Zaburi 78:56-72 NEN

Zaburi 78:56-72

Lakini wao walimjaribu Mungu,

na kuasi dhidi ya Yeye Aliye Juu Sana,

wala hawakuzishika sheria zake.

78:57 2Nya 30:7; Za 78:9; Eze 20:27; Hos 7:16Kama baba zao, hawakuwa thabiti wala waaminifu,

wakawa wasioweza kutegemewa

kama upinde wenye kasoro.

78:58 Amu 2:12; Law 26:30; Kut 20:4; Kum 12:2; 5:8; 32:21; Hes 33:51Wakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia miungu,

wakachochea wivu wake kwa sanamu zao.

78:59 Za 55:19; Law 26:28; Hes 32:14; Kum 32:19; Ebr 4:13Wakati Mungu alipowasikia, alikasirika sana,

akamkataa Israeli kabisa.

78:60 Yos 18:1; Eze 8:6; 1Sam 4:11; Yer 7:12Akaiacha hema ya Shilo,

hema aliyokuwa ameiweka katikati ya wanadamu.

78:61 Amu 18:30; 1Sam 4:12; Za 132:8; 1Sam 4:17Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani,

utukufu wake mikononi mwa adui.

78:62 Kum 28:25; 1Sam 10:1Aliachia watu wake wauawe kwa upanga,

akaukasirikia sana urithi wake.

78:63 1Fal 4:32; Yer 7:32; 16:9; 25:10; Hes 11:1Moto uliwaangamiza vijana wao,

na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi,

78:64 Ay 27:15; 1Sam 4:17makuhani wao waliuawa kwa upanga,

wala wajane wao hawakuweza kulia.

78:65 Za 44:23; Isa 42:13Ndipo Bwana alipoamka kama vile kuamka usingizini,

kama vile mtu aamkavyo kutoka kwenye bumbuazi la mvinyo.

78:66 1Sam 5:6Aliwapiga na kuwashinda adui zake,

akawatia katika aibu ya milele.

78:67 Yer 7:15; Hos 9:13; 12:1Ndipo alipozikataa hema za Yosefu,

hakulichagua kabila la Efraimu,

78:68 Hes 1:7; Kut 15:17; Za 68:16; 108:8lakini alilichagua kabila la Yuda,

Mlima Sayuni, ambao aliupenda.

78:69 Za 15:1; 1Fal 6:1Alijenga patakatifu pake kama vilele,

kama dunia ambayo aliimarisha milele.

78:70 1Sam 16:1Akamchagua Daudi mtumishi wake

na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo.

78:71 Mwa 37:2; Za 28:9; 2Sam 5:2; 1Nya 11:2; Mik 5:2-4; Zek 11:4Kutoka kuchunga kondoo alimleta

kuwa mchungaji wa watu wake Yakobo,

wa Israeli urithi wake.

78:72 1Fal 9:4; Mwa 17:1Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo,

kwa mikono ya ustadi aliwaongoza.

Read More of Zaburi 78