Zaburi 92:1-15
Zaburi 92
Wimbo Wa Kumsifu Mungu
Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato.
92:1 Za 27:6; 147:1; 135:3Ni vyema kumshukuru Bwana
na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,
92:2 Za 55:17kuutangaza upendo wako asubuhi,
na uaminifu wako wakati wa usiku,
92:3 Za 71:22; 1Sam 10:5; Neh 12:27; Za 33:2; 81:2kwa zeze yenye nyuzi kumi
na kwa sauti ya kinubi.
92:4 Za 5:11; 27:6; 8:6; 111:7; 143:5Ee Bwana, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha,
nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako.
92:5 Ay 36:24; Ufu 15:3; Za 40:5; 139:17; Isa 28:29; 31:2; Rum 11:33Ee Bwana, tazama jinsi yalivyo makuu matendo yako,
tazama jinsi yalivyo ya kina mawazo yako!
92:6 Za 73:22Mjinga hafahamu,
mpumbavu haelewi,
92:7 Ay 21:7; Yer 12:1; Mal 3:15; Za 37:1ingawa waovu huchipua kama majani
na wote watendao mabaya wanastawi,
wataangamizwa milele.
Bali wewe, Ee Bwana,
utatukuzwa milele.
92:9 Za 45:5; 68:1; 89:10Ee Bwana, hakika adui zako,
hakika adui zako wataangamia.
Wote watendao mabaya watatawanyika.
92:10 Za 89:17; 29:6; 89:10Umeitukuza pembe92:10 Pembe inawakilisha nguvu. yangu kama ile ya nyati dume,
mafuta mazuri yamemiminwa juu yangu.
92:11 Za 54:7; 91:8Macho yangu yamewaona adui zangu wakishindwa,
masikio yangu yamesikia maangamizi ya adui zangu waovu.
92:12 Za 72:7; 1:3; 52:8; Yer 17:8; Hos 14:6; Wim 7:7Wenye haki watastawi kama mtende,
watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni,
92:13 Isa 60:21; Mt 15:13; Yn 15:2, 5; Za 135:2waliopandwa katika nyumba ya Bwana,
watastawi katika nyua za Mungu wetu.
92:14 Za 1:3; Yn 15:2Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda,
watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu,
92:15 Ay 34:10wakitangaza, “Bwana ni mkamilifu;
yeye ni Mwamba wangu,
na ndani yake hamna uovu.”