Ufunuo 2:1-17 NEN

Ufunuo 2:1-17

Kwa Kanisa Lililoko Efeso

2:1 Ufu 1:16; 1:12-13“Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika:

“Haya ndiyo maneno ya yule aliyezishika zile nyota saba katika mkono wake wa kuume na ambaye hutembea kati ya vile vinara saba vya taa vya dhahabu. 2:2 1Yn 4:1; 2Kor 11:13Nayajua matendo yako, bidii yako na saburi yako. Najua kuwa huwezi kuvumiliana na watu waovu na ya kwamba umewajaribu wale wanaojifanya kuwa mitume na kumbe sio, nawe umewatambua kuwa ni waongo. 2:3 Yn 15:21Umevumilia na kustahimili taabu kwa ajili ya Jina langu, wala hukuchoka.

2:4 Yer 2:2; Mt 24:12“Lakini nina neno dhidi yako: Umeuacha upendo wako wa kwanza. 2:5 Ufu 1:20Kumbuka basi ni wapi ulikoangukia! Tubu na ukafanye matendo yale ya kwanza. Kama usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa kutoka mahali pake. 2:6 Ufu 2:15; Za 139:21Lakini una jambo hili kwa upande wako: Unayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo nami pia nayachukia.

2:7 Mt 11:15; Ufu 13:9; Mwa 2:9; Ufu 22:2, 14; Lk 23:43“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa haki ya kula matunda toka kwa mti wa uzima, ambao uko katika paradiso2:7 Paradiso hapa ina maana ya Bustani, yaani shamba dogo la miti izaayo matunda. ya Mungu.

Kwa Kanisa Lililoko Smirna

2:8 Ufu 1:11-13“Kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika:

“Haya ndiyo maneno yake yeye aliye wa Kwanza na wa Mwisho, aliyekufa kisha akafufuka. 2:9 Yak 2:5; Ufu 3:9; Mt 4:10Naijua dhiki yako na umaskini wako, lakini wewe ni tajiri! Nayajua masingizio ya wale wasemao kuwa ni Wayahudi lakini sio, bali wao ni sinagogi la Shetani. 2:10 Ufu 3:10; Dan 1:12-14Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuambia ibilisi atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.

2:11 Ufu 20:6-14; 21:8“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatadhuriwa kamwe na mauti ya pili.

Kwa Kanisa Lililoko Pergamo

2:12 Ufu 1:11-16; 1:17, 18; 2:7“Kwa malaika wa Kanisa lililoko Pergamo andika:

“Haya ndiyo maneno yake yeye aliye na upanga mkali wenye makali kuwili. 2:13 Ufu 14:12Ninajua unakoishi, ni kule ambako Shetani ana kiti chake cha enzi. Lakini umelishika Jina langu. Wala hukuikana imani yako kwangu hata katika siku za shahidi wangu mwaminifu Antipa, ambaye aliuawa katika mji mkuu wenu, ambako ndiko anakoishi Shetani.

2:14 1Pet 2:15; 1Kor 6:13“Hata hivyo, nina mambo machache dhidi yako: Unao watu wafuatao mafundisho ya Balaamu, yule aliyemfundisha Balaki kuwashawishi Waisraeli watende dhambi kwa kula vitu vilivyotolewa kafara kwa sanamu na kufanya uasherati. 2:15 Ufu 2:6Vivyo hivyo unao wale wayashikayo mafundisho ya Wanikolai. 2:16 2The 2:8Basi tubu! Ama sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga wa kinywa changu.

2:17 Yn 6:49-50; Isa 62:2; Ufu 19:12“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa. Nitampa pia jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.

Read More of Ufunuo 2