Zaburi 9:7-12
9:7 Mik 5:2; Ufu 19:6; Ebr 1:11; Hab 1:12; Za 90:2; 1Nya 16:31Bwana anatawala milele,
ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu.
9:8 Za 7:11; 11:7; 45:6; 72:29:8 Kum 33:27; 2Sam 22:3; Za 10:18; 32:7; 74:21; 121:7Mungu atahukumu ulimwengu kwa haki,
atatawala mataifa kwa haki.
Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa,
ni ngome imara wakati wa shida.
9:10 Mwa 28:15; Kum 4:31; Za 22:1; 37:25; 71:11; 70:4; 91:14; Isa 49:14; Yer 15:18; Ebr 13:5; Yn 17:3; 2Kor 4:6; 1Yn 2:3, 4; 2Tim 1:12Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe,
kwa maana wewe Bwana,
hujawaacha kamwe wakutafutao.
9:11 Za 7:17; 2:6; 57:9; 18:49; 44:11; 105:1; 106:27; Isa 24:13; Eze 20:23; 1Tim 3:16Mwimbieni Bwana sifa, amefanywa mtawala Sayuni,
tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda.
9:12 2Sam 4:11; Za 10:17; 22:24; Isa 49:13Kwa maana yeye alipizaye kisasi cha damu hukumbuka,
hapuuzi kilio cha wanaoonewa.