Warumi 2:17-29, Warumi 3:1-8 NEN

Warumi 2:17-29

Wayahudi Na Sheria

2:17 Yer 8:8; Yn 5:45Tazama, wewe ukiwa unaitwa Myahudi na kuitegemea sheria na kujisifia uhusiano wako na Mungu, 2:18 Flp 1:10; Kum 4:8; Za 147:19, 20; Flp 1:10kama unajua mapenzi ya Mungu na kukubali lililo bora kwa sababu umefundishwa na hiyo sheria, 2:19 Mt 15:14; Lk 18:9kama unatambua kuwa wewe ni kiongozi wa vipofu, na mwanga kwa wale walio gizani, 2:20 2Tim 1:13; 3:5mkufunzi wa wajinga na mwalimu wa watoto wachanga, kwa kuwa una maarifa ya kweli katika hiyo sheria, 2:21 Mt 23:3, 4; Za 50:16basi wewe, uwafundishaye wengine, mbona hujifunzi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, wewe mwenyewe waiba? 2:22 Mdo 19:32; Mal 3:8Wewe usemaye mtu asizini, wewe mwenyewe wazini? Wewe uchukiaye miungu ya sanamu, wafanya jambo la kumchukiza katika mahekalu? Wewe ujivuniaye sheria, wamwaibisha Mungu kwa kuvunja sheria? 2:24 Isa 52:5; 2Pet 2:2Kama ilivyoandikwa, “Kwa ajili yenu ninyi, Jina la Mungu linatukanwa miongoni mwa watu wa Mataifa.”

2:25 Gal 5:3; Yer 4:4; 9:25, 26Kutahiriwa kuna thamani ikiwa unatii sheria, lakini kama unavunja sheria, kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa. 2:26 Rum 8:4; 1Kor 7:19Hivyo, ikiwa wale wasiotahiriwa wanatimiza mambo ambayo sheria inataka, je, kutokutahiriwa kwao hakutahesabiwa kuwa sawa na kutahiriwa? 2:27 Mt 12:41, 42Ndipo wale ambao hawakutahiriwa kimwili lakini wanaitii sheria watawahukumu ninyi, ambao ingawa mmetahiriwa na kuijua sana sheria ya Mungu iliyoandikwa, lakini mwaivunja.

2:28 Mt 3:9; Yn 8:39Kwa maana mtu si Myahudi kwa vile alivyo kwa nje, wala tohara ya kweli si kitu cha nje au cha kimwili. 2:29 Flp 3:3; Kol 2:11; Rum 7:6; 2Kor 3:6; Yn 12:43; Gal 1:10Lakini mtu ni Myahudi alivyo ndani, nayo tohara ya kweli ni jambo la moyoni, ni la Roho, wala si la sheria iliyoandikwa. Mtu wa namna hiyo hapokei sifa kutoka kwa wanadamu bali kwa Mungu.

Read More of Warumi 2

Warumi 3:1-8

Uaminifu Wa Mungu

Basi kuna faida gani kuwa Myahudi? Au kuna thamani gani katika tohara? 3:2 Za 147:19; Mdo 7:38Kuna faida kubwa kwa kila namna! Kwanza kabisa, Wayahudi wamekabidhiwa lile Neno halisi la Mungu. 3:3 Rum 10:16; Ebr 4:2; 2Tim 2:13Ingekuwaje kama wengine hawakuwa na imani? Je, kutokuamini kwao kungebatilisha uaminifu wa Mungu? 3:4 Yn 3:33; Za 116:11La hasha! Mungu na aonekane mwenye haki, na kila mwanadamu kuwa mwongo, kama ilivyoandikwa:

“Ili uthibitike kuwa wa kweli unaponena,

na ukashinde utoapo hukumu.”

3:5 Rum 6:19; Gal 3:15Ikiwa uovu wetu unathibitisha haki ya Mungu waziwazi, tuseme nini basi? Je, Mungu kuileta ghadhabu yake juu yetu ni kwamba yeye si mwenye haki? (Nanena kibinadamu.) 3:6 Mwa 18:25; Rum 2:16La hasha! Kama hivyo ndivyo ilivyo, Mungu angehukumuje ulimwengu? 3:7 Rum 3:4; 9:19Mtu aweza kuuliza, “Kama uongo wangu unasaidia kuonyesha kweli ya Mungu na kuzidisha utukufu wake, kwa nini basi mimi nahukumiwa kuwa mwenye dhambi?” 3:8 Rum 6:1; Mdo 5:20; 6:1; 15Nasi kwa nini tusiseme, kama wengine wanavyotusingizia kuwa tunasema, “Tutende maovu ili mema yapate kuja?” Wao wanastahili hukumu yao.

Read More of Warumi 3