Warumi 10:5-21, Warumi 11:1-10 NEN

Warumi 10:5-21

Wokovu Ni Kwa Ajili Ya Wote

Mose anaandika kuhusu haki ile itokanayo na sheria, kwamba, “Mtu atendaye matendo hayo ataishi kwa hayo.” 10:6 Rum 9:30; Kut 30:12Lakini ile haki itokanayo na imani husema hivi: “Usiseme moyoni mwako, ‘Ni nani atakayepanda mbinguni?’ ” (yaani ili kumleta Kristo chini) 10:7 Kum 30:13; Mdo 2:24“au ‘Ni nani atashuka kwenda kuzimu?’ ” (yaani ili kumleta Kristo kutoka kwa wafu.) 10:8 Kum 30:14Lakini andiko lasemaje? “Lile neno liko karibu nawe, liko kinywani mwako na moyoni mwako,” yaani, lile neno la imani tunalolihubiri. 10:9 Mt 10:32; Lk 12:8; Mdo 2:24Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba “Yesu ni Bwana,” na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini na hivyo kuhesabiwa haki, tena kwa kinywa mtu hukiri na hivyo kupata wokovu. 10:11 Isa 28:16; Mt 28:18; Mdo 10:36Kama yasemavyo Maandiko, “Yeyote amwaminiye hataaibika kamwe.” Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani, yeye ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao. 10:13 Mdo 2:21; Yoe 2:32Kwa maana, “Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokolewa.”

10:14 Tit 1:3Lakini watamwitaje yeye ambaye hawajamwamini? Nao watawezaje kumwamini yeye ambaye hawajamsikia? Tena watamsikiaje bila mtu kuwahubiria? 10:15 Isa 52:7Nao watahubirije wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, “Tazama jinsi ilivyo mizuri miguu yao wale wanaohubiri habari njema!”

10:16 Isa 53:1Lakini si wote waliotii Habari Njema. Kwa maana Isaya asema, “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?” 10:17 Gal 3:2, 5; Kol 3:16Basi, imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo. 10:18 Za 19:4; Mt 24:14Lakini nauliza: Je, wao hawakusikia? Naam, wamesikia, kwa maana:

“Sauti yao imeenea duniani pote,

nayo maneno yao yameenea

hadi miisho ya ulimwengu.”

10:19 Rum 11:11, 14; Kut 32:21Nami nauliza tena: Je, Waisraeli hawakuelewa? Kwanza, Mose asema,

“Nitawafanya mwe na wivu

kwa watu wale ambao si taifa.

Nitawakasirisha kwa taifa

lile lisilo na ufahamu.”

10:20 Isa 65:1; Rum 9:20Naye Isaya kwa ujasiri mwingi anasema,

“Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta.

Nilijifunua kwa watu

wale ambao hawakunitafuta.”

10:21 Isa 65:2; Yer 35:17Lakini kuhusu Israeli anasema,

“Mchana kutwa nimewanyooshea

watu wakaidi na wasiotii mikono yangu.”

Read More of Warumi 10

Warumi 11:1-10

Mabaki Ya Israeli

11:1 Law 26:46; Za 94:14; 2Kor 11:22; Flp 3:5Basi nauliza: Je, Mungu amewakataa watu wake? La, hasha! Mimi mwenyewe ni Mwisraeli, tena uzao wa Abrahamu kutoka kabila la Benyamini. 11:2 Rum 8:29; 11:1; 1Fal 19:10, 14Mungu hajawakataa watu wake, ambao yeye aliwajua tangu mwanzo. Je, hamjui yale Maandiko yasemayo kuhusu Eliya, jinsi alivyomlalamikia Mungu kuhusu Israeli? 11:3 1Fal 19:10, 14Alisema, “Bwana, wamewaua manabii wako na kuzibomoa madhabahu zako, nimebaki mimi peke yangu, nao wanataka kuniua?” 11:4 1Fal 19:18Je, Mungu alimjibuje? “Nimejibakizia watu elfu saba ambao hawajapiga magoti kumwabudu Baali.” 11:5 Rum 9:27; 3:24Vivyo hivyo pia, sasa wapo mabaki waliochaguliwa kwa neema ya Mungu. 11:6 Rum 4:4; Gal 3:18Lakini ikiwa wamechaguliwa kwa neema, si tena kwa msingi wa matendo. Kama ingekuwa kwa matendo, neema isingekuwa neema tena.

11:7 Rum 9:31; 9:18Tuseme nini basi? Kile kitu ambacho Israeli alikitafuta kwa bidii hakukipata. Lakini waliochaguliwa walikipata. Waliobaki walifanywa wagumu, 11:8 Mt 13:13-15; Kum 29:4; Isa 29:10kama ilivyoandikwa:

“Mungu aliwapa bumbuazi la mioyo,

macho ili wasiweze kuona,

na masikio ili wasiweze kusikia,

hadi leo.”

11:9 Za 69:22, 23; 35:8Naye Daudi anasema:

“Karamu zao na ziwe tanzi na mtego wa kuwanasa,

kitu cha kuwakwaza waanguke, na adhabu kwao.

11:10 Za 69:22, 23; Rum 11:8Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona,

nayo migongo yao iinamishwe daima.”

Read More of Warumi 11