Zaburi 94:12-23 NEN

Zaburi 94:12-23

94:12 Ay 5:17; Kum 8:3; 1Kor 11:32; Mit 3:11; Ebr 12:5; 1Sam 12:23Ee Bwana, heri mtu anayeadhibishwa na wewe,

mtu unayemfundisha kwa sheria yako,

94:13 Za 86:7; 7:15; 55:23unampa utulivu siku za shida,

mpaka shimo litakapokuwa limechimbwa

kwa ajili ya mwovu.

94:14 Kum 31:6; Za 37:28; Rum 11:2; 1Sam 12:22; 1Fal 6:13; Yer 31:37Kwa kuwa Bwana hatawakataa watu wake,

hatauacha urithi wake.

94:15 Za 97:2; 7:10; 11:2; 36:10Hukumu itasimamishwa tena kwenye haki,

wote walio na mioyo minyofu wataifuata.

94:16 Hes 10:35; Isa 14:22; Za 17:13; 59:2Ni nani atakayeinuka dhidi ya mwovu kwa ajili yangu?

Ni nani atakayenikinga dhidi ya watenda maovu?

94:17 Za 124:2; 31:17Kama Bwana asingelinisaidia upesi,

ningelikuwa ninaishi katika ukimya wa kifo.

94:18 Kum 32:35; Ay 12:5Niliposema, “Mguu wangu unateleza,”

Ee Bwana, upendo wako ulinishikilia.

94:19 Mhu 11:10; Ay 6:10Wakati wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu,

faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu.

94:20 Za 58:2; Isa 10:1; 2Kor 6:14; Amo 6:3; Yer 22:30; 36:30Je, kiti cha utawala wa udhalimu kitajiunga nawe,

ule utawala uletao taabu kutokana na sheria zake?

94:21 Za 56:6; 106:38; Mit 17:15, 26; 28:21; Isa 5:20, 23; Mt 27:1, 4; Mwa 18:23; Mit 17:15; Kut 23:7Huungana kuwashambulia wenye haki,

kuwahukumu kufa wasio na hatia.

94:22 Za 18:2; 61:2; 2Sam 22:3Lakini Bwana amekuwa ngome yangu,

na Mungu wangu amekuwa mwamba ninaoukimbilia.

94:23 Za 37:38; 145:20; 54:5; 9:5; Mit 2:22; Kut 32:34Yeye atawalipa kwa ajili ya dhambi zao

na atawaangamiza kwa ajili ya maovu yao;

Bwana Mungu wetu atawaangamiza.

Read More of Zaburi 94