Warumi 2:1-16 NEN

Warumi 2:1-16

Hukumu Ya Mungu

2:1 Rum 1:20; 2Sam 12:5-7; Mt 7:12Kwa hiyo huna udhuru wowote, wewe utoaye hukumu kwa mwingine, kwa maana katika jambo lolote unalowahukumu wengine, unajihukumu wewe mwenyewe kwa sababu wewe unayehukumu unafanya mambo hayo hayo. 2:2 2Sam 12:5-7; Mt 7:12Basi tunajua kwamba hukumu ya Mungu dhidi ya wale wafanyao mambo kama hayo ni ya kweli. Hivyo wewe mwanadamu, utoapo hukumu juu yao na bado unafanya mambo yale yale, unadhani utaepuka hukumu ya Mungu? 2:4 Efe 3:8, 16; Kol 2:2; Rum 11:22; 3:25; Kut 34:6Au waudharau wingi wa wema, ustahimili na uvumilivu wake, bila kujua kuwa wema wa Mungu wakuelekeza kwenye toba?

2:5 1Pet 3:20; 2Pet 3:9Lakini kwa sababu ya ukaidi wenu na mioyo yenu isiyotaka kutubu, mnajiwekea akiba ya ghadhabu dhidi yenu wenyewe kwa siku ile ya ghadhabu ya Mungu, wakati hukumu yake ya haki itakapodhihirishwa. 2:6 Za 62:12; Mt 16:27Kwa maana Mungu atamlipa kila mtu sawasawa na matendo yake. 2:7 1Kor 15:53, 54; 2Tim 1:10Wale ambao kwa kuvumilia katika kutenda mema hutafuta utukufu, heshima na maisha yasiyoharibika, Mungu atawapa uzima wa milele. 2:8 2The 2:12Lakini kwa wale watafutao mambo yao wenyewe na wale wanaokataa kweli na kuzifuata njia mbaya, kutakuwa na ghadhabu na hasira ya Mungu. 2:9 1Pet 4:17; Rum 1:16; 3:9; Za 32:10Kutakuwa na taabu na dhiki kwa kila mmoja atendaye maovu, Myahudi kwanza na mtu wa Mataifa pia, 2:10 Rum 1:16; 2:9bali utukufu, heshima na amani kwa ajili ya kila mmoja atendaye mema, kwa Myahudi kwanza, kisha kwa mtu wa Mataifa. 2:11 Mdo 10:34; 1Pet 1:17Kwa maana Mungu hana upendeleo.

2:12 1Kor 9:20, 21; Gal 4:21Watu wote waliotenda dhambi pasipo sheria wataangamia pasipo sheria, nao wote wale waliotenda dhambi chini ya sheria watahukumiwa kwa sheria. 2:13 Yak 1:22, 23, 25Kwa maana si wale wanaoisikia sheria ambao ni wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale wanaoitii sheria ndio watakaohesabiwa haki. 2:14 Mdo 10:34(Naam, wakati wa watu wa Mataifa, ambao hawana sheria, wanapofanya kwa asili mambo yatakiwayo na sheria, wao ni sheria kwa nafsi zao wenyewe, hata ingawa hawana sheria. 2:15 Mhu 12:14; 1Kor 4:5; Mdo 10:42; Rum 16:25; 2Tim 2:8Wao wanaonyesha kwamba lile linalotakiwa na sheria limeandikwa kwenye mioyo yao, ambayo pia dhamiri zao zikiwashuhudia, nayo mawazo yao yenye kupingana yatawashtaki au kuwatetea.) 2:16 Mhu 12:14; 1Kor 4:5; Mdo 10:42; Rum 16:25; 2Tim 2:8Hili litatukia siku hiyo Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu kwa njia ya Yesu Kristo, kama isemavyo Injili yangu.

Read More of Warumi 2