Zaburi 91:1-8 NEN

Zaburi 91:1-8

Zaburi 91

Mungu Mlinzi Wetu

91:1 Kut 33:2; Isa 49:2; Mao 4:20; Za 63:7Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana,

atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.91:1 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania.

91:2 Za 9:9; 91:9; 2Sam 22:2, 3Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu,

Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.”

91:3 Za 124:7; Mit 6:5; 1Fal 8:37Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji,

na maradhi ya kuambukiza ya kuua.

91:4 Za 61:4; 17:8; 35:2; Rum 2:12; Kum 32:10; Isa 27:3; 31:5; Zek 12:8Atakufunika kwa manyoya yake,

chini ya mbawa zake utapata kimbilio,

uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako.

91:5 Ay 5:21; 5:19; Mit 3:23; Isa 43:2Hutaogopa vitisho vya usiku,

wala mshale urukao mchana,

wala maradhi ya kuambukiza

yanayonyemelea gizani,

wala tauni iharibuyo adhuhuri.

Ijapo watu elfu wataangukia kando yako,

kumi elfu mkono wako wa kuume,

lakini haitakukaribia wewe.

91:8 Za 37:34; 58:10; Mal 1:5Utatazama tu kwa macho yako

na kuona adhabu ya waovu.

Read More of Zaburi 91