Warumi 11:11-32 NEN

Warumi 11:11-32

Matawi Yaliyopandikizwa

11:11 Mdo 13:46; Rum 10:19; 11:1Hivyo nauliza tena: Je, Waisraeli walijikwaa ili waanguke na kuangamia kabisa? La, hasha! Lakini kwa sababu ya makosa yao, wokovu umewafikia watu wa Mataifa, ili kuwafanya Waisraeli waone wivu. 11:12 Rum 11:25Basi ikiwa kukosa kwao kumekuwa utajiri mkubwa kwa ulimwengu, tena kama kuangamia kwao kumeleta utajiri kwa watu wa Mataifa, kurudishwa kwao kutaleta utajiri mkuu zaidi.

11:13 Mdo 9:15Sasa ninasema nanyi watu wa Mataifa. Maadamu mimi ni mtume kwa watu wa Mataifa, naitukuza huduma yangu 11:14 1Kor 10:33; 1The 2:16; Mt 1:21; Lk 2:11ili kuwafanya watu wangu waone wivu na hivyo kuwaokoa baadhi yao. 11:15 Rum 5:10; Lk 15:24, 32Kwa kuwa ikiwa kukataliwa kwao ni kupatanishwa kwa ulimwengu, kukubaliwa kwao si kutakuwa ni uhai baada ya kufa? 11:16 Law 23:10, 17; Hes 15:18-21Kama sehemu ya donge la unga uliotolewa kuwa limbuko ni mtakatifu, basi unga wote ni mtakatifu, nalo shina kama ni takatifu, vivyo hivyo na matawi nayo.

11:17 Yer 11:16; Yn 15:2; Mdo 2:39; Efe 2:11-13Lakini kama baadhi ya matawi yalikatwa, nawe chipukizi la mzeituni mwitu ukapandikizwa mahali pao ili kushiriki unono pamoja na matawi mengine kutoka shina la mzeituni, 11:18 Yn 4:22; 1Kor 10:12basi usijivune juu ya hayo matawi. Kama ukijivuna, kumbuka jambo hili: si wewe unayelishikilia shina, bali ni shina linalokushikilia wewe. Basi utasema, “Matawi yale yalikatwa ili nipate kupandikizwa katika hilo shina.” 11:20 1Kor 10:12; 2Kor 1:24; Rum 12:16; 1Tim 6:17; 1Pet 1:17Hii ni kweli. Matawi hayo yalikatwa kwa sababu ya kutokuamini kwake, lakini wewe umesimama tu kwa sababu ya imani. Kwa hiyo usijivune, bali simama kwa kuogopa. Kwa maana kama Mungu hakuyahurumia matawi ya asili, wala hatakuhurumia wewe.

11:22 Rum 2:4; Ebr 3:6; Yn 15:2Angalia basi wema na ukali wa Mungu: Kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, kama utadumu katika wema wake. La sivyo, nawe utakatiliwa mbali. 11:23 2Kor 3:16Wao nao wasipodumu katika kutokuamini kwao, watapandikizwa tena kwenye shina, kwa maana Mungu anao uwezo wa kuwapandikiza tena kwenye hilo shina. 11:24 Yer 11:16Ikiwa wewe ulikatwa kutoka kile ambacho kwa asili ni mzeituni mwitu na kupandikizwa kinyume cha asili kwenye mzeituni uliopandwa, si rahisi zaidi matawi haya ya asili kupandikizwa tena kwenye shina lake la mzeituni!

Israeli Wote Wataokolewa

11:25 Rum 1:13; 1Kor 10:1; 12:1; 2Kor 1:8; 1The 4:13; Rum 12:16; Lk 21:24Ndugu zangu, ili msije mkajidai kuwa wenye hekima kuliko mlivyo, nataka mfahamu siri hii: Ugumu umewapata Israeli kwa sehemu hadi idadi ya watu wa Mataifa watakaoingia itimie. 11:26 Isa 45:17; Yer 31:34Hivyo Israeli wote wataokolewa. Kama ilivyoandikwa:

“Mkombozi atakuja kutoka Sayuni;

ataondoa kutokumcha Mungu katika Yakobo.

11:27 Isa 59:20, 21; 27; 9; Ebr 8:10, 12Hili ndilo agano langu nao

nitakapoziondoa dhambi zao.”

11:28 Rum 5:10; Kum 7:8; 10:15; Rum 9:5Kwa habari ya Injili, wao ni adui wa Mungu kwa ajili yenu, lakini kuhusu kule kuteuliwa kwao ni wapendwa, kwa ajili ya mababa zao wa zamani, 11:29 Rum 8:28; Ebr 7:21kwa maana akishawapa watu karama, Mungu haziondoi, wala wito wake. 11:30 Efe 2:2; Kol 3:7Kama vile ninyi wakati fulani mlivyokuwa waasi kwa Mungu lakini sasa mmepata rehema kwa sababu ya kutokutii kwao, hivyo nao Waisraeli wamekuwa waasi ili kwamba wao nao sasa waweze kupata rehema kwa ajili ya rehema za Mungu kwenu. 11:32 Rum 3:9; Gal 3:22; 1Tim 2:4Kwa maana Mungu amewafunga wanadamu wote kwenye kuasi ili apate kuwarehemu wote.

Read More of Warumi 11