Zaburi 89:38-45 NEN

Zaburi 89:38-45

89:38 1Nya 28:9; Isa 22:5; Mao 2:2Lakini wewe umemkataa, umemdharau,

umemkasirikia sana mpakwa mafuta wako.

89:39 Mao 5:16Umelikana agano lako na mtumishi wako,

na umeinajisi taji yake mavumbini.

89:40 Za 80:12; Isa 22:5; Mao 2:2Umebomoa kuta zake zote,

na ngome zake zote umezifanya kuwa magofu.

89:41 Amu 2:14; Za 44:13Wote wapitao karibu wamemnyangʼanya mali zake;

amekuwa dharau kwa jirani zake.

89:42 Za 13:2; 80:6Umeutukuza mkono wa kuume wa adui zake,

umewafanya watesi wake wote washangilie.

89:43 Za 44:10Umegeuza makali ya upanga wake,

na hukumpa msaada katika vita.

Umeikomesha fahari yake,

na kukiangusha kiti chake cha enzi.

89:45 Za 39:5; 44:15; 109:29Umezifupisha siku za ujana wake,

umemfunika kwa vazi la aibu.

Read More of Zaburi 89