Zaburi 78:17-31 NEN

Zaburi 78:17-31

78:17 Za 78:32Lakini waliendelea kutenda dhambi dhidi yake,

wakiasi jangwani dhidi ya Aliye Juu Sana.

78:18 Kut 15:24; 17:2; 1Kor 10:9; Hes 11:4Kwa makusudi walimjaribu Mungu,

wakidai vyakula walivyovitamani.

78:19 Hes 11:4; 21:5Walinena dhidi ya Mungu, wakisema,

“Je, Mungu aweza kuandaa meza jangwani?

78:20 Hes 20:11; Kut 17:6Alipopiga mwamba, maji yalitoka kwa nguvu,

vijito vikatiririka maji mengi.

Lakini je, aweza kutupa chakula pia?

Je, anaweza kuwapa watu wake nyama?”

78:21 Hes 11:1Bwana alipowasikia, alikasirika sana,

moto wake ukawa dhidi ya Yakobo,

na ghadhabu yake ikawaka dhidi ya Israeli,

78:22 Kum 1:32; Ebr 3:19; 3:10kwa kuwa hawakumwamini Mungu,

wala kuutumainia ukombozi wake.

78:23 Mwa 7:11; Kum 28:12; 2Fal 7:2Hata hivyo alitoa amri kwa anga zilizo juu

na kufungua milango ya mbingu,

78:24 Kut 16:4; Yn 6:31; Neh 9:15, 20; 1Kor 10:3akawanyeshea mana ili watu wale;

aliwapa nafaka ya mbinguni.

Watu walikula mkate wa malaika,

akawatumia chakula chote ambacho wangeliweza kula.

78:26 Hes 11:31Aliachia upepo wa mashariki kutoka kwenye mbingu

na kuuongoza upepo wa kusini kwa uwezo wake.

78:27 Kut 16:13; Hes 11:31Aliwanyeshea nyama kama mavumbi,

ndege warukao kama mchanga wa pwani.

Aliwafanya washuke ndani ya kambi yao,

kuzunguka mahema yao yote.

78:29 Hes 11:20Walikula na kusaza,

kwa maana alikuwa amewapa kile walichotamani.

78:30 Hes 11:33Kabla hawajamaliza kula walichokitamani,

hata kilipokuwa kingali bado vinywani mwao,

78:31 Isa 10:16hasira ya Mungu ikawaka juu yao,

akawaua wale waliokuwa na nguvu zaidi miongoni mwao,

akiwaangusha vijana wa Israeli.

Read More of Zaburi 78