Zaburi 78:32-39 NEN

Zaburi 78:32-39

78:32 Za 78:11, 17, 22Licha ya haya yote, waliendelea kutenda dhambi,

licha ya maajabu yake, hawakuamini.

78:33 Hes 14:29, 35Kwa hiyo akamaliza siku zao katika ubatili

na miaka yao katika vitisho.

78:34 Kum 4:29; Hos 5:15; Hes 5:15Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao,

waliosalia walimtafuta,

walimgeukia tena kwa shauku.

78:35 Mwa 49:24; Kum 9:26Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao,

kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao.

78:36 Eze 33:31Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao,

wakisema uongo kwa ndimi zao,

78:37 Za 78:8; Mdo 8:21mioyo yao haikuwa thabiti kwake,

wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.

78:38 Kut 34:6; Neh 9:17; Za 25:11; 85:2; 86:15; 1Fal 21:29; Isa 1:25; 27:9; 48:9, 10; 30:18; Mik 7:18; Rum 2:4; Dan 11:35Hata hivyo alikuwa na huruma,

alisamehe maovu yao

na hakuwaangamiza.

Mara kwa mara alizuia hasira yake,

wala hakuchochea ghadhabu yake yote.

78:39 Mwa 6:3; Isa 29:5; Ay 7:7; Yak 4:14; Yn 3:6Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu,

upepo upitao ambao haurudi.

Read More of Zaburi 78