Zaburi 89:19-29 NEN

Zaburi 89:19-29

Ulizungumza wakati fulani katika maono,

kwa watu wako waaminifu, ukasema:

“Nimeweka nguvu kwa shujaa,

nimemwinua kijana miongoni mwa watu.

89:20 Mdo 13:22; Za 78:70; Kut 29:7; 1Fal 1:39; 1Sam 2:35; 2Sam 22:51Nimemwona Daudi, mtumishi wangu,

na nimemtia mafuta yangu matakatifu.

89:21 Za 89:13; 18:35Kitanga changu kitamtegemeza,

hakika mkono wangu utamtia nguvu.

89:22 Amu 3:15; 2Sam 7:10Hakuna adui atakayemtoza ushuru,

hakuna mtu mwovu atakayemwonea.

89:23 Za 18:40; 2Sam 7:9Nitawaponda adui zake mbele zake

na kuwaangamiza watesi wake.

89:24 2Sam 7:15; Za 61:7Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye,

kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa.

89:25 Za 72:8Nitauweka mkono wake juu ya bahari,

mkono wake wa kuume juu ya mito.

89:26 Za 62:2; Yer 3:4; 2Sam 7:14; 22:47; 1Nya 22:10; Yn 5:17; Ebr 1:5Naye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu,

Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’

89:27 Kol 1:18; Hes 24:7; Za 2:6, 7; Ufu 1:5; 19:16Nitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza,

aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia.

89:28 Za 89:33-34; Isa 55:3Nitadumisha upendo wangu kwake milele,

na agano langu naye litakuwa imara.

89:29 Isa 9:7; Yer 33:17; Dan 7:14; Kum 11:21; Za 89:4, 36Nitaudumisha uzao wake milele,

kiti chake cha enzi kama mbingu zinavyodumu.

Read More of Zaburi 89