Ufunuo 19:11-21 NEN

Ufunuo 19:11-21

Aliyepanda Farasi Mweupe

19:11 Ufu 6:2; 3:14; Kut 15:3Kisha nikaona mbingu imefunguka na hapo mbele yangu akiwepo farasi mweupe, ambaye yeye aliyempanda aliitwa Mwaminifu na Kweli. Yeye huhukumu kwa haki na kufanya vita. 19:12 Ufu 1:14; 6:2; 2:17Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa chake kuna taji nyingi. Ana jina lililoandikwa ambalo hakuna mtu yeyote anayelijua isipokuwa yeye mwenyewe. 19:13 Isa 63:2, 3; Yn 1:1Amevaa joho lililochoviwa katika damu, na Jina lake ni “Neno la Mungu.” 19:14 Ufu 19:8; 3:4; 17:14Majeshi ya mbinguni walikuwa wakimfuata, wakiwa wamepanda farasi weupe, hali wamevaa mavazi ya kitani safi, nyeupe na nzuri. 19:15 Ufu 1:16; 12:5; 14:20; Isa 11:4; 2The 2:8; Za 2:9Kinywani mwake hutoka upanga mkali ambao kwa huo atayaangusha mataifa. “Atayatawala kwa fimbo yake ya utawala ya chuma.” Hulikanyaga shinikizo la mvinyo wa ghadhabu ya Mungu Mwenyezi. 19:16 Ufu 17:14; 19:12; 1Tim 6:15Kwenye joho lake na paja lake pameandikwa jina hili:

Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana.

Mnyama Na Majeshi Yake Yashindwa

19:17 Ufu 8:13; Eze 39:17Nami nikamwona malaika amesimama ndani kwenye jua, akaita ndege wote warukao angani kwa sauti kuu, “Njooni, kusanyikeni kwa ajili ya karamu kubwa ya Mungu, 19:18 Eze 39:18-20ili mpate kula nyama ya wafalme na ya majemadari, ya mashujaa, ya farasi na ya wapanda farasi, nyama ya wanadamu, wote walio huru na watumwa, wadogo na wakubwa.”

19:19 Ufu 16:14, 16Kisha nikamwona yule mnyama na wafalme wa dunia pamoja na majeshi yao wakiwa wamekusanyika pamoja ili kufanya vita dhidi ya yule aliyempanda farasi pamoja na jeshi lake. 19:20 Ufu 16:13; 13:12; Dan 7:11; Ufu 21:8; 14:19Lakini yule mnyama akakamatwa pamoja na huyo nabii wa uongo ambaye alikuwa amefanya ishara kwa niaba ya huyo mnyama, ambaye kwa ishara hizi aliwadanganya wale waliopokea chapa ya huyo mnyama na kuiabudu sanamu yake. Hawa wawili wakatupwa wakiwa hai ndani ya ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti. Wale waliosalia waliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa yule aliyekuwa amempanda farasi nao ndege wote wakajishibisha kwa nyama yao.

Read More of Ufunuo 19