Zaburi 86:11-17 NEN

Zaburi 86:11-17

86:11 Kut 33:13; 1Sam 12:23; Za 25:5; Eze 11:19; Za 26:3; Kum 6:24; Yer 24:7; 32:39; 1Kor 7:35Ee Bwana, nifundishe njia yako,

nami nitakwenda katika kweli yako;

nipe moyo usiositasita,

ili niweze kulicha jina lako.

86:12 Za 9:1Ee Bwana wangu, nitakusifu kwa moyo wote;

nitaliadhimisha jina lako milele.

86:13 Za 56:13; 116:8; 34:4; 49:15; 16:10Kwa maana upendo wako ni mkuu kwangu;

umeniokoa kutoka kwenye vilindi vya kaburi.86:13 Yaani Kuzimu.

86:14 Za 54:3Ee Mungu, wenye majivuno wananishambulia;

kundi la watu wakatili linatafuta uhai wangu:

watu wasiokuheshimu wewe.

86:15 Za 116:5; 103:8; 111:4; 145:8; 51:1; Hes 14:18; Za 86:5; Kut 34:6; Yoe 2:13; Neh 9:17Lakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema,

si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo na uaminifu.

86:16 Za 6:4; 9:13; 18:1; 116:16Nigeukie na unihurumie;

mpe mtumishi wako nguvu zako,

mwokoe mwana wa mtumishi wako wa kike.86:16 Au: mwokoe mwanao mwaminifu.

86:17 Kut 3:12; Mt 24:3; Yn 2:11Nipe ishara ya wema wako,

ili adui zangu waione nao waaibishwe,

kwa kuwa wewe, Ee Bwana,

umenisaidia na kunifariji.

Read More of Zaburi 86