Warumi 6:1-14 NEN

Warumi 6:1-14

Kufa Na Kufufuka Pamoja Na Kristo

6:1 Rum 3:5, 6Tuseme nini basi? Je, tuendelee kutenda dhambi ili neema ipate kuongezeka? 6:2 Kol 3:5, 8La hasha! Sisi tulioifia dhambi, tutawezaje kuendelea kuishi tena katika dhambi? 6:3 Mt 28:19Au hamjui ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? 6:4 Mdo 2:24; Kol 2:12; 2Kor 5:17; Gal 6:15Kwa hiyo tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti, ili kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka kwa wafu kwa utukufu wa Baba, vivyo hivyo sisi nasi pia tupate kuenenda katika upya wa uzima.

6:5 Efe 2:6; 2Tim 2:11Kwa maana ikiwa tumeungana naye katika mauti yake, bila shaka tutaungana naye katika ufufuo wake. 6:6 Gal 5:24; Kol 3:9; 2Kor 4:10; Gal 2:20; Rum 7:24Kwa maana twajua kwamba utu wetu wa kale ulisulubiwa pamoja naye ili ule mwili wa dhambi upate kuangamizwa, nasi tusiendelee kuwa tena watumwa wa dhambi. 6:7 1Pet 4:1; Rum 6:18Kwa maana mtu yeyote aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.

6:8 Rum 6:5; 2Tim 2:11Basi ikiwa tulikufa pamoja na Kristo, tunaamini kwamba pia tutaishi pamoja naye. 6:9 Mdo 2:24; Ufu 1:18Kwa maana tunajua kwamba Kristo, kwa sababu alifufuliwa kutoka kwa wafu, hawezi kufa tena; mauti haina tena mamlaka juu yake. 6:10 Rum 6:2; Ebr 7:27; 9:26-28; Gal 2:19; 1Pet 3:18Kifo alichokufa, aliifia dhambi mara moja tu, lakini uzima alio nao anamwishia Mungu.

6:11 Rum 6:2; 2Kor 5:15; 1Pet 2:24Vivyo hivyo, jihesabuni wafu katika dhambi lakini mlio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. 6:12 Rum 6:16; Mwa 4:7; Za 19:13; 119:133Kwa hiyo, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na kufa, ili kuwafanya mzitii tamaa mbaya. 6:13 Rum 7:5; 2Kor 5:156:13 1Pet 2:24Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu kwake kama vyombo vya haki. 6:14 Rum 2:12; Gal 5:18; Rum 3:24Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria, bali chini ya neema.

Read More of Warumi 6