Zaburi 74:10-17 NEN

Zaburi 74:10-17

74:10 Za 6:3; 79:5; 80:4; 74:22; 44:16Ee Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini?

Je, adui watalitukana jina lako milele?

74:11 Kut 15:6; Neh 5:13; Eze 5:3Kwa nini unazuia mkono wako,

mkono wako wa kuume?

Uutoe kutoka makunjo ya vazi lako

na uwaangamize!

74:12 Za 2:6; 24:7; 68:24; 44:4Lakini wewe, Ee Mungu, ni mfalme wangu tangu zamani,

unaleta wokovu duniani.

74:13 Isa 51:9; 27:1; Eze 29:3; 32:2; Kut 14:21Ni wewe uliyeigawanya bahari kwa uweza wako;

ulivunja vichwa vya wanyama wakubwa wa kutisha katika maji.

74:14 Hes 14:9; Za 72:9; Ay 3:8; Isa 13:21; 23:13; 34:14; Yer 50:39Ni wewe uliyeponda vichwa vya Lewiathani74:14 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.

nawe ukamtoa kama chakula

kwa viumbe vya jangwani.

74:15 Kut 14:29; 17:6; Hes 20:11; Isa 11:16; Hab 3:9; Ufu 16:12; Yos 2:10Ni wewe uliyefungua chemchemi na vijito,

ulikausha mito ambayo ilikuwa ikitiririka daima.

74:16 Mwa 1:16; Za 136:7-9Mchana ni wako, nao usiku ni wako pia,

uliziweka jua na mwezi.

74:17 Mdo 17:26; Kum 32:8; Mwa 8:22Ni wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia,

ulifanya kiangazi na masika.

Read More of Zaburi 74