Zaburi 84:8-12 NEN

Zaburi 84:8-12

84:8 Za 4:1Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, sikia maombi yangu;

nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo.

84:9 1Sam 16:6; Za 2:2; 59:11; 18:50; 132:17Ee Mungu, uitazame ngao yetu,

mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako.

84:10 1Nya 23:5Siku moja katika nyua zako ni bora

kuliko siku elfu mahali pengine;

afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu

kuliko kukaa katika mahema ya waovu.

84:11 Isa 60:19; Yer 43:13; Ufu 21:23; Mwa 15:1; Za 34:10Kwa kuwa Bwana ni jua na ngao,

Bwana hutoa wema na heshima;

hakuna kitu chema anachowanyima

wale ambao hawana hatia.

84:12 Za 2:12Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,

heri ni mtu yule anayekutumaini wewe.

Read More of Zaburi 84