Zaburi 84:1-7 NEN

Zaburi 84:1-7

Zaburi 84

Kuionea Shauku Nyumba Ya Mungu

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya wana wa Kora.

84:1 Kum 33:27; Za 27:4; 43:3; 90:1; 132:5; 26:8; 27:4; Ebr 9:23; Ufu 21:2, 3Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,

makao yako yapendeza kama nini!

84:2 Ay 19:27; Yos 3:10Nafsi yangu inatamani sana,

naam, hata kuona shauku,

kwa ajili ya nyua za Bwana;

moyo wangu na mwili wangu

vinamlilia Mungu Aliye Hai.

84:3 Za 2:6; 5:2; 43:4; Yer 44:11Hata shomoro amejipatia makao,

mbayuwayu amejipatia kiota

mahali awezapo kuweka makinda yake:

mahali karibu na madhabahu yako,

Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,

Mfalme wangu na Mungu wangu.

Heri wale wanaokaa nyumbani mwako,

wanaokusifu wewe daima.

84:5 Za 81:1; Yer 31:6Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako,

na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao.

84:6 Ay 38:26; Yoe 2:23Wanapopita katika Bonde la Baka,84:6 Yaani Bonde la Vilio.

hulifanya mahali pa chemchemi,

pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi.84:6 Au: baraka.

84:7 Ay 17:9; Kum 16:16; 1Fal 8:1Huendelea toka nguvu hadi nguvu,

hadi kila mmoja afikapo

mbele za Mungu huko Sayuni.

Read More of Zaburi 84