Zaburi 88:1-9 NEN

Zaburi 88:1-9

Zaburi 88

Kilio Kwa Ajili Ya Kuomba Msaada

Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi leanothi. Utenzi wa Hemani Mwezrahi.

88:1 Za 51:14; 3:4; 22:2; Lk 18:7Ee Bwana, Mungu uniokoaye,

nimelia mbele zako usiku na mchana.

Maombi yangu yafike mbele zako,

utegee kilio changu sikio lako.

88:3 Ay 33:22; Isa 38:10; Za 6:3; 25:17; 107:18Kwa maana nafsi yangu imejaa taabu,

na maisha yangu yanakaribia kaburi.88:3 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

88:4 Za 31:12; 18:1Nimehesabiwa miongoni mwa wale waendao shimoni,

niko kama mtu asiye na nguvu.

88:5 Za 31:22Nimetengwa pamoja na wafu,

kama waliochinjwa walalao kaburini,

ambao huwakumbuki tena,

ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako.

88:6 Za 30:1; 69:15; Mao 3:55; Yon 2:3Umenitupa katika shimo lenye kina kirefu sana,

katika vina vya giza nene.

88:7 Za 7:11; 42:7Ghadhabu yako imekuwa nzito juu yangu,

umenigharikisha kwa mawimbi yako yote.

88:8 Ay 3:23; 19:13; Za 31:11; Yer 32:2; 33:1Umenitenga na rafiki zangu wa karibu

na kunifanya chukizo kwao.

Nimezuiliwa, wala siwezi kutoroka;

88:9 Za 38:10; 5:2; 143:6; Ay 11:13nuru ya macho yangu

imefifia kwa ajili ya huzuni.

Ee Bwana, ninakuita kila siku,

ninakunyooshea wewe mikono yangu.

Read More of Zaburi 88