Zaburi 9:13-20 NEN

Zaburi 9:13-20

9:13 Hes 10:9; Za 3:7; 18:3; 6:2; 41:4; 51:1; 86:3, 16; 119:132; Ay 17:16; Mt 16:18Ee Bwana, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa!

Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti,

9:14 2Fal 19:21; Isa 1:8; 10:32; 37:22; 62:11; Yer 4:31; 6:2; Mao 1:6; Mt 21:5; Mik 1:13; Sef 3:14; Zek 2:10; Yn 12:15ili niweze kutangaza sifa zako

katika malango ya Binti Sayuni

na huko niushangilie wokovu wako.

9:15 Ay 4:8; Za 35:7, 8; 57:6Mataifa wameanguka kwenye shimo walilolichimba,

miguu yao imenaswa kwenye wavu waliouficha.

9:16 Kut 7:5; Mt 5:22Bwana anajulikana kwa haki yake,

waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao.

9:17 Hes 16:30; Mt 5:5; Za 50:22; Ay 8:13; Hos 2:13; Yer 2:32Waovu wataishia kuzimu,

naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.

9:18 Za 25:3; 39:7; 71:5; Mt 23:18; Yer 14:8, 12; Za 74:19; 12:5; Flp 1:20Lakini mhitaji hatasahaulika siku zote,

wala matumaini ya walioonewa hayatapotea.

9:19 2Nya 14:11; Za 3:7; 110:6; Isa 2:4; Yoe 3:12Ee Bwana, inuka, usimwache binadamu ashinde.

Mataifa na yahukumiwe mbele zako.

9:20 Mwa 35:5; Isa 13:8; Lk 21:26; Za 31:13; 62:9; Isa 31:3; Eze 28:2Ee Bwana, wapige kwa hofu,

mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu.

Read More of Zaburi 9