Ufunuo 2:18-29, Ufunuo 3:1-6 NEN

Ufunuo 2:18-29

Kwa Kanisa Lililoko Thiatira

2:18 Ufu 1:11-15“Kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika:

“Haya ndiyo maneno ya Mwana wa Mungu, ambaye macho yake ni kama mwali wa moto na ambaye miguu yake ni kama shaba iliyosuguliwa sana. 2:19 Ufu 2:2Nayajua matendo yako, upendo wako na imani yako, huduma na saburi yako na kwamba matendo yako ya sasa yamezidi yale ya kwanza.

2:20 1Fal 21:25; 2Fal 9:7“Hata hivyo, nina neno dhidi yako: Unamvumilia yule mwanamke Yezebeli ambaye anajiita nabii, lakini anawafundisha na kuwapotosha watumishi wangu ili wafanye uasherati na kula vyakula vilivyotolewa kafara kwa sanamu. 2:21 Rum 2:4; Ufu 9:20Nimempa muda ili atubu kwa ajili ya uasherati wake, lakini hataki. 2:22 Ufu 17:2; 18:9Kwa hiyo nitamtupa kwenye kitanda cha mateso, na nitawafanya hao wanaozini naye kupata mateso makali wasipotubia njia zake. 2:23 1Sam 16:7; Yer 11:20Nami nitawaua watoto wake. Nayo makanisa yote yatajua kwamba Mimi ndiye nichunguzaye mioyo na nia, na kwamba nitamlipa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. 2:24 Mdo 15:28Basi nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, ninyi ambao hamyafuati mafundisho ya Yezebeli, wala hamkujifunza hayo yanayoitwa mambo ya ndani sana ya Shetani (sitaweka mzigo mwingine wowote juu yenu): 2:25 Ufu 3:11Lakini shikeni sana mlicho nacho, mpaka nitakapokuja.

2:26 Za 2:8; Ufu 3:21“Atakayeshinda na kutenda mapenzi yangu mpaka mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa:

2:27 Ufu 12:5; Za 2:9; Yer 19:11“ ‘Atawatawala kwa fimbo ya chuma,

atawavunja vipande vipande

kama chombo cha udongo’:

kama vile mimi nilivyopokea mamlaka kutoka kwa Baba yangu. 2:28 Ufu 22:16Nami nitampa pia ile nyota ya asubuhi. Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa.

Read More of Ufunuo 2

Ufunuo 3:1-6

Kwa Kanisa Lililoko Sardi

3:1 Ufu 1:4; 1:16; 2:2; 1Tim 5:6“Kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika:

“Haya ndiyo maneno ya aliye na zile Roho saba3:1 Roho saba za Mungu hapa inamaanisha Roho wa Mungu katika ukamilifu wa utendaji wake. za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya kuwa hai, lakini umekufa. 3:2 Eze 34:4Amka! Nawe uyaimarishe yale yaliyosalia na yaliyo karibu kufa, kwa maana sikuona kwamba kazi zako zimekamilika machoni pa Mungu wangu. 3:3 Ufu 2:5; 2Pet 3:10Kumbuka basi yale uliyoyapokea na kuyasikia, yatii na ukatubu. Lakini usipoamka, nitakuja kama mwizi wala hutajua saa nitakayokuja kwako.

3:4 Yud 23; Ufu 6:11“Lakini bado una watu wachache katika Sardi ambao hawajayachafua mavazi yao. Wao wataenda pamoja nami, wakiwa wamevaa mavazi meupe, kwa maana wanastahili. 3:5 Ufu 20:12; Mt 10:32Yeye ashindaye atavikwa vazi jeupe kama wao. Sitafuta jina lake kutoka kitabu cha uzima, bali nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu na mbele za malaika wake. 3:6 Ufu 2:7Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa.

Read More of Ufunuo 3