Zaburi 89:30-37
89:30 2Sam 7:14; Yer 9:13“Kama wanae wataacha amri yangu
na wasifuate sheria zangu,
kama wakihalifu maagizo yangu
na kutoshika amri zangu,
89:32 2Sam 7:14nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo,
uovu wao kwa kuwapiga,
89:33 2Sam 7:15lakini sitauondoa upendo wangu kwake,
wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe.
89:34 Hes 23:19Mimi sitavunja agano langu
wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka.
89:35 Za 110:4; Ebr 6:13, 17; Amo 4:2; 8:7Mara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu,
nami sitamdanganya Daudi:
89:36 Za 89:4; 2Sam 7:18; Lk 1:33; Yn 12:34kwamba uzao wake utaendelea milele,
na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua;
89:37 Yer 31:35; 33:20, 21kitaimarishwa milele kama mwezi,
shahidi mwaminifu angani.”