Zaburi 81:8-16 NEN

Zaburi 81:8-16

81:8 Za 50:7; 78:1“Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya:

laiti kama mngenisikiliza, ee Israeli!

81:9 Kut 20:3Hamtakuwa na mungu mgeni miongoni mwenu;

msimsujudie mungu wa kigeni.

81:10 Kut 6:6; 13:3; 29:46; Eze 2:8; Za 107:9; 37:3; Yn 13:7Mimi ni Bwana Mungu wako,

niliyekutoa nchi ya Misri.

Panua sana kinywa chako

nami nitakijaza.

81:11 Kut 32:1-6“Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza;

Israeli hakutaka kunitii.

81:12 Eze 20:25; Mdo 7:42; Rum 1:24Basi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao

wafuate mashauri yao wenyewe.

81:13 Kum 5:29; Isa 48:18; Yer 44:4, 5; Mt 23:37“Laiti kama watu wangu wangalinisikiliza,

kama Israeli wangalifuata njia zangu,

81:14 Za 47:3; Amo 1:8ningaliwatiisha adui zao kwa haraka,

na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao!

81:15 2Sam 22:45Wale wanaomchukia Bwana wangalinyenyekea mbele zake,

na adhabu yao ingedumu milele.

81:16 Kum 32:14Bali ninyi mngalilishwa ngano iliyo bora,

na kuwatosheleza kwa asali itokayo kwenye mwamba.”

Read More of Zaburi 81