Ufunuo 18:17-24, Ufunuo 19:1-10 NEN

Ufunuo 18:17-24

18:17 Ufu 17:16; Eze 27:28-30Katika muda wa saa moja utajiri wote mkubwa

kama huu umeangamia!’

“Kila nahodha, na wote wasafirio kwa meli, na wote wapatao kipato chao kutokana na bahari, watasimama mbali. 18:18 Eze 27:32; Ufu 13:4Watakapouona moshi wa kuungua kwake watalia wakisema, ‘Je, kulipata kuwako mji mkubwa kama huu?’ 18:19 Eze 27:30; Ufu 17:16Nao watajirushia mavumbi vichwani mwao, huku wakilia na kuomboleza, wakisema:

“ ‘Ole! Ole, ee mji mkubwa,

mji ambao wote wenye meli baharini

walitajirika kupitia kwa mali zake!

Katika saa moja tu ameangamizwa!

18:20 Yer 51:48; Ufu 12:12; 19:2Furahia kwa ajili yake, ee mbingu!

Furahini watakatifu, mitume na manabii!

Mungu amemhukumu

kwa vile alivyowatendea ninyi.’ ”

18:21 Ufu 5:2; Yer 51:63Kisha malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe kubwa kama la kusagia akalitupa baharini akisema:

“Hivyo ndivyo mji mkubwa Babeli

utakavyotupwa chini kwa nguvu

wala hautaonekana tena.

18:22 Isa 24:8; Eze 26:13; Yer 25:10Nyimbo za wapiga vinubi na waimbaji,

wapiga filimbi na wapiga tarumbeta

kamwe hazitasikika tena ndani yako.

Ndani yako kamwe hataonekana tena fundi

mwenye ujuzi wa aina yoyote.

Wala sauti ya jiwe la kusagia

kamwe haitasikika tena.

18:23 Yer 16:9; 25:10; Isa 23:8; Nah 3:4Mwanga wa taa

hautaangaza ndani yako tena.

Sauti ya bwana arusi na bibi arusi

kamwe haitasikika ndani yako tena.

Wafanyabiashara wako walikuwa watu maarufu wa dunia.

Mataifa yote yalipotoshwa kwa uchawi wako.

18:24 Ufu 16:6; 17:6; Yer 51:49Ndani yake ilionekana damu ya manabii na ya watakatifu

na wote waliouawa duniani.”

Read More of Ufunuo 18

Ufunuo 19:1-10

Shangwe Huko Mbinguni

19:1 Ufu 11:15; 7:10; 4:11Baada ya haya nikasikia sauti kama ya umati mkubwa mbinguni wakipiga kelele wakisema:

“Haleluya!

Wokovu na utukufu na uweza ni vya Mungu wetu,

19:2 Kum 32:43; Ufu 6:10kwa maana hukumu zake

ni za kweli na za haki.

Amemhukumu yule kahaba mkuu

aliyeuharibu ulimwengu kwa uzinzi wake.

Mungu amemlipiza kisasi

kwa ajili ya damu ya watumishi wake.”

19:3 Isa 34:10; Ufu 14:11Wakasema tena kwa nguvu:

“Haleluya!

Moshi wake huyo kahaba unapanda juu

milele na milele.”

19:4 Ufu 4:4-6; 5:14Wale wazee ishirini na wanne pamoja na wale viumbe wanne wenye uhai wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu, aliyekuwa ameketi kwenye kile kiti cha enzi. Wakasema kwa sauti kuu:

“Amen, Haleluya!”

19:5 Za 134:1; Ufu 11:18Kisha sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi, ikisema:

“Msifuni Mungu wetu,

ninyi watumishi wake wote,

ninyi nyote mnaomcha,

wadogo kwa wakubwa!”

19:6 Ufu 11:15Kisha nikasikia sauti kama ya umati mkubwa, kama sauti ya maji mengi yaendayo kasi na kama ngurumo kubwa ya radi wakipiga kelele wakisema:

“Haleluya!

Kwa maana Bwana Mungu wetu Mwenyezi anatawala.

19:7 Mt 25:10; Efe 5:32; Ufu 21:2, 9Tufurahi, tushangilie

na kumpa utukufu!

Kwa maana arusi ya Mwana-Kondoo imewadia

na bibi arusi wake amejiweka tayari.

19:8 Ufu 15:4; 19:14; 15:6; Isa 61:10; Eze 44:17; Zek 3:4Akapewa kitani safi, nyeupe

inayongʼaa, ili avae.”

(Hiyo kitani safi inawakilisha matendo ya haki ya watakatifu.)

19:9 Ufu 1:19; Lk 14:15; Ufu 21:5; 22:6Ndipo malaika akaniambia, “Andika: ‘Wamebarikiwa wale walioalikwa kwenye karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo!’ ” Naye akaongeza kusema, “Haya ndiyo maneno ya kweli ya Mungu.”

19:10 Ufu 22:8; Mdo 10:25, 26; Ufu 22:9; 12:17Ndipo nikaanguka kifudifudi miguuni pake ili kumwabudu, lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi pia ni mtumishi mwenzako pamoja na ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Mwabudu Mungu! Maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.”

Read More of Ufunuo 19