Ruthu 1:1-22, Ruthu 2:1-23 NEN

Ruthu 1:1-22

Naomi Na Ruthu

1:1 Amu 2:16-18; Mwa 12:10; 35:19; 36:35; 47:4; 2Fal 6:25; Hag 1:11; Za 105:16; Kum 28:38; 1Fal 18:2; Mik 5:2Wakati Waamuzi walipotawala Israeli, kulikuwa na njaa katika nchi. Mtu mmoja kutoka nchi ya Bethlehemu ya Yuda, pamoja na mke wake na wanawe wawili, akaenda kuishi katika nchi ya Moabu. 1:2 Rut 2:1; 4:3; Amu 3:30; 1Sam 16:18; Mwa 35:16-19Mtu huyu aliitwa Elimeleki, mkewe aliitwa Naomi, na hao wanawe wawili waliitwa Maloni na Kilioni. Walikuwa Waefrathi kutoka Bethlehemu ya Yuda. Wakaenda katika nchi ya Moabu, wakaishi huko.

Elimeleki mumewe Naomi akafa, hivyo Naomi akabaki na wanawe wawili. 1:4 1Fal 11:1; Mt 1:5; Rut 4:13; Ezr 9:2; Neh 13:23Nao wakaoa wanawake Wamoabu, jina la mmoja aliitwa Orpa, na wa pili aliitwa Ruthu. Baada ya kama miaka kumi, 1:5 Rut 2:11Maloni na Kilioni pia wakafa. Basi Naomi akabaki hana mume wala wanawe wawili.

1:6 Mwa 11:31; 36:35; 38:16; 50:24; Kut 4:31; Yer 29:10; Sef 2:7; Za 80:14; Zek 10:3; Lk 1:68; 7:16; Mwa 28:20; 48:15; Mit 30:8; Isa 55:10; Mt 6:11; Za 132:15Aliposikia akiwa huko Moabu kwamba Bwana amewasaidia watu wake kwa kuwapa chakula, Naomi na wakweze wakajiandaa kurudi nyumbani. Yeye na wakweze wawili wakaondoka pale walipokuwa wakiishi na kushika njia kurudi nchi ya Yuda.

1:8 Mwa 38:11; 19:19; Yos 24:25; 2Tim 1:16Ndipo Naomi akawaambia wale wakwe zake wawili, “Rudini, kila mmoja wenu nyumbani kwa mama yake. Bwana na awatendee fadhili kama mlivyowatendea hao waliofariki, na pia mimi. 1:9 Rut 3:1; Mwa 27:27, 38; 29:11; Hes 25:6Bwana na amjalie kila mmoja wenu maisha mema nyumbani kwa mume mwingine.”

Kisha akawabusu, nao wakalia kwa sauti kubwa, wakamwambia, “Tutarudi pamoja na wewe nyumbani kwa watu wako.”

1:11 Mwa 38:11; Kum 25:5Lakini Naomi akasema, “Rudini nyumbani, binti zangu. Kwa nini mnifuate? Je, mimi nitaweza tena kuwa na wana wengine ambao wataweza kuwaoa ninyi? Rudini nyumbani, binti zangu; mimi ni mzee kiasi kwamba siwezi kumpata mume mwingine. Hata kama ningefikiria kuwa bado kuna tumaini kwangu, hata kama ningekuwa na mume usiku huu na kuwazaa wana, 1:13 Mwa 38:11; Kut 1:14; 15:23; 1Sam 30:6; Ay 19:21; Za 32:4; 38:2; Amu 2:15; 4:5je, mngesubiri mpaka wakue? Mngebakia bila kuolewa mkiwasubiri? La, hasha, binti zangu. Nimepata uchungu kuliko ninyi, kwa sababu mkono wa Bwana umekuwa kinyume nami!”

1:14 Rut 2:11; 3:1; Mik 7:6; Mit 17:17; 18:24; Yn 6:66-69; Ebr 10:39; Mwa 31:28; Kum 10:20Kisha wakalia tena kwa sauti. Orpa akambusu mama mkwe wake, akaenda zake, lakini Ruthu akaambatana naye.

1:15 Kum 25:7; Yos 24:14; Amu 11:24Naomi akamwambia, “Tazama, mwenzako anarejea kwa watu wake na kwa miungu yake. Rudi pamoja naye.”

1:16 2Fal 2:2; Yos 24:15; Mwa 24:58; Za 45:10; Rut 2:11-12Lakini Ruthu akajibu, “Usinisihi nikuache au niache kukufuata. Utakakokwenda nami nitakwenda, na wewe utakapoishi nitaishi. Watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu. 1:17 1Sam 3:17; 14:44; 20:13; 25:22; 1Fal 2:23; 19:2; 20:10; 2Sam 3:9; 19:13; 2Fal 6:31; 15:21Pale utakapofia nami nitafia hapo, na papo hapo nitazikwa. Bwana na aniadhibu vikali, kama kitu kingine chochote kitanitenga nawe isipokuwa kifo.” 1:18 Mdo 21:14Naomi alipotambua kwamba Ruthu amenuia kufuatana naye, hakuendelea kumsihi tena.

1:19 Amu 17:7; Isa 23:7; Mt 21:10; Mao 2:15Kwa hiyo hao wanawake wawili wakaondoka, wakafika Bethlehemu. Walipofika Bethlehemu, mji mzima ulitaharuki, wanawake wakashangaa, wakasema, “Huyu aweza kuwa ni Naomi?”

1:20 Mwa 15:1; 17:1; Za 91:1; Kut 6:3; Ay 6:4Akawaambia, “Msiniite tena Naomi,1:20 Naomi maana yake Wa Kupendeza, Wa Kufurahisha. niiteni Mara,1:20 Mara maana yake Chungu. kwa sababu Mwenyezi1:20 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. amenitendea mambo machungu sana. 1:21 Ay 1:21; 30:11; Za 88:7; Isa 53:4Mimi niliondoka hali nimejaa, lakini Bwana amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi? Bwana amenitendea mambo machungu; Mwenyezi ameniletea msiba.”

1:22 Rut 2:2-6, 21; 4:5, 10; Kut 9:31; Mwa 11:31; Law 19:9; 2Sam 21:9Kwa hiyo Naomi alirudi pamoja na Ruthu Mmoabu mkwe wake, nao wakafika Bethlehemu mwanzoni mwa kuvuna shayiri.

Read More of Ruthu 1

Ruthu 2:1-23

Ruthu Akutana Na Boazi

2:1 Rut 2:3; 4:21; Mit 7:4; 1Sam 9:1; 1Fal 11:28; 1Nya 2:12; Mt 1:5; Lk 3:32Basi Naomi alikuwa na jamaa wa upande wa mume wake, kutoka ukoo wa Elimeleki, mtu maarufu ambaye aliitwa Boazi.

2:2 Rut 1:22; Law 19:9; 23:22; Mwa 6:8; 18:3; Kum 24:19Ruthu, Mmoabu, akamwambia Naomi, “Nitakwenda mashambani nikaokote mabaki ya nafaka nyuma ya yule nitakayepata kibali machoni pake.”

Naomi akamwambia, “Nenda, binti yangu.” 2:3 2Fal 4:18; Yer 9:22; Amo 9:13Basi akaenda, akaokota mabaki ya nafaka mashambani nyuma ya wavunaji. Ikatokea kwamba alijikuta anafanya kazi kwenye shamba lililokuwa mali ya Boazi, ambaye alitoka kwenye ukoo wa Elimeleki.

2:4 Lk 1:28; Mwa 28:3; 2The 3:16; 2Tim 4:22; Kol 4:6; Hes 6:24; Amu 6:12; Za 129:7-8Papo hapo Boazi akarudi kutoka Bethlehemu, akawasalimu wavunaji, akasema, “Bwana awe nanyi!”

Nao wakamjibu, “Bwana akubariki.”

Boazi akamuuliza msimamizi wa wavunaji, “Je, yule mwanamwali ni wa nani?”

2:6 Rut 1:22Msimamizi akamjibu, “Ni yule Mmoabu aliyerudi kutoka nchi ya Moabu pamoja na Naomi. 2:7 Mwa 37:7; Law 19:9; 2Sam 4:5Yeye aliomba, ‘Tafadhali niruhusu niokote na kukusanya miongoni mwa miganda nyuma ya wavunaji.’ Naye ameshinda shambani tangu asubuhi pasipo kupumzika, isipokuwa kwa muda mfupi kivulini.”

Kisha Boazi akamwambia Ruthu, “Binti yangu, nisikilize. Usiende kuokota mabaki ya mavuno katika shamba lingine, na usiondoke hapa. Kaa hapa na hawa watumishi wangu wa kike. Angalia shamba wanaume wanamovuna, ufuate nyuma yao. Nimewaamuru wanaume hawa wasikuguse. Wakati wowote ukiona kiu, nenda kwenye mitungi ukanywe maji waliyoyateka wanaume hawa.”

2:10 Mwa 19:1; 31:15; 1Sam 25:23; 20:41; Kum 15:3Kwa ajili ya hili, akasujudu mpaka nchi, akamwambia, “Jinsi gani nimepata kibali machoni pako, hata ukanijali mimi mgeni?”

2:11 Rut 1:5, 14, 16-17; Isa 55:5; Mit 31:31; Rut 1:14; Lk 5:11, 28; 14:33; 18:29, 30Boazi akamjibu, “Nimeambiwa yote uliyomtendea mama mkwe wako tangu mume wako alipofariki, na jinsi ulivyomwacha baba yako na mama yako na nchi yako ulimozaliwa, ukaja kuishi na watu ambao hukuwafahamu awali. 2:12 1Sam 24:19; 26:23-25; Za 17:8; 18:20; 36:7; 57:1; 61:4; 63:7; 91:4; 71:1; Mit 25:22; Yer 31:16; Yos 24:15Bwana na akulipe kwa yale uliyoyatenda. Ubarikiwe kwa wingi na Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye umekimbilia mabawani mwake.”

2:13 Mwa 18:3; Flp 2:3; 1Sam 25:41Kisha Ruthu akasema, “Naomba niendelee kupata kibali machoni pako, bwana wangu. Kwa maana umenifariji na umezungumza kwa ukarimu na mjakazi wako, hata ingawa mimi si bora kama mmoja wa watumishi wako wa kike.”

2:14 Mwa 3:19; Law 23:14Wakati wa chakula, Boazi akamwambia Ruthu, “Karibia hapa. Kula mkate na uchovye ndani ya siki.”

Alipoketi pamoja na wavunaji, akampa nafaka zilizookwa. Akala kiasi alichotaka na kusaza. 2:15 Mwa 37:7; Law 19:9Alipoinuka ili kuokota mabaki ya nafaka, Boazi akawaagiza watu wake, “Hata kama atakusanya kati ya miganda, msimzuie. 2:16 Mwa 37:10Badala yake, toeni masuke katika miganda, mwachieni ayaokote, na msimkemee.”

2:17 Amu 6:11; Law 19:36Basi Ruthu akaokota masazo shambani hata jioni. Akatwanga ile shayiri aliyokusanya, ikajaa efa moja.2:17 Efa moja ni sawa na kilo 22. Akaibeba na kuelekea mjini, naye mama mkwe wake akaona jinsi alivyoweza kuokota nafaka nyingi. Pia Ruthu akachukua kile alichobakiza baada ya kula na kushiba, akampa.

Basi mkwewe akamuuliza, “Je, umeokota wapi leo? Umefanya kazi wapi? Abarikiwe mtu yule aliyekujali.”

Ndipo Ruthu akamwambia mama mkwe wake juu ya yule ambaye yeye alikuwa amefanyia kazi katika shamba lake. Akasema, “Yule mtu niliyefanyia kazi kwake leo, anaitwa Boazi.”

2:20 Amu 17:2; 1Sam 23:21; Mwa 11:31; 19:19; 2Sam 2:5; Ay 29:13; 2Tim 1:16; Mit 17:17; Law 25:25; Rut 3:9; 4:1, 14Naye Naomi akamwambia mkwewe, “Bwana ambariki! Hakuacha kuonyesha fadhili zake kwa walio hai na kwa waliokufa.” Pia akamwambia, “Huyo mtu ni mmoja wa jamaa yetu wa karibu anayestahili kutukomboa.”

2:21 Rut 1:22Kisha Ruthu, Mmoabu, akasema, “Hata aliniambia, ‘Kaa pamoja na watumishi wangu mpaka watakapomaliza kuvuna nafaka yangu yote.’ ”

Kisha Naomi akamwambia Ruthu mkwewe, “Binti yangu, itakuwa vyema wewe ufuatane na wasichana wake, kwa sababu katika shamba la mtu mwingine wanaweza kukudhuru.”

2:23 Kut 9:31; Mwa 30:14; 1Sam 6:13; Kum 16:9Kwa hivyo Ruthu akafuatana na watumishi wa kike wa Boazi, akaokota mpaka mwisho wa mavuno ya shayiri na ya ngano. Naye aliishi na mama mkwe wake.

Read More of Ruthu 2