Zaburi 80:1-7 NEN

Zaburi 80:1-7

Zaburi 80

Maombi Kwa Ajili Ya Kuponywa Kwa Taifa

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi za Agano.” Zaburi ya Asafu.

80:1 Kut 25:22; 1Sam 4:4; Za 77:20; 89:1; Kum 33:2Ee Mchungaji wa Israeli tusikie,

wewe umwongozaye Yosefu kama kundi;

wewe uketiye katika kiti cha enzi

katikati ya makerubi, angaza

80:2 Hes 2:18-24; Za 35:23; 54:1; 71:2; 109:26; 116:4; 119:94mbele ya Efraimu, Benyamini na Manase.

Uamshe nguvu zako,

uje utuokoe.

80:3 Za 71:20; 85:4; Yer 31:18; Mao 5:21; Hes 6:25; Za 80:7, 19; 1Fal 18:37Ee Mungu, uturejeshe,

utuangazie uso wako,

ili tuweze kuokolewa.

80:4 Za 74:10; Kum 29:20Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote,

hata lini hasira yako itawaka na kufoka moshi

dhidi ya maombi ya watu wako?

80:5 Ay 3:24; Isa 30:20Umewalisha kwa mkate wa machozi,

umewafanya wanywe machozi bakuli tele.

80:6 Za 79:4Tumekuwa chanzo cha ugomvi kwa jirani zetu,

na adui zetu wanatudhihaki.

80:7 Za 80:3Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe;

utuangazie uso wako,

nasi tuweze kuokolewa.

Read More of Zaburi 80