Warumi 3:9-31 NEN

Warumi 3:9-31

Wote Wametenda Dhambi

3:9 1Fal 8:46; Gal 3:22Tusemeje basi? Je, sisi ni bora kuwaliko wao? La hasha! Kwa maana tumekwisha kuhakikisha kwa vyovyote kwamba Wayahudi na watu wa Mataifa wote wako chini ya nguvu ya dhambi. 3:10 Za 14:1, 3; 53:1Kama ilivyoandikwa:

“Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja.

Hakuna hata mmoja mwenye ufahamu,

hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu.

3:12 Za 53:1-3; Mhu 7:20Wote wamepotoka,

wote wameoza pamoja;

hakuna atendaye mema,

naam, hakuna hata mmoja.”

3:13 Za 5:9; 140:3“Makoo yao ni makaburi wazi;

kwa ndimi zao wao hufanya udanganyifu.”

“Sumu ya nyoka iko midomoni mwao.”

3:14 Za 10:7“Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.”

3:15 Isa 59:7, 8; Mit 1:16“Miguu yao ina haraka kumwaga damu;

maangamizi na taabu viko katika njia zao,

3:17 Isa 59:7, 9wala njia ya amani hawaijui.”

3:18 Za 36:1“Hakuna hofu ya Mungu machoni pao.”

3:19 Yn 10:34; Rum 2:12Basi tunajua ya kwamba chochote sheria inachosema, inawaambia wale walio chini ya sheria ili kila kinywa kinyamazishwe na ulimwengu wote uwajibike kwa Mungu. 3:20 Mdo 13:39; Gal 2:16; Rum 4:15; 7:7Kwa hiyo hakuna binadamu hata mmoja atakayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa matendo ya sheria, kwa maana sheria hutufanya tuitambue dhambi.

Haki Kwa Njia Ya Imani

3:21 Isa 46:13; Rum 9:30; Mdo 10:43; Rum 1:2Lakini sasa, haki itokayo kwa Mungu imedhihirishwa pasipo sheria, ambayo Sheria na Manabii wanaishuhudia. 3:22 Rum 9:30; Gal 3:28; Kol 3:11Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa Yesu Kristo kwa wote wamwaminio. Kwa maana hapo hakuna tofauti, 3:23 Rum 9:19; 5:2; 3:9; Gal 3:22kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, 3:24 2Kor 12:9; Tit 2:11; Za 130:7; Gal 4:5wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu. 3:25 Za 65:3; Ebr 9:28; 1Pet 1:19; Ufu 1:5; Mdo 14:16; 17:30Yeye ambaye Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki yake, kwa sababu kwa ustahimili wake aliziachilia zile dhambi zilizotangulia kufanywa. Alifanya hivyo ili kuonyesha haki yake wakati huu, ili yeye awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yule anayemwamini Yesu.

Umuhimu Wa Kuwa Na Imani

3:27 1Kor 1:29-31; Efe 2:9Basi, kujivuna kuko wapi? Kumewekwa mbali. Kwa sheria gani? Je, ni kwa ile ya matendo? La hasha, bali kwa ile sheria ya imani. 3:28 Gal 3:11; Yn 2:19Kwa maana twaona kwamba mwanadamu huhesabiwa haki kwa njia ya imani wala si kwa matendo ya sheria. 3:29 Mdo 10:34, 35Je, Mungu ni Mungu wa Wayahudi peke yao? Je, yeye si Mungu wa watu wa Mataifa pia? Naam, yeye ni Mungu wa watu wa Mataifa pia. 3:30 Rum 4:11, 12; Gal 3:8Basi kwa kuwa tuna Mungu mmoja tu, atawahesabia haki wale waliotahiriwa kwa imani na wale wasiotahiriwa kwa imani iyo hiyo. Je, basi ni kwamba tunaibatilisha sheria kwa imani hii? La, hasha! Badala yake tunaithibitisha sheria.

Read More of Warumi 3