Warumi 4:1-15 NEN

Warumi 4:1-15

Abrahamu Alihesabiwa Haki Kwa Imani

4:1 Rum 8:31; Lk 3:8Tuseme nini basi, kuhusu Abrahamu baba yetu kwa jinsi ya mwili: yeye alipataje kujua jambo hili? 4:2 1Kor 13:1; Mdo 13:20; 27:28Kwa maana ikiwa Abrahamu alihesabiwa haki kwa matendo, basi, anacho kitu cha kujivunia, lakini si mbele za Mungu. 4:3 Mwa 15:6; Yak 2:23Kwa maana Maandiko yasemaje? “Abrahamu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki.”

4:4 Rum 11:6Basi mtu afanyapo kazi, mshahara wake hauhesabiwi kwake kuwa ni zawadi, bali ni haki yake anayostahili. 4:5 Yos 24:2Lakini kwa mtu ambaye hafanyi kazi na anamtumaini Mungu, yeye ambaye huwahesabia waovu haki, imani yake inahesabiwa kuwa haki. 4:6 Za 32:1, 2Daudi pia alisema vivyo hivyo aliponena juu ya baraka za mtu ambaye Mungu humhesabia haki pasipo matendo:

4:7 Za 32:1, 2“Wamebarikiwa wale

ambao wamesamehewa makosa yao,

ambao dhambi zao zimefunikwa.

4:8 Za 103:12; 2Kor 5:19Heri mtu yule

Bwana hamhesabii dhambi zake.”

Haki Kabla Ya Tohara

4:9 Rum 3:30Je, huku kubarikiwa ni kwa wale waliotahiriwa peke yao, au pia na kwa wale wasiotahiriwa? Tunasema, “Imani ya Abrahamu ilihesabiwa kwake kuwa haki.” 4:10 Rum 8:7Je, ni lini basi ilipohesabiwa kwake kuwa haki? Je, ilikuwa kabla au baada ya kutahiriwa kwake? Haikuwa baada, ila kabla hajatahiriwa. 4:11 Mwa 17:10, 11; Lk 3:8; 19:9; Rum 3:22Alipewa ishara ya tohara kuwa muhuri wa haki aliyokuwa nayo kwa imani hata alipokuwa bado hajatahiriwa. Kusudi lilikuwa kumfanya baba wa wote wale waaminio pasipo kutahiriwa na ambao wamehesabiwa haki. 4:12 Mwa 2:17; 3:19; Rum 6:23Vivyo hivyo awe baba wa wale waliotahiriwa ambao si kwamba wametahiriwa tu, bali pia wanafuata mfano wa imani ambayo Baba yetu Abrahamu alikuwa nayo kabla ya kutahiriwa.

Ahadi Ya Mungu Hufahamika Kwa Imani

4:13 Mdo 13:32; Gal 3:16, 29; Mwa 17:4-6Kwa maana ile ahadi kwamba angeurithi ulimwengu haikuja kwa Abrahamu au kwa wazao wake kwa njia ya sheria bali kwa njia ya haki ipatikanayo kwa imani. 4:14 Gal 3:18Kwa maana ikiwa wale waishio kwa sheria ndio warithi, imani haina thamani na ahadi haifai kitu, 4:15 2Kor 3:7kwa sababu sheria huleta ghadhabu. Mahali ambapo hakuna sheria hakuna makosa.

Read More of Warumi 4