Zaburi 89:46-52 NEN

Zaburi 89:46-52

89:46 Za 79:5Hata lini, Ee Bwana? Utajificha milele?

Ghadhabu yako itawaka kama moto hata lini?

89:47 Mwa 47:9; Ay 7:7; Za 39:5; 1Pet 1:24Kumbuka jinsi maisha yangu yanavyopita haraka.

Ni kwa ubatili kiasi gani umemuumba mwanadamu!

89:48 Mwa 5:24; Za 22:29; Ebr 11:5Ni mtu gani awezaye kuishi na asione kifo,

au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi?89:48 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

89:49 2Sam 7:12; Isa 55:13Ee Bwana, uko wapi upendo wako mkuu wa mwanzoni,

ambao katika uaminifu wako ulimwapia Daudi?

89:50 Za 69:19Bwana kumbuka jinsi mtumishi wako amesimangwa,

jinsi ninavyovumilia moyoni mwangu dhihaka za mataifa yote,

89:51 Za 74:10dhihaka ambazo kwazo adui zako

wamenisimanga, Ee Bwana,

ambazo kwazo wamesimanga

kila hatua ya mpakwa mafuta wako.

89:52 Za 41:13; 72:19Msifuni Bwana milele!

Amen na Amen.

Read More of Zaburi 89