Zaburi 78:9-16 NEN

Zaburi 78:9-16

78:9 Za 78:57; 1Nya 12:2; Hos 7:16; Amu 20:39Watu wa Efraimu, ingawa walijifunga pinde,

walikimbia siku ya vita.

78:10 Yos 7:10; 2Fal 17:15; Kut 16:28; Yer 11:8Hawakulishika agano la Mungu

na walikataa kuishi kwa sheria yake.

78:11 Za 106:13; Isa 17:10; Yer 2:32Walisahau aliyokuwa ameyatenda,

maajabu aliyokuwa amewaonyesha.

78:12 Neh 9:17; Za 106:22; Kut 11:9; Hes 13:22; Mwa 32:3; Isa 19:11Alitenda miujiza machoni mwa baba zao,

huko Soani, katika nchi ya Misri.

78:13 Kut 14:21, 22; 15:8; Za 66:6; 136:13Aliigawanya bahari akawapitisha,

alifanya maji yasimame imara kama ukuta.

78:14 Kut 13:21; Za 105:39Aliwaongoza kwa wingu mchana

na kwa nuru kutoka kwenye moto usiku kucha.

78:15 Hes 20:11; 1Kor 10:4; Kut 17; 6; Za 105:41; Isa 41:18Alipasua miamba jangwani

na akawapa maji tele kama bahari,

78:16 Kum 9:21alitoa vijito kutoka kwenye jabali lililochongoka,

akayafanya maji yatiririke kama mito.

Read More of Zaburi 78