Ufunuo 3:7-22 NEN

Ufunuo 3:7-22

Kwa Kanisa Lililoko Filadelfia

3:7 Yn 5:20; Isa 22:22; Mt 16:19“Kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika:

“Haya ndiyo maneno yake yeye aliye mtakatifu na wa kweli, yeye aliye na ufunguo wa Daudi. Anachokifungua hakuna awezaye kukifunga, wala anachokifunga hakuna awezaye kukifungua. 3:8 Mdo 14:27; Ufu 2:13Nayajua matendo yako. Tazama, nimeweka mbele yako mlango uliofunguliwa, wala hakuna awezaye kuufunga. Ninajua kwamba una nguvu kidogo lakini umelishika neno langu wala hukulikana Jina langu. 3:9 Ufu 2:9; Isa 49:23; 43:4Nitawafanya wale wa sinagogi la Shetani, wale ambao husema kuwa ni Wayahudi lakini sio, bali ni waongo, nitawafanya waje wapige magoti miguuni pako, na wakiri ya kwamba nimekupenda. 3:10 2Pet 2:9; Ufu 2:10; 11:10; 17:8Kwa kuwa umeshika amri yangu ya kuvumilia katika saburi, nitakulinda katika saa ya kujaribiwa inayokuja ulimwenguni pote, ili kuwajaribu wote wakaao duniani.

3:11 Ufu 2:25; Mt 16:27; Ufu 2:25; 1Kor 9:25“Ninakuja upesi. Shika sana ulicho nacho, ili mtu asije akaichukua taji yako. 3:12 Gal 2:9; Ufu 14:1; 22:4; 21:2-10Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo kamwe. Nitaandika juu yake Jina la Mungu wangu na jina la mji mkubwa wa Mungu wangu, Yerusalemu mpya, ambao unashuka kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Nami pia nitaandika juu yake Jina langu jipya. 3:13 Ufu 2:7Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa.

Kwa Kanisa Lililoko Laodikia

3:14 Kol 1:16-18“Kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika:

“Haya ndiyo maneno yake yeye aliye Amen, shahidi mwaminifu na wa kweli, mtawala wa uumbaji wote wa Mungu. 3:15 Rum 12:11Nayajua matendo yako, ya kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungelikuwa moja au lingine. Hivyo kwa kuwa u vuguvugu, si baridi wala moto, nitakutapika utoke kinywani mwangu. 3:17 Hos 12:8; 1Kor 4:8Kwa maana unasema: ‘Mimi ni tajiri, nimejilimbikizia mali, wala sihitaji kitu chochote.’ Lakini hutambui ya kwamba wewe ni mnyonge, wa kuhurumiwa, maskini, kipofu, tena uliye uchi. 3:18 Ufu 16:15Nakushauri ununue kutoka kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, ili upate kuwa tajiri, na mavazi meupe ili uyavae upate kuficha aibu ya uchi wako, na mafuta ya kupaka macho yako ili upate kuona.

3:19 Kum 8:5; 1Kor 11:32; Ufu 2:5“Wale niwapendao, ninawakemea na kuwaadibisha. Hivyo uwe na bidii ukatubu. 3:20 Mt 24:33; Lk 12:36; Yn 14:23Tazama! Nasimama mlangoni nabisha. Kama mtu yeyote akisikia sauti yangu na kufungua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye, naye pamoja nami.

3:21 Mt 19:28; Ufu 5:5“Yeye ashindaye nitampa haki ya kuketi pamoja nami kwenye kiti changu cha enzi, kama vile mimi nilivyoshinda na nikaketi pamoja na Baba yangu kwenye kiti chake cha enzi. 3:22 Ufu 2:7Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa.”

Read More of Ufunuo 3