Zaburi 74:18-23 NEN

Zaburi 74:18-23

74:18 Ufu 16:19; Kum 32:9Ee Bwana, kumbuka jinsi mtesi alivyokudhihaki,

jinsi watu wapumbavu walivyolitukana jina lako.

74:19 Mwa 8:8; Isa 59:11; Za 9:18Usiukabidhi uhai wa njiwa wako kwa wanyama wakali wa mwitu;

usisahau kabisa uhai wa watu wako wanaoteseka milele.

74:20 Mwa 6:18; 17:7; Law 26:44; Yer 33:21; Ay 34:22Likumbuke agano lako,

maana mara kwa mara mambo ya jeuri

yamejaa katika sehemu za giza nchini.

74:21 Isa 58:10; Za 9:9, 18; 10:18; 103:6; 35:10Usiruhusu walioonewa warudi nyuma kwa aibu;

maskini na wahitaji hebu walisifu jina lako.

74:22 Za 17:13; 53:1Inuka, Ee Mungu, ujitetee;

kumbuka jinsi wapumbavu

wanavyokudhihaki mchana kutwa.

74:23 Isa 31:4; Za 65:7; 46:6; Hes 25:17Usipuuze makelele ya watesi wako,

ghasia za adui zako, zinazoinuka mfululizo.

Read More of Zaburi 74