Zaburi 91:9-16 NEN

Zaburi 91:9-16

Kama ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako:

naam, Bwana ambaye ni kimbilio langu,

91:10 Mit 1:33; 12:21; 2The 3:3; 2Pet 2:9basi hakuna madhara yatakayokupata wewe,

hakuna maafa yataikaribia hema yako.

91:11 Mwa 32:1; Ebr 1:14; Lk 4:10; Za 34:7; Mt 4:6Kwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako,

wakulinde katika njia zako zote.

91:12 Lk 1:10, 11; Ay 5:23; Mt 4:6; Za 37:24Mikononi mwao watakuinua,

ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.

91:13 Dan 6:22; Lk 10:19Utawakanyaga simba na nyoka wakali,

simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu.

91:14 1Sam 2:30; Yn 12:26; Ay 22:27; Za 18:3; Yer 33:3; Zek 13:9; Ebr 5:7Bwana asema, “Kwa kuwa ananipenda, nitamwokoa;

nitamlinda, kwa kuwa analikiri Jina langu.

91:15 Za 43:2; 1Sam 2:30Ataniita, nami nitamjibu;

nitakuwa pamoja naye katika taabu,

nitamwokoa na kumheshimu.

91:16 Kum 6:2; Za 21:4; 50:23Kwa siku nyingi nitamshibisha

na kumwonyesha wokovu wangu.”

Read More of Zaburi 91