Warumi 14:19-23, Warumi 15:1-13 NEN

Warumi 14:19-23

14:19 Za 34:14; 1Kor 7:15; Rum 15:2; Efe 4:12, 29Kwa hiyo na tufanye bidii kutafuta yale yaletayo amani na kujengana sisi kwa sisi. 14:20 Rum 14:15; Mt 15:11; Mdo 10:15; Tit 1:15Usiiharibu kazi ya Mungu kwa ajili ya chakula. Hakika vyakula vyote ni safi, lakini ni kosa kula kitu chochote kinachomsababisha ndugu yako ajikwae. 14:21 1Kor 8:13; Mt 15:29Ni afadhali kutokula nyama wala kunywa divai au kufanya jambo lingine lolote litakalomsababisha ndugu yako ajikwae.

14:22 1Yn 3:21; Mt 15:29Je, wewe unayo imani? Ile imani uliyo nayo, uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiye na sababu ya kujihukumu nafsi yake kwa ajili ya kile anachokifanya. Lakini kama mtu ana shaka kuhusu kile anachokula, amehukumiwa, kwa sababu hakula kwa imani. Kwa kuwa chochote kinachofanywa pasipo imani ni dhambi.

Read More of Warumi 14

Warumi 15:1-13

Usijipendeze Mwenyewe, Bali Wapendeze Wengine

15:1 Rum 14:1; 1The 5:14Sisi tulio na nguvu, hatuna budi kuchukuliana na kushindwa kwa wale walio dhaifu wala si kujipendeza nafsi zetu wenyewe. 15:2 1Kor 10:33Kila mmoja wetu inampasa kumpendeza jirani yake kwa mambo mema, ili kumjenga katika imani. 15:3 2Kor 8:9; Za 69:9Kwa maana hata Kristo hakujipendeza mwenyewe, bali kama ilivyoandikwa: “Matukano yao wale wanaokutukana wewe yalinipata mimi.” 15:4 Rum 4:23, 24; 1Kor 10:11; 9:9, 10; 10:11; 2Tim 3:16, 17Kwa maana kila kitu kilichoandikwa zamani, kiliandikwa kutufundisha, ili kwamba kwa saburi na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini.

15:5 2Kor 13:11; Efe 4:3Mungu atoaye saburi na faraja, awajalie ninyi roho ya umoja miongoni mwenu mnapomfuata Kristo Yesu, 15:6 Ufu 1; 6; Za 34:3; Mdo 4:24, 32ili kwa moyo mmoja mpate kumtukuza Mungu aliye Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Injili Sawa Kwa Wayahudi Na Kwa Watu Wa Mataifa

15:7 Rum 14:1; 5:2Karibishaneni ninyi kwa ninyi kama Kristo alivyowakaribisha ninyi ili kumletea Mungu utukufu. 15:8 Mt 15:24; Mdo 3:25, 26; 2Kor 1:20Kwa maana nawaambia kwamba, Kristo amekuwa mtumishi kwa wale waliotahiriwa ili kuonyesha kweli ya Mungu na kuthibitisha zile ahadi walizopewa baba zetu wa zamani, 15:9 Rum 3:29; Mt 9:8; 2Sam 22:50; Za 18:49pia ili watu wa Mataifa wamtukuze Mungu kwa rehema zake. Kama ilivyoandikwa:

“Kwa hiyo nitakutukuza katikati ya watu wa Mataifa;

nitaliimbia sifa jina lako.”

15:10 Kum 32:43Tena yasema,

“Enyi watu wa Mataifa, furahini

pamoja na watu wa Mungu.”

15:11 Za 117:1Tena,

“Msifuni Bwana, ninyi watu wa Mataifa wote,

na kumwimbia sifa, enyi watu wote.”

15:12 Ufu 5:5; Isa 11:10; Mt 12:21Tena Isaya anasema,

“Shina la Yese litachipuka,

yeye atakayeinuka ili kutawala juu ya mataifa.

Watu wa Mataifa watamtumaini.”

15:13 Rum 14:17; 1Kor 4:20Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Read More of Warumi 15