Zaburi 89:14-18 NEN

Zaburi 89:14-18

89:14 Za 97:2; 85:10, 11Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi;

upendo na uaminifu vinakutangulia.

89:15 Za 1:1; 44:3; Hes 10:10Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe,

wanaotembea katika mwanga

wa uwepo wako, Ee Bwana.

89:16 Za 30:4; 105:3Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa,

wanafurahi katika haki yako.

89:17 Za 18:1, 24; 75:10; 92:10; 112:9; 148:14Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao,

kwa wema wako unatukuza pembe89:17 Pembe inawakilisha nguvu. yetu.

89:18 Hos 13:10; Za 18:2; 47:9; Isa 16:5; 33:17, 22Naam, ngao yetu ni mali ya Bwana,

na mfalme wetu mali ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.

Read More of Zaburi 89