Ufunuo 8:1-13, Ufunuo 9:1-12 NEN

Ufunuo 8:1-13

Lakiri Ya Saba Na Chetezo Cha Dhahabu

8:1 Ufu 6:1Mwana-Kondoo alipoivunja ile lakiri ya saba, pakawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa.

8:2 Ufu 9:1, 13; 11:15; Mt 24:31; Ufu 8:6-13Nami nikawaona wale malaika saba wanaosimama mbele za Mungu, nao wakapewa tarumbeta saba.

8:3 Ufu 7:2; 5:8; Kut 30:1-6; Ebr 9:4Malaika mwingine aliyekuwa na chetezo cha dhahabu, akaja na kusimama mbele ya madhabahu. Akapewa uvumba mwingi ili autoe pamoja na maombi ya watakatifu wote, juu ya yale madhabahu ya dhahabu yaliyo mbele ya kile kiti cha enzi. 8:4 Za 141:2; Lk 1:10Ule moshi wa uvumba pamoja na yale maombi ya watakatifu, vikapanda juu mbele za Mungu, kutoka mkononi mwa huyo malaika. 8:5 Law 16:12-13; Ufu 4:5; 6:12Kisha yule malaika akachukua kile chetezo, akakijaza moto kutoka kwa yale madhabahu, akautupa juu ya dunia. Pakatokea sauti za radi, ngurumo, umeme wa radi na tetemeko la ardhi.

Tarumbeta Ya Kwanza

8:6 Ufu 8:2Basi wale malaika saba waliokuwa na zile tarumbeta saba wakajiandaa kuzipiga.

8:7 Eze 38:22; Ufu 9:15-18; 12:4; 9:4Malaika wa kwanza akaipiga tarumbeta yake, pakatokea mvua ya mawe na moto uliochanganyika na damu, navyo vikatupwa kwa nguvu juu ya nchi. Na theluthi ya dunia ikateketea, theluthi ya miti ikateketea, na nyasi yote mbichi ikateketea.

Tarumbeta Ya Pili

8:8 Yer 51:25; 16:3Malaika wa pili akaipiga tarumbeta yake na kitu kama mlima mkubwa unaowaka moto kikatupwa baharini. Theluthi ya bahari ikawa damu, 8:9 Ufu 8:7; 16:3theluthi ya viumbe vyenye uhai viishivyo baharini vikafa na theluthi ya meli zikaharibiwa.

Tarumbeta Ya Tatu

8:10 Isa 14:12; Ufu 9:1; 14:7; 16:4Malaika wa tatu akaipiga tarumbeta yake, na nyota kubwa iliyokuwa ikiwaka kama taa ikaanguka toka angani, ikaangukia theluthi ya mito na chemchemi za maji. 8:11 Yer 9:15; 23:15Nyota hiyo inaitwa Uchungu. Theluthi ya maji yakawa machungu na watu wengi wakafa kutokana na maji hayo kwa maana yalikuwa machungu.

Tarumbeta Ya Nne

8:12 Kut 10:21-23; Ufu 6:12-13Kisha malaika wa nne akaipiga tarumbeta yake, na theluthi ya jua, theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota zikapigwa. Kwa hiyo theluthi moja ya mwanga ikawa giza. Theluthi ya mchana ikawa haina mwanga na pia theluthi ya usiku.

8:13 Ufu 14:6; 19:17; 11:14; 12:12Nilipokuwa tena nikitazama, nikamsikia tai mmoja akipiga kelele kwa sauti kuu wakati akiruka katikati ya mbingu, akisema, “Ole! Ole! Ole wa watu waishio duniani, kwa sababu ya tarumbeta ambazo malaika hao wengine watatu wanakaribia kuzipiga!”

Read More of Ufunuo 8

Ufunuo 9:1-12

Tarumbeta Ya Tano

9:1 Ufu 8:10; Lk 8:31Malaika wa tano akaipiga tarumbeta yake, nami nikaona nyota iliyokuwa imeanguka toka angani hadi ardhini. Nyota hiyo ilipewa ufunguo wa lile Shimo.9:1 Yaani Abyss kwa Kiyunani; maana yake ni Kuzimu, yaani makao ya pepo wachafu. 9:2 Mwa 19:28; Kut 19:18; Yoe 2:2-10Alipolifungua hilo Shimo, moshi ukapanda kutoka humo kama moshi wa tanuru kubwa sana. Jua na anga vikatiwa giza na ule moshi uliotoka katika hilo Shimo. 9:3 Kut 10:12-15Ndipo katika ule moshi wakatoka nzige wakaenda juu ya nchi, nao wakapewa nguvu kama zile za nge wa duniani. 9:4 Ufu 7:2-3; 6:6; 8:7; Eze 9:4; Ufu 7:3Wakaambiwa wasidhuru nyasi ya nchi, wala mmea wala mti wowote, bali wawadhuru tu wale watu ambao hawana muhuri wa Mungu kwenye vipaji vya nyuso zao. 9:5 Ufu 9:3, 10Wakaruhusiwa kuwatesa kwa muda wa miezi mitano, lakini wasiwaue. Uchungu wa kuuma kwao ulikuwa kama ule wa mtu aumwapo na nge. 9:6 Ay 7:15; Ufu 6:16Katika siku hizo watu watatafuta kifo lakini hawatakiona, watatamani kufa, lakini kifo kitawakimbia.

9:7 Yoe 2:4; Dan 7:8Wale nzige walikuwa na umbo kama la farasi waliotayarishwa kwa ajili ya vita. Kwenye vichwa vyao kulikuwa na kitu kama taji za dhahabu na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu. 9:8 Yoe 1:6Walikuwa na nywele kama za wanawake, na meno yao yalikuwa kama ya simba. 9:9 Yoe 2:5Walikuwa na dirii kama za chuma, na sauti za mabawa yao zilikuwa kama ngurumo za farasi wengi na magari mengi yakikimbilia vitani. 9:10 Ufu 9:3, 5, 19Walikuwa na mikia yenye miiba ya kuumia kama nge. Nguvu yao ya kutesa watu kwa huo muda wa miezi mitano ilikuwa katika hiyo mikia yao. 9:11 Ufu 9:1, 2; Lk 8:31; 16:16; Ay 26:6; 28:22Walikuwa na mfalme wao, ambaye ni malaika wa lile Shimo, ambaye jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani ni Apolioni.9:11 Abadoni au Apolioni maana yake ni Mharabu, yaani Yule aharibuye.

9:12 Ufu 8:13Ole ya kwanza imepita, bado nyingine mbili zinakuja.

Read More of Ufunuo 9