Zaburi 89:9-13 NEN

Zaburi 89:9-13

89:9 Za 65:7; Ay 38:11; Nah 1:4; Mt 8:26Wewe unatawala bahari yenye msukosuko;

wakati mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza.

89:10 Ay 9:13; Za 59:11; 68:1; 92:9; Isa 30:9Wewe ulimponda Rahabu89:10 Rahabu hapa ina maana jina la Misri kwa fumbo, yaani mwenye majivuno (lakini sio Rahabu wa Yos 2).

kama mmojawapo wa waliochinjwa;

kwa mkono wako wenye nguvu,

uliwatawanya adui zako.

89:11 Kum 10:14; Za 24:1; 115:6; 1Nya 29:11; Mwa 1:1Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako,

uliuwekea ulimwengu msingi

pamoja na vyote vilivyomo.

89:12 Yos 19:22; Kum 3:8; 4:48; Za 98:8; Yos 12:1; Amu 4:6Uliumba kaskazini na kusini;

Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha.

89:13 Yos 4:24Mkono wako umejaa uwezo;

mkono wako una nguvu,

mkono wako wa kuume umetukuzwa.

Read More of Zaburi 89