa ni mkuu kushinda hata ule ulioonyesha mwanzoni. Hukuwakimbilia vijana, wakiwa matajiri au maskini. 3:11 Mit 12:4; 14:1; 31:10Sasa, binti yangu, usiogope. Nitakufanyia yote uliyoomba. Kwa maana mji wote wa watu wangu wanakujua ya kwamba wewe ni mwanamke mwenye tabia nzuri. 3:12 Rut 2:20; 4:1Ingawa ni kweli kwamba mimi ndiye jamaa aliye karibu, bado kuna mtu mwingine wa jamaa aliye karibu zaidi wa kukomboa kuliko mimi. 3:13 Kum 25:5; Rut 4:5, 6; Mt 22:24; Amu 8:19; Yer 4:2; Ebr 6:16; Hes 14:21; Hos 4:15Wewe kaa hapa usiku huu, kisha asubuhi kama akikubali kukomboa, vyema na akomboe. La sivyo kama hayuko tayari, hakika kama Bwana aishivyo nitafanya hivyo. Lala hapa mpaka asubuhi.”

3:14 Hes 18:27; Rum 14:16; 2Kor 8:21; Rum 12:17; 14:16; 2Kor 8:21; 1The 5:22; 1Pet 2:12Hivyo huyo mwanamke akalala miguuni pake mpaka asubuhi, akaondoka mapema pasipo mtu kuweza kumtambua mwenzake, maana Boazi alisema, “Isijulikane kabisa ya kuwa mwanamke alifika kwenye sakafu ya kupuria.”

3:15 Isa 3:22Pia akamwambia, “Leta shela yako uliyoivaa, uitandaze.” Naye alipoitandaza, akamimina vipimo sita vya shayiri, akamtwika. Kisha Ruthu akarudi zake mjini.

Basi Ruthu alipofika kwa mama mkwe wake Naomi, akamuuliza, “Je, binti yangu, ilikuwaje huko?”

Ndipo akamwelezea kila kitu Boazi alichomfanyia. Akaendelea kusema, “Amenipa shayiri vipimo sita3:17 Vipimo sita vya shayiri ni sawa na kilo 15. akisema, ‘Usiende kwa mama mkwe wako mikono mitupu.’ ”

3:18 Za 37:3-5Kisha Naomi akasema, “Subiri binti yangu, mpaka utakapojua kwamba hili jambo limekwendaje. Kwa sababu mtu huyu hatatulia mpaka akamilishe jambo hili leo.”

Read More of Ruthu 3

Ruthu 4:1-22

Boazi Amwoa Ruthu

4:1 Mwa 18:1; 23:10; Rut 2:20; 3:12Boazi akakwea mpaka kwenye lango la mji, akaketi pale. Yule mtu wa jamaa aliyekuwa wa karibu wa kukomboa, ambaye Boazi alimtaja, akaja. Boazi akasema, “Njoo hapa, rafiki yangu. Karibu uketi.” Naye akakaribia, akaketi.

4:2 Kut 3:16; 18:21, 22; Kum 16:18; 17:9; 29:10; 25:7; 1Fal 21:8; Za 82:2; Mit 31:21, 23Boazi akatwaa watu kumi miongoni mwa wazee wa mji, akawaambia, “Ketini hapa.” Nao wakaketi. 4:3 Law 25:25; Rut 1:2Kisha akamwambia yule jamaa wa karibu wa kukomboa, “Naomi, aliyerudi hapa kutoka nchi ya Moabu, anauza sehemu ya ardhi iliyokuwa mali ya ndugu yetu Elimeleki. 4:4 Law 25:25; Rum 12:17; 2Kor 8:21; Flp 4:8; Mwa 23:18; Yer 32:7-8Nami niliwaza nikujulishe wewe na kukuambia uinunue mbele ya hawa waliopo hapa, na mbele ya wazee wa watu wangu. Kama wewe utaikomboa, haya fanya hivyo. Lakini kama hutaikomboa, uniambie, ili nijue. Kwa kuwa hakuna mtu mwingine mwenye haki ya kuikomboa ila wewe na baada yako ni mimi.”

Naye akasema, “Nitaikomboa mimi.”

4:5 Rut 1:22; 3:13; Mwa 38:8; Kum 25:5-6; Mt 22:24Ndipo Boazi akasema “Siku utakaponunua hiyo ardhi kutoka kwa Naomi na Ruthu, Mmoabu, itakubidi kumchukua pia huyo mjane, ili kudumisha jina la marehemu pamoja na mali yake.”

4:6 Law 25:25; Rut 3:13; Kum 25:7Aliposikia hili, yule jamaa wa karibu wa kukomboa akasema, “Basi mimi sitaweza kuikomboa, kwa sababu inaonekana nitauhatarisha urithi wangu. Wewe ikomboe mwenyewe. Mimi sitaweza.”

4:7 Law 25:24; Isa 8:1-2, 16-20; Kum 25:7-9(Basi katika siku za kale huko Israeli, ili kukamilisha tendo la kukomboa na kukabidhiana mali, mmoja huvua kiatu chake na kumpatia mwingine. Hii ilikuwa ni njia ya kuhalalisha mabadilishano katika Israeli.)

4:8 Kum 25:9Basi yule jamaa wa karibu wa kukomboa akamwambia Boazi, “Wewe inunue mwenyewe.” Naye huyo jamaa akavua kiatu chake.

4:9 Isa 8:2; Yer 32:10, 44Kisha Boazi akawatangazia wazee na watu wote waliokuwepo, “Leo ninyi ni mashahidi kwamba mimi nimenunua kutoka kwa Naomi yote yaliyokuwa mali ya Elimeleki, Kilioni na Maloni. 4:10 Rut 1:22; Kum 25:5-6; Yos 24:22Nimemchukua pia Ruthu, Mmoabu, mjane wa Maloni, awe mke wangu, ili kuendeleza jina la marehemu pamoja na mali zake, ili jina lake marehemu lisitoweke miongoni mwa jamaa yake, wala katika kumbukumbu za mji wake. Leo hivi ninyi ni mashahidi!”

4:11 Mwa 4:19; 23:10; 29:16; 35:16; Kum 25:9; Rut 1:19; Za 127:3Kisha wazee pamoja na watu wote waliokuwa langoni wakasema, “Sisi ni mashahidi. Bwana na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wanawake wawili ambao pamoja waliijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrathi na uwe mashuhuri katika Bethlehemu. 4:12 1Nya 2:4; Mt 1:3; 1Sam 2:20; Mwa 38:6, 24, 29Kupitia kwa watoto ambao Bwana atakupa kutokana na huyu mwanamwali, jamaa yako na ifanane na ya Peresi, ambaye Tamari alimzalia Yuda.”

Wazao Wa Boazi

4:13 Mwa 8:1; 29:31-32; 33:5; 30:6; Lk 1:57Basi Boazi akamwoa Ruthu, naye akawa mke wake. Alipoingia kwake, Bwana akamjalia Ruthu, naye akapata mimba, akamzaa mtoto wa kiume. 4:14 Lk 1:58; Rum 12:15; Mwa 24:27; Rut 2:20Wanawake wakamwambia Naomi: “Ahimidiwe Bwana, asiyekuacha bila kuwa na jamaa wa karibu wa kukomboa. Na awe mashuhuri katika Israeli yote! 4:15 Mwa 11:31; Isa 1:8; 2:5; Ay 1:2Atakurejeshea uhai wako na kukuangalia katika siku za uzee wako. Kwa maana mkweo ambaye anakupenda, na ambaye kwako ni bora zaidi ya watoto wa kiume saba, ndiye alimzaa.”

Basi Naomi akamchukua yule mtoto, akampakata na akawa mlezi wake. 4:17 1Sam 16:1, 13, 18; 17:12, 17, 58; 1Nya 2:12-15; Za 72:20Wanawake waliokuwa jirani zake wakasema, “Naomi ana mtoto wa kiume.” Wakamwita jina lake Obedi. Yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.

4:18 Mwa 38:29; Hes 26:21Hivi ndivyo vizazi vya Peresi:

Peresi alimzaa Hesroni,

4:19 Kut 6:23Hesroni akamzaa Ramu,

Ramu akamzaa Aminadabu,

4:20 Hes 1:7; 7:12Aminadabu akamzaa Nashoni,

Nashoni akamzaa Salmoni,

4:21 Rut 1:2; Mt 1:21Salmoni akamzaa Boazi,

Boazi akamzaa Obedi,

Obedi akamzaa Yese,

na Yese akamzaa Daudi.

Read More of Ruthu 4