Zaburi 88:9-18 NEN

Zaburi 88:9-18

88:9 Za 38:10; 5:2; 143:6; Ay 11:13nuru ya macho yangu

imefifia kwa ajili ya huzuni.

Ee Bwana, ninakuita kila siku,

ninakunyooshea wewe mikono yangu.

88:10 Za 6:5Je, wewe huwaonyesha wafu maajabu yako?

Je, wale waliokufa huinuka na kukusifu?

88:11 Za 30:9Je, upendo wako hutangazwa kaburini,

uaminifu wako katika Uharibifu?88:11 Yaani Abadon.

88:12 Ay 10:21; 31:12; Mhu 8:10Je, maajabu yako hujulikana mahali pa giza,

au matendo yako ya haki katika nchi ya usahaulifu?

88:13 Za 30:2; 5:3; 55:17; 119:147Lakini ninakulilia wewe, Ee Bwana, unisaidie;

asubuhi maombi yangu huja mbele zako.

88:14 Za 43:2; 13:1Ee Bwana, kwa nini unanikataa

na kunificha uso wako?

88:15 Dan 9:26; Za 9:12; 129:1; Yer 22:21; Eze 16:22; Hos 2:15; Isa 53:8; Ay 6:4; 18:11; 2Kor 4:8Tangu ujana wangu nimeteseka, nikakaribia kifo;

nimepatwa na hofu zako, nami nimekata tamaa.

88:16 Za 7:11; Ay 6:4Ghadhabu yako imepita juu yangu;

hofu zako zimeniangamiza.

88:17 Za 124:4Mchana kutwa zinanizunguka kama mafuriko;

zimenimeza kabisa.

88:18 Za 88:8; 38:11; Ay 19:13Umeniondolea marafiki na wapendwa wangu;

giza limekuwa ndilo rafiki yangu wa karibu kuliko wote.

Read More of Zaburi 88