Warumi 4:16-25, Warumi 5:1-11 NEN

Warumi 4:16-25

4:16 Rum 3:24; 15:8Kwa hiyo, ahadi huja kwa njia ya imani, ili iwe ni kwa neema, na itolewe kwa wazao wa Abrahamu, si kwa wale walio wa sheria peke yao, bali pia kwa wale walio wa imani ya Abrahamu. Yeye ndiye baba yetu sisi sote. 4:17 Mwa 17:5; Yn 5:21; Isa 48:13; 1Kor 1:28Kama ilivyoandikwa: “Nimekufanya wewe kuwa baba wa mataifa mengi.” Yeye ni baba yetu mbele za Mungu, ambaye yeye alimwamini, yule Mungu anaye fufua waliokufa, na kuvitaja vile vitu ambavyo haviko kana kwamba vimekwisha kuwako.

Mfano Wa Imani Ya Abrahamu

4:18 Mwa 15:5Akitarajia yasiyoweza kutarajiwa, Abrahamu akaamini, akawa baba wa mataifa mengi, kama alivyoahidiwa kwamba, “Uzao wako utakuwa mwingi mno.” 4:19 Ebr 11:11, 12; Mwa 17:17; 18:11; Mt 9:8Abrahamu hakuwa dhaifu katika imani hata alipofikiri juu ya mwili wake, ambao ulikuwa kama uliokufa, kwani umri wake ulikuwa unakaribia miaka mia moja, au alipofikiri juu ya ufu wa tumbo la Sara. 4:20 1Sam 30:6; Mt 9:8; Rum 4:15; Gal 3:19Lakini Abrahamu hakusitasita kwa kutokuamini ahadi ya Mungu, bali alitiwa nguvu katika imani yake na kumpa Mungu utukufu, 4:21 Mwa 18:14; Ebr 11:9akiwa na hakika kabisa kwamba Mungu alikuwa na uwezo wa kutimiza lile aliloahidi. 4:22 Rum 1:17; 9:30; Gal 2:16; 3:22Hii ndio sababu, “ilihesabiwa kwake kuwa haki.” 4:23 Rum 3:9; Mdo 15; 4; 1Kor 10:6, 11Maneno haya “ilihesabiwa kwake kuwa haki,” hayakuandikwa kwa ajili yake peke yake, 4:24 Hab 2:2; 1Kor 10:11; Rum 10:9; 1Pet 1:21; Mdo 2:24bali kwa ajili yetu sisi pia ambao Mungu atatupa haki, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu kutoka kwa wafu. 4:25 Isa 53:5, 6; 2Kor 5:21Alitolewa afe kwa ajili ya dhambi zetu, naye alifufuliwa kutoka mauti ili tuhesabiwe haki.

Read More of Warumi 4

Warumi 5:1-11

Matokeo Ya Kuhesabiwa Haki

5:1 Rum 3:28; Isa 32:17; Yn 16:33Kwa hiyo, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa imani, tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, 5:2 Efe 2:18; 3:12; 1Kor 15:1; Ebr 3:5; Mt 5:12ambaye kwa kupitia kwake tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo ndani yake sasa tunasimama, nasi twafurahia katika tumaini letu la kushiriki utukufu wa Mungu. 5:3 Ebr 10:36; Yak 1:2-3; Ebr 3:6; 1Yn 3:2-3; Mdo 10:43Si hivyo tu, bali twafurahi pia katika mateso, kwa sababu tunajua kuwa mateso huleta saburi, 5:4 Yak 1:12nayo saburi huleta uthabiti wa moyo, na uthabiti wa moyo huleta tumaini, 5:5 Flp 1:20; Ebr 3:6; Yn 3:2, 3; Rum 5:8; Yn 3:16; Rum 8:39; Tit 3:3, 6wala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo lake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ametupatia.

5:6 Mk 1:15; Efe 1:10; Rum 4:25Kwa maana hata tulipokuwa dhaifu, wakati ulipowadia, Kristo alikufa kwa ajili yetu sisi wenye dhambi. Hakika, ni vigumu mtu yeyote kufa kwa ajili ya mwenye haki, ingawa inawezekana mtu akathubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema. 5:8 Yn 3:16; 1Yn 4:10Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.

5:9 Rum 3:25; Kum 1:18Basi, kwa kuwa sasa tumehesabiwa haki kwa damu yake, si zaidi sana tutaokolewa kutoka ghadhabu ya Mungu kupitia kwake! 5:10 Rum 11:28; 1Kor 1:21; 2Kor 5:18, 19; Kol 1:20, 22; Ebr 7:25Kwa kuwa kama tulipokuwa adui wa Mungu tulipatanishwa naye kwa njia ya kifo cha Mwanawe, si zaidi sana tukiisha kupatanishwa, tutaokolewa kwa uzima wake. 5:11 Rum 5:10; 2:17; 3:29, 30; Gal 4:9Lakini zaidi ya hayo, pia tunafurahi katika Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kupitia kwake tumepata upatanisho.

Read More of Warumi 5